Mtazamo wangu kwa Media Tanzania: Waandishi Makanjanja nao ni Gamba Jingine

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Messages
1,025
Points
1,195

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2011
1,025 1,195
Mtazamo wangu kwa Media Tanzania: Waandishi Makanjanja nao ni Gamba Jingine

Kwa Muongo mmoja sasa naweza kukiri kuwa Tanzania tumepiga hatua kubwa sana katika sekta ya habari kutoka ukiritimba wa RTD na masafa yao ya Kati hadi masafa ya FM na hatimaye sasa kuelkea mfumo mpya wa Kidigitali.
Haitii shaka kuwa huu ni ushindi mkubwa katika sekta ya Habari Nchini ambapo uwekezaji huu uende sambamba na kuajiri waandishi wa Habari walioelimika na kupevuka katika maadili ya Tasnia hiyo.

Katika Kipindi hiki Taifa linahitaji MEDIA kufanya majukumu yake kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu na si mchezo huu wa kuigiza ninaouona katika media zetu, habari moja kila mwandishi anaonyesha ushabiki na mawazo yake bila kujali misingi na miiko ya Taaluma hiyo.

Media inaendeshwa kwa mfumo kama chama cha siasa, unakusanya wapambe ambao hawana hata taaluma wao kazi yao ni kupiga debe ili kuganga njaa, Taifa halihitaji waandishi wapiga Debe. Wanahitajika waandishi wadadisi wa mambo na wenye kuakisi mustkbali na majaaliwa ya Taifa na Utaifa.

Nasukumwa na haya baada ya kusikiliza Hotuba ya Jana ya JK masjid Gadaffi Dodoma, nilitarajia leo kila mwandishi ataibuka na Ushabiki wake na ndio limetokea leo.

MY TAKE:
  • Mgogoro ni nini? Owners mnapenda cheap na hamtaki kuajiri professionals au ni njaa iliyokithiri Sekta ya MEDIA Tanzania?
  • Hali hii ikifumbiwa macho tunaelekea Kubaya…Owners leteni mabadiliko sasa

ADIOS
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,187
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,187 2,000
ghost rider, hebu tusaidiane, hotuba si ulisikiliza na magazeti asubuhi hii umeyaona, kwa vile tayari ulishategemea kuona ushabiki na ni kweli umeouna sasa jee ungetaka uone tofauti gani?.
 
Mkuu Pasco, Nilitegemea interpretative Journalism ifanye kazi...Na wala haikuhitaji kukunja maneno na kuongeza moto zaidi katika kadhia hii (Jukumu jingine la media: Minimize harm not fueling chaotic moves) na walipaswa kufanya reflection kwenye sera na mifumo ya uendeshaji kubaini wapi accounatbility imekosekana hadi kutufikisha hapa.

Ombwe (vacum) ambayo wangeibaini ingekuwa story nzuri kusaidia Taifa kupiga hatua moja kwenda nyingine katika mikanganyiko hii zaidi ya kuendelea kumchonganisha Rais na Viongozi wa Dini...

Tumesikia...Rais Amjibu Pengo...WHY....JK awakatalia BAKWATA Ombi lao...Its Obvious (Wangeangalia TAKWIMU na suggestion alizozitoa katika kupitia randama ya LOWASA ya 1992...na kuonyesha Waislamu wanawezaje kunufaika na nafasi hiyo si kulalama. Ungekuwa msaada mzuri kwa Umma wa Kiislam na BAKWATA.
 
Doc

Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
38
Points
70

Doc

Member
Joined Aug 13, 2011
38 70
Hauwezi kutarajia mabadiliko kwenye sekta ambayo waajiri wao ndiyo haohao wanasiasa wakubwa nchini.
Huo ni ukweli, lazma kama ni gazet litakuma siku zote katika mlengo wa mwanasiasa mmiliki. Lakin je ina maana media zote zimeegamia upande fulani?
 
Doc

Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
38
Points
70

Doc

Member
Joined Aug 13, 2011
38 70
Mkuu Pasco, Nilitegemea interpretative Journalism ifanye kazi...Na wala haikuhitaji kukunja maneno na kuongeza moto zaidi katika kadhia hii (Jukumu jingine la media: Minimize harm not fueling chaotic moves) na walipaswa kufanya reflection kwenye sera na mifumo ya uendeshaji kubaini wapi accounatbility imekosekana hadi kutufikisha hapa.

Ombwe (vacum) ambayo wangeibaini ingekuwa story nzuri kusaidia Taifa kupiga hatua moja kwenda nyingine katika mikanganyiko hii zaidi ya kuendelea kumchonganisha Rais na Viongozi wa Dini...

