Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 7,802
- 20,759
Mimi binafsi sina chama, si kwa sababu nataka iwe ivyo, ni kwa sababu sijaona chama Tanzania chenye misimamo nayotaka mimi.
Rais Magufuli na Bunge:
Kwa mtazamo wangu nadhani si kwamba raisi Magufuli anapinga mhimili wa bunge, hili limedhihirishwa na mkataba alioingia Muheshimiwa Kangi Lugola. Kwa kauli yake kupinga mkataba ule Kwa kuwa haukushirikisha bunge wala serikali yake wala wizara nyingine husika Kama Wizara Ya Fedha. Nafikiri tu kwa raisi magufuli kukubali kupeleka mambo mengi ambayo anafanya sasa bungeni basi hayo mambo yangebaki kwenye ubishani yasingefanyika.
Kupeleka majadiliano bungeni inakuwa Kama mbwa ukimshika mkia hata afanye vipi atafanya unavyotaka wewe. Serikali yetu ingekuwa imeshikiliwa mkia ingebweka tu ila bunge lingekuwa linapoteza mda mwingi kwenye mabishano ya kisiasa yasiyo zaa matunda na mambo mengi yangesimama kama tulivyoona serikali zilizopita. Hapa tuna kubwa la kujifunza, kutokuwa Na uwiano mzuri kati ya serikali Na bunge.
Raisi Magufuli na Misimamo Yake Kisiasa:
Nakumbuka raisi Magufuli alivyoingia madarakani katika mambo aliyoyafanya mwanzo Ni kupinga siasa zisifanyike wakati uchaguzi umepita. Kwa wapinzani waliona Kama wananyimwa kuwa huru kisiasa kiasi cha kumwita Magufuli Ni ditekta. Upande wa pili kwa raisi Magufuli alipinga hili ili kupisha maendeleo yafanywe na wale viongozi waliochaguliwa, akisisitizia, siasa za majukwaa zimepita sasa waliochaguliwa wafanye siasa za ktekeleza yale waliyoyaimba kwenye majukwaa. Lakini kitu ambacho nakiwaza tu Ni kuwa raisi Magufuli aliruhusu waliochaguliwa wawe wapinzani au awe CCM anaruhusiwa kufanya siasa kwenye jimbo lake hususani madiwani Na wabunge.
Mimi binafsi niko wilaya ya Ubungo Na nimepita sana Pwani huko na hata mkoani Kilimanjaro ambapo ni nyumbani, lakini sijaona madiwani au wabunge walioita mikutano kujadili lipi lifanyike kuleta maendeleo (nimeuliza maeneo mengi ila hiki ndicho kinachoendelea). Nani kaenda kufanya mikutano ya hadhara kakataliwa kwenye jimbo lake?
Magufuli na Tundu Lisu:
Kwanza kabisa nasikitika Sana kwa mheshimiwa Tundu Lisu kupigwa risasi mchana kweupe na jambo hili kupelekwa kisiasa. Ila nimeona jambo ndani ya Mheshimiwa Tundu Lisu na chuki yake dhidi ya raisi Magufuli. Binafsi wanasiasa wanachukiana ila chuki zao ni za kisiasa wakiwa kwenye mziki wanacheza pamoja, binafsi sijui chuki hizi zililetwa na nini ila wao binafsi wanaelewa kindaki ndaki sio tunashabikia tu. Ila nasikitika sana kitendo cha mheshimiwa Tundu Lisu kwenda kuichafua Tanzania ili tusipewe misaada kwa chuki yake binafsi dhidi ya raisi, bila kujali anachikiomba anawaathiri vipi wa Tanzania.
Mheshimiwa Tundu Lissu anazunguka sehemu nyingi duniani kutaka wajitenge Na Tanzania wakati familia yake, ndugu zake Na ukoo wake wapo Tanzania. Amezunguka akiomba mabeberu watunyime misaada kitu ambacho hajui kingemuathiri kila mTanzania. Amediriki kukubaliana Na mabeberu tena nimesikitika Sana kusikia mheshimiwa Tundu Lisu akisapoti ushoga kabisa kwa mdomo wake mwenyewe na kuikandia serikali ya Tanzania ka kukataa ushiga ilihali anajua tamaduni hizi kwetu hazipo. Mbali na kuichafua Tanzania hao mabeberu bado wamekuwa mstari wa mbele kuleta misaada na kuikopesha Tanzania.
Mheshimiwa Tundu Lisu amekosa uzalendo kuhusu Tanzania juu ya chuki yake dhidi ya Magufuli. Kama alikuwa na mashtaka binafsi juu ya Magufuli sikatai ila hana ulazima wa kuichafua Tanzania na kuchinganisha na nchi rafiki, hata Magufuli akitoka madarakani uhusiano uliopo kati ya Tanzania na nchi nyingine utabaki, anapotaka kuuvuruga hata aje raisi mwingine lile doa litakuwepo tu ..
