Mtazamo wangu kuhusu siasa za Tanzania na Rais Magufuli

Nina wasiwasi kama wapinzani walivyokuwa wanasema watajenga mashule, barabara, n.k ulikuwa unawaelewa.

Hata hivyo wapinzani, na wananchi, bila ushirikiano na serikali iliyopo madarakani peke yao ni vigumu sana kujenga hivyo vitu.

Hujawahi kusikia kauli " serikali haipeleki maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani?"

Sent using Jamii Forums mobile app
Linabaki pale pale upinzani ingeweza kuleta maendele kupitia wananchi, hawakuwa na haja ya kutumia pesa zao ila kwa kuchangisha pesa za wananchi
Najua unanielewa sana ila unataka kunibishia
Umeamini katika upinzani mda mrefu kupinga hili ina maana umepinga imani/hisia zako kwa mda mrefu
 
Samahani Mfiaukweli mataga ni nini?
Mimi sijasema Magu hana mapungufu yake mbona mnanipiga mawe, Magu sio Mungu
Tubishane kwa Hoja tu ila sio kelele

Nifundishe na mie nielewe ambacho unadhani sikielewi

Niambie hoja yako nikujibu. Ila ulichokiandika na nikakijibu is at the very best balderdash.
 
Lakini ndivyo mahakama zetu zilivyowahukumu. Na hakuna hukumu nyingine iliyoiua hukumu ya jaji Mihayo !!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli unachosema ila nabaki na msimamo ule ule kila mtu hata mtoto mdogo anajua ile kesi ilikuwa ya kutengenezwa na ndivyo nilivyosikia kwenye media. Nakumbuka Lowasa akiwa anagombea alihaidi kuwa atamtoa mzee seya na wanae

Ila kilichooneka ni kuwa mzee seya alishindwa ku prove kuwa hakufanya hivyo na ndicho kilichomfunga ila sio kuwa lifungwa kwa sababu amefanya hivyo. You get it?
 
Are you stupid or something? Otherwise utasemaje kuwa "watu wachache wana influence watu wengi"? Does it mean unakiri kuwa majority ya Watanzania ni mbumbumbu wasioweza kufikiri wenyewe hadi wawe influenced?

Siasa za wapinzani ni matusi, hakuna mpinzani aliyenijibu hapa bila kutukana
Unashangaa kuwa watu wako influenced na siasa???? serious? unavyotetea hapa upinzani are you not influenced? haijakuathiri? is that not the reason you are arguing?
 
Unaandika gazeti halafu ulichoandika ndani ni upuuzi mtupu.

Kwanini usingeandika huo upuuzi hata kwa sentensi walau moja tu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona umeandika maneno mengi kuonyesha kuwa nimeaandika upuuzi, kwa nini hukuandika sentensi moja lenye neni UPUUZI
Huna hoja, ungeweka hoja ya kupinga ningekuona una hoja umetaka tu useme maneno yenye sentensi moja inayimaanisha UPUUZI
 
Wewe umekubali kabisa Tundu Lisu alivyojibu wakati anahojiwa kuwa Tanzania ikubali ushoga?
Mimi nazungumzia siasa zake za Tundu Lisu kuichafua Tanzania, wewe unazungumzia Tundu Lisu kupigwa risasi vitu viwili tofauti ila ngoja nikuwekee uzi ambao kuna walichangia mada yako:

JE Tundu Anti Pasi LISU analichafua TAIFA au anaichafua SELIKARI?JE serikali ni Taifa?
Suala la Lissu kuanza kusakamwa anaichafua Tanzania ni baada ya yeye kuwa nje ya nchi na kuanza kuelezea madhila aliyofanyiwa, sasa kumbe na wewe ni miongoni mwa wale wachache mliomezeshwa sumu na CCM mkaamini Lissu anaichafua Tanzania.

Lissu sio kichaa atoke tu aanze kuisema vibaya serikali ya Magufuli ( tena hapa unielewe vizuri, serikali ya Magufuli sio Tanzania kama wewe na wenzako mnavyodhani) kama mkitaka kusifiwa watendeeni wengine vile mnavyopenda kutendewa nyie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujasoma nilichokiandika vizuri naomba ukasome tena

Nimeandika Upinzani kwa juhudi za kukusanya michango au kuwaleta wananchi pamoja wangeweza kuleta maendeleo mengi sana. Mfano wangeweza wakakusanya hela halafu wakanunua madawati, serikali ingekataa tu wananchi wangejua Upinzani unafanya kazi nyingi za kuleta maendeleo huku utawala unapinga huoni ingeleta tija kwa upinzani bila kutumia nguvu nyingi kushidana kwa kelele ambazo hazina msingi

Navyozungumza hivi naomba msininukuu vibaya mie napinga CCM kwa kuwa ni mbovu mno, hata viongozi wengi wanaochaguliwa ndani ya CCM na Magufuli wameonyesha udhaifu wa hali ya juu mbali na usomi wao .Ila vile vile napinga upinzani Pia kwa kunionyesha kuwa bado wanashindwa kuleta mabadiliko, hoja zao hata humu ndani ni matusi na kelele tu. .

..hujasikia Mh.Kishoa [ mbunge viti maalum] alikwenda kutoa