Tumesikia...Rais Amjibu Pengo...WHY....JK awakatalia BAKWATA Ombi lao...Its Obvious (Wangeangalia TAKWIMU na suggestion alizozitoa katika kupitia randama ya LOWASA ya 1992...na kuonyesha Waislamu wanawezaje kunufaika na nafasi hiyo si kulalama. Ungekuwa msaada mzuri kwa Umma wa Kiislam na BAKWATA.
Lakin kaka kumbka pia hii ni biashara wakat huo huo.wakat mwngne vichwa vya habar vinawekwa katika muonekano wa kuweza kumvutia mnunuzi ila habar yenyew inakuwa na maelezo/uchambuzi unaokidhi..
 
Nsiande

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2009
Messages
1,649
Points
1,195

Nsiande

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2009
1,649 1,195
Nafikiri Ghost ryder u r expecting too much from our journalists, the journos are led by personalities and protecting who they currently support

Notwithstanding that, I have seen many editorials lacking even basic journalistic edge, yaani ofisini kwangu naletewa magazeti kama 6 na yote ninakuja kuyasomea nyumbani ili nisome kwa kutulia, lakini makosa mengine ...mpaka nimeishia kuomba waniletee Mwananchi, The East African na Dailynews tu, mengine ni kama yanasindikiza harusi

Gazeti la mwanahalisi juzi liliandika habari ya Barrick unaona 'kunakuwa na utalatibu...' Sasa jamani kama editor unapitisha hii habari bila hata ku correct kiswahili, u wonder about the entire content

Barrick inamiliki Geita, Bulyanhulu,Buzwagi na Tulawaka wakati GGM ni ya anglogold Ashanti, pengine hata kugoogle tu ili kupata undani wa makampuni haya hakuna, hapo wametoa habari ya wanaoumwa baada ya kuacha kazi, hakuna mahali walipocheki na uongozi wa Barrick HR ambapo labda waelezee exit medical zinafanyika kwa dhumuni lipi...sio kwamba natetea Barrick, ila uandishi mwingine ukiwa unaandika kulipua tuhuma jaribu kuonyesha u covered all angles na mwishoni onyesha ur take...

Anyways sijasomea uandishi but tht type of writing is best reserved for tabloids
 
ndetichia

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
27,723
Points
2,000

ndetichia

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
27,723 2,000
media zenyewe bongo zipo kwa ajili ya kujikomba kwa wanasiasa wewe unategemea nini zaidi ya kupotosha jamii.
kwa mfano uliowa kweli kuna dogo mmoja alipigwa na polisi bila ya hatia wakapelekea mpaka kifo cha huyo dogo halafu watu wamedia walipoambiwa wakaandika na kutangaza dogo ni jambazi wakati sio na baada ya kuchunguzi kumbe walipewa 10000 kila mtu alafu waandike kuwa dogo ni jambazi kuanzia hapo si polisi wala media wote hata waniaminishe vipi mi nawaona tu kama ma snitch..

ni hayo tu jombaa.
 
Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Messages
1,693
Points
1,500

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2009
1,693 1,500
Mtazamo wangu kwa Media Tanzania: Waandishi Makanjanja nao ni Gamba Jingine

Kwa Muongo mmoja sasa naweza kukiri kuwa Tanzania tumepiga hatua kubwa sana katika sekta ya habari kutoka ukiritimba wa RTD na masafa yao ya Kati hadi masafa ya FM na hatimaye sasa kuelkea mfumo mpya wa Kidigitali.
Haitii shaka kuwa huu ni ushindi mkubwa katika sekta ya Habari Nchini ambapo uwekezaji huu uende sambamba na kuajiri waandishi wa Habari walioelimika na kupevuka katika maadili ya Tasnia hiyo.

Katika Kipindi hiki Taifa linahitaji MEDIA kufanya majukumu yake kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu na si mchezo huu wa kuigiza ninaouona katika media zetu, habari moja kila mwandishi anaonyesha ushabiki na mawazo yake bila kujali misingi na miiko ya Taaluma hiyo.

Media inaendeshwa kwa mfumo kama chama cha siasa, unakusanya wapambe ambao hawana hata taaluma wao kazi yao ni kupiga debe ili kuganga njaa, Taifa halihitaji waandishi wapiga Debe. Wanahitajika waandishi wadadisi wa mambo na wenye kuakisi mustkbali na majaaliwa ya Taifa na Utaifa.

Nasukumwa na haya baada ya kusikiliza Hotuba ya Jana ya JK masjid Gadaffi Dodoma, nilitarajia leo kila mwandishi ataibuka na Ushabiki wake na ndio limetokea leo.