Raisi Magufuli hata Kama anayoyafanya analazimisha Kwa wananchi wa Tanzania na yatabaki kwa wananchi wa Tanzania. Hizo ndege si zake Ni za waTanzania, Na juhudi hizi zinaonekana ni za kujenga Tanzanua; huku Tundu Lisu anabomoa kile kinachojengwa kwa wa Tanzania. Tanzania inasonga mbele Kwa shida kwa raha ila inasonga mbele.
Siasa na Taaluma:
Kwa mtazamo wangu tu nchi yetu imeshindwa kutofautisha siasa na taaluma, hapo mwanzo tulikuwa tuko kwenye shimo dogo tu ila kwa sasa tuko kwenye shimo kubwa sana. Raisi Magufuli kwa kuchagua viongozi wenye taaluma zao kwa asilimia kubwa ameua nguvu nzito kwenye taaluma yetu. Kila m Tanzania sasa amekuwa mwanasiasa kitu ambacho kimekuwa sana katika utawala huu wa awamu ya tano. Ukienda chuoni, mashuleni, jeshini na maofisini watu wengi wamekuwa wanaacha taaluma zao na kuingia kwenye siasa. Baadhi ya viongozi au taaluma (mfano maprofesa, madokta, wanajeshi) ambao wamechaguliwa na raisi wetu wangeweza kuwa walimu wazuri wazalishe wanasiasa wazuri ila wameacha kuzalisha wanasiasa na wamekuwa ndio wanasiasa wakubwa. Sasa kumekuwa na taaluma mbovu kwa sababu ya siasa za kupita, ila manufaa ya taaluma si ya kupita.
Magufuli na Wananchi Wake:
Kwa mtazamo wangu kuna wananchi wanakubali Sana kazi na mwenendo wa serikali ya raisi Magufuli. Ila pia kuna wananchi wanachukia sana mwenendo wa serikali hii ya awamu ya tano kwa mitazamo yao mingi tu. La kusikitisha kipindi hiki cha miaka mitano wananchi wamepandikizwa chuki mbaya ambazo Ni kinyume Na utamaduni wetu Kama waTanzania. Chuki hizi zinaonekana mpaka baina ya ndugu Na ndugu huku watu wakiwa wamesahau siasa si chuki. Mfano tu humu ndani ya JF nimesoma nyuzi nyingi humu ndani watu wameshindwa kabisa kubishana kwa hoja majibu yao yanakuwa mfano “nenda kachukue buku saba lumbumba”, huku jukwaa hili la siasa likikosa sifa kabisa kwa kuwa na matusi mengi ambayo nashindwa kuyaandika hapa kwa maadili yangu yalivyo. Nahimiza tu watu wawe CCM, CHADEMA, au chama chochote kile siasa sio ‘Matusi’ “Hoja Hupingwa Kwa Hoja”
Siasa za Upinzani:
Kwa mtazamo wangu tu siasa zimebadilika Sana Kwa wapinzania Kwa sasa zile siasa za kusema tutajenga mashule, hospitali, barabara, tutaleta maji nk Kwa sasa hazisikiki. Nimekuwa najiuliza Sana Kwa nini hazisikiki? Nimegundua kuwa Kwa sasa vitu vingi vimejengwa au kuboreshwa Na serikali hii ya awamu ya Tano. Wapinzani wa raisi Magufuli kwa asilimia kubwa kazi zao zimekuwa ni kuponda tu huku huku hawawi mbele kusema kipi kifanyike. Kwa akili ya kawaida tu huwezi kuwa mmekaa kibarazani aje mwenye nyumba awaulize ‘mmekula nataka kuwaletea chakula’ alafu mmoja wenu ajibu “sie tumeshiba” huku mnakuta wengine wana njaa kali amewasemea bila kuwauliza kama wanahitaji kula. Kwa sasa siasa zimekita kwenye udikteta wa raisi Magufuli na kuponda yale anayofanya huku wakiwa hawasemi nini kifanyike tusonge mbele..
Kwa mtazamo wangu tu Wapinzani kuleta maendeleo si lazima wawe wamechaguliwa: Kwa jinsi nilivyoona wapinzani wakiwa msatri wa mbele kuomba michango ya kuwatoa wenzao gerezani au kuomba hela za hospitali za mheshimiwa Tundu Lisu basi wangeweza kutumia njia hizo hizo kukusanya michango kwa waTanzania ili kuleta maendeleo. Hata Kama hili lingepingwa wapinzani hawa wangeweza kuanzisha utaratibu Kwa viongozi waliowachaguliwa ndani ya upinzani kuleta maendeleo Kwa michango ya wananchi wenyewe ILA zingeonekana Ni juhudi zao ndio zimeleta maendeleo. Wapinzani wanaonekana kuwa wamesahau kabisa kuwa ‘Maendeleo Hayana Chama”
La mwisho ningependa sana kuona siku moja upinzani umeshika madaraka Tanzania ila si kwa upinzani huu naouona sasa. Na ningependa sana kuona CCM inavunjwa Na kuanzishwa chama kipya chenye wanasiasa mahiri wanaoweza kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania Kwa wananchi wake. Ningependelea sana kuona siasa zenye tija na maendeleo kwa waTanzania wote bila kujali wametokea vyama gani vya siasa. .