MY TAKE:
  • Mgogoro ni nini? Owners mnapenda cheap na hamtaki kuajiri professionals au ni njaa iliyokithiri Sekta ya MEDIA Tanzania?
  • Hali hii ikifumbiwa macho tunaelekea Kubaya…Owners leteni mabadiliko sasa

ADIOS
Usituletee uwongo hapa, magazeti karibu yote tz hasa ya kila siku yapo online. Ebu chukua gazeti unalodai limekengeuka na weka hapa tulijadili, siyo kulalamika kwa ujumla. Inaonesha wewe hukubaliani na taarifa ya JK wala siyo magazeti.

Toa mifano halisi,au sema gazeti fulani,tukuwekee sisi humu.

Punguza hasira,mkubwa amekwisha sema
 
Mathias Byabato

Verified Member
Joined
Nov 24, 2010
Messages
985
Points
250

Mathias Byabato

Verified Member
Joined Nov 24, 2010
985 250
Ndugu yangu ulichoandika ni upupu mtupu! Huna uhakika na usemacho; hebu nipe mfano kupitia magazeti haya:

Kuhusu hotuba ya JK, Nipashe/The Guardian yameandika hivi
Kuhusu Hotuba ya JK,Tanzania daima limeandika hivi
Kuhusu hotuba ya JK ,uhuru limeandika hivi
Kuhusu Hotuba ya JK,Mwananchi lemadika hivi
Kuhusu Hotiuba ya JK,Habarileo limeandika hivi

Hivyo nakuomba soma tena habari za magazeti hayo na rejea tena na hoja zako.

Note: Ni kinyume media kuandika maoni badala ya habari labda kupitia katika sehemu za maoni siyo katika news.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,187
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,187 2,000
Mkuu Pasco, Nilitegemea interpretative Journalism ifanye kazi...Na wala haikuhitaji kukunja maneno na kuongeza moto zaidi katika kadhia hii (Jukumu jingine la media: Minimize harm not fueling chaotic moves) na walipaswa kufanya reflection kwenye sera na mifumo ya uendeshaji kubaini wapi accounatbility imekosekana hadi kutufikisha hapa.

Ombwe (vacum) ambayo wangeibaini ingekuwa story nzuri kusaidia Taifa kupiga hatua moja kwenda nyingine katika mikanganyiko hii zaidi ya kuendelea kumchonganisha Rais na Viongozi wa Dini...

Tumesikia...Rais Amjibu Pengo...WHY....JK awakatalia BAKWATA Ombi lao...Its Obvious (Wangeangalia TAKWIMU na suggestion alizozitoa katika kupitia randama ya LOWASA ya 1992...na kuonyesha Waislamu wanawezaje kunufaika na nafasi hiyo si kulalama. Ungekuwa msaada mzuri kwa Umma wa Kiislam na BAKWATA.
GHOST RYDER, hapa sasa ndio umesema haswa ulichotakiwa kusema posti yako ya kwanza. Kwanza nakubaliana na wewe kuhusu udhaifu wa media zetu lakini hili la interpretive journalism kwa ajili ya kujenga na sio kubomoa, sikubaliani nawe, kazi ya media kujenga, ndio doctrine ya wana media wote waliosomea East, wale wa West kazi ya media ni ku push agenda zao forward hata ikibidi kubomoa na wanabomoa, na sasa hii ndio kazi ya tablod kazibu zote, wakiwemo Mwanahalisi na Raia Mwema.

Suala la Mahakama ya Kadhi kwa muda mrefu limekuwa ni suala tete ambayo CCM ililitumia katika ilani yake ya 2005 kuwa hoodwink Waislamu, na baada uya kuupata urais, 2010 wakalidrop. Juzi kwenye baraza la Iddi usifikiri JK amelizungumzia kwa kupenda, ameshurutishwa.

Kwa vile lilishazua mdadala tangu nyuma, vyombo vyetu vya habari ambavyo vinatakiwa kuwa neutral, karibu vyote vimetake side au pro, au against, hivyo kila vyombo vya pro, vitaiandika habari hiyo in affimative way na vile vya against vitairipoti in negative, ali muradi bora liende.

Kama hata Daily News wana side na serikali, unategemea nini kwa magazeti mengine?!.

Kesho nunua na gazeti la Al Huda na Al Noor uone yatakavyoripoti negative kwa vile wanataka mahakama hizi zigharimiwe na serikali!. Kama kuna magazeti uchonganishi ndio agenda yao, utakapoleta hoja upatanishi, unadhani kwao ni habari?.

No news is good news, jee wasomaji wanahitaji kusikia good news?. Magazeti yanawalisha wasomaji wake kile ambacho yanajua ndicho wanachotaka kula. Watanzania tunapenda zaidi majibu mepesi kwenye maswali magumu, ndio maana readership ya magazeti serious kama Citizen na Eastafrican ni low ukilinganisha na magazeti ya udaku ambayo sasa wameyabatiza jina "magazeti pendwa" .

Binafsi, siwalaumu waandishi wetu kwa sababu nime expiriance what does it make to be a journalist in Tanzania!.
 
GHOST RYDER

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Messages
1,025
Points
1,195

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2011
1,025 1,195
Lakin kaka kumbka pia hii ni biashara wakat huo huo.wakat mwngne vichwa vya habar vinawekwa katika muonekano wa kuweza kumvutia mnunuzi ila habar yenyew inakuwa na maelezo/uchambuzi unaokidhi..
Mkuu hakuna Biashara Nzuri kama ya kuandika ukweli uliotafitiwa na si compounded headline ambazo ukiisoma habari unagundua hakuna reflection ya Asilimia 100 kama headline inavyojionyesha.

Mfano: Serious paper kama Mwananchi linaandika headline kubwa '' Pengo Atema Cheche'' - kwanza umeondoa heshima yake maana kwa protokali za Roma huwezi kumtaja bila kuweka wadhifa wake Muadhama Polycarp Kardinali Pengo...Lakini tunajua mwenye asili ya kutema cheche ni Dragon. sasa kumlinganisha pengo na Dragon huu ni usanifu wa Lugha usiouwiana na Tabia za viumbe hawa wawili. Tena kwa serious paper kuvaa udaku huu wa lugha na kuifanya kuonekana ya kishabiki kulikochochewa na media kumewafikisha watanzania hapo kupenda habari za kada hiyo.

MEDIA bado ina uwezo wa kuwafnya watu kusoma habari za mlengo fulani wenye kuzingatia miiko na watu bado wakanunua tu magazeti bila shaka Mkuu.
 
GHOST RYDER

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Messages
1,025
Points
1,195

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2011
1,025 1,195
Ndugu yangu ulichoandika ni upupu mtupu! Huna uhakika na usemacho; hebu nipe mfano kupitia magazeti haya:

Kuhusu hotuba ya JK, Nipashe/The Guardian yameandika hivi
Kuhusu Hotuba ya JK,Tanzania daima limeandika hivi
Kuhusu hotuba ya JK ,uhuru limeandika hivi
Kuhusu Hotuba ya JK,Mwananchi lemadika hivi
Kuhusu Hotiuba ya JK,Habarileo limeandika hivi

Hivyo nakuomba soma tena habari za magazeti hayo na rejea tena na hoja zako.

Note: Ni kinyume media kuandika maoni badala ya habari labda kupitia katika sehemu za maoni siyo katika news.

Bahati nzuri nakubalika kwa kutoandika matusi na lugha za mtaani.

Nimemaliza utafiti wangu na kujiridhisha na nilichoandika, kazi hiyo fanya wewe kuniprove wrong. Am stand to be corrected halafu tuone aliyeandika upupu ni nani kati yetu

ADIOS
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,187
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,187 2,000
Nafikiri Ghost ryder u r expecting too much from our journalists, the journos are led by personalities and protecting who they currently support

Notwithstanding that, I have seen many editorials lacking even basic journalistic edge, yaani ofisini kwangu naletewa magazeti kama 6 na yote ninakuja kuyasomea nyumbani ili nisome kwa kutulia, lakini makosa mengine ...mpaka nimeishia kuomba waniletee Mwananchi, The East African na Dailynews tu, mengine ni kama yanasindikiza harusi

Gazeti la mwanahalisi juzi liliandika habari ya Barrick unaona 'kunakuwa na utalatibu...' Sasa jamani kama editor unapitisha hii habari bila hata ku correct kiswahili, u wonder about the entire content

Barrick inamiliki Geita, Bulyanhulu,Buzwagi na Tulawaka wakati GGM ni ya anglogold Ashanti, pengine hata kugoogle tu ili kupata undani wa makampuni haya hakuna, hapo wametoa habari ya wanaoumwa baada ya kuacha kazi, hakuna mahali walipocheki na uongozi wa Barrick HR ambapo labda waelezee exit medical zinafanyika kwa dhumuni lipi...sio kwamba natetea Barrick, ila uandishi mwingine ukiwa unaandika kulipua tuhuma jaribu kuonyesha u covered all angles na mwishoni onyesha ur take...

Anyways sijasomea uandishi but tht type of writing is best reserved for tabloids
Nsiande, hii fani ya uandishi wa habari siku hizi imevamiwa, hata wasio na wito ndio pen pushers wakuu, ukijumlisha na 'petty cash journalism' ndio usiseme.

Tanzania inabidi tufike mahali tuwe na specialization kwenye media zetu kwa wamiliki kuwalipa vizuri waandishi mahiri. Hawa kina Ben Mkapa, Dr, Mwakiyembe, Prof. Palamagamba Kabudi, Dr. Sengodo Mvungi, wote walikuwa waandishi, wa branch kwenye sheria, tukitegemea ndio wangerudi na kuimarisha sekta ya habari, wapi, wote walitokomea kwenye greener pasture.

Unajua huu ni mwaka wa tatu sasa Daily News halina Managing Editor?, aliyepo anakaimu tuu kisa mwenye sifa hajapatikana!.
 
Mathias Byabato

Verified Member
Joined
Nov 24, 2010
Messages
985
Points
250

Mathias Byabato

Verified Member
Joined Nov 24, 2010
985 250
Bahati nzuri nakubalika kwa kutoandika matusi na lugha za mtaani.

Nimemaliza utafiti wangu na kujiridhisha na nilichoandika, kazi hiyo fanya wewe kuniprove wrong. Am stand to be corrected halafu tuone aliyeandika upupu ni nani kati yetu

ADIOS
Hujanielewa! katika post no 3 nimekuwekea link za magazeti y akila siku y aleo namna yalivyoandika habari hiyo ebu gonga hizo link hapo kwenye post no 13 kisha niambie gazeti lipi limepotosha? siyo kuongea kwa ujumla.tunataka tujadili hoja moja kwa moja siyo tuhuma za uongo.
 
Vin Diesel

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2011
Messages
9,011
Points
2,000

Vin Diesel

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2011
9,011 2,000
Mkuu ni kweli kabisa kuwa media ya Tanzania inapwaya sana...habari nyingi zaandikwa kishabiki kwa faida ya mtu,kikundi,chama, au taasisi husika.
Mbaya zaidi sekta ya habari imevamiwa na watu wasio na weledi kabisa kwenye nyanja hii.
 
kibananhukhu

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2009
Messages
368
Points
195

kibananhukhu

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2009
368 195
What is news? News should include, 5WS + H, News worthiness, news elements. Nani, Kasema nini, wapi, lini, na kwa namna gani au kilichosemwa kimetokeaje? A journalist does not say. Should keep on reporting. Vitu kama habari ilikotokea, mhusika, uajabu, nk ni vya kuzingatia. Gazeti huandika habari za jana. Runinga ni lazima itoe habari za leo. Kinyume chake ni udhaifu.
Hata hivyo, ni sector gani inafanya vizuri Tanzania? Makandarasi zaidi ya elfu moja wamefukuzwa pamoja na mshauri elekezi wa barabara ya kila road. Ni wahandisi hao. Makanjanja ni nani?
Madaktari waliwahi pasua kichwa badala ya mguu, ni makanjanja na makaso mengi ya ajabu yanatokea mahospitalini na hayajulikani. Katika siasa kuna nini? Madactari kibao katika siasi lakini bado sijaridhika na utendaji. Leo dhahabu ni dola 1890 {Spot rate}, Wakati wawekezajia wanakuja na mikataba mingi imesainiwa wakati bei ya dhahabu ni dola 250. Lkn hata katika walipa kodi wakubwa hakuna kampuni ya madini hata moja. Bia na sigara wanaongoza pamoja na benki ya makabwela. NMB. Makanjanja ni Nani?

Tanzanite iliyonunuliwa mwaka 2000 na nchi 12 tu duniani, thamani yake ilikuwa sawa na mafuta yaliyouzwa na kuweit mwaka 2000. Pesa hiyo ingeliweza kuendesha Tanzania kwa miaka zaidi ya 20. Makanjanja ni nani. Nitatoa maoni zaidi baadaye.

Kuhusu makanjanja wa uandishi, wamejaribu, wameweza na wanasonga mbele. Biashara rasmi Tanzania ni asilimia 2 tu ndugu zangu. 98% ya biashara za Tanzania siyo rasmi na hazijulikani. Tuanze urasimishaji katika kila sector. Hayo yanahitaji utaratibu, uvumilivu na kuelemishana. Nipi tayari kuwaelimisha makanjanja wote Tanzania kwa gharama ndogo sana. Warasimishwe na wasilaaniwe.
 
Forum statistics

Threads 1,364,579
Members 520,767
Posts 33,320,767
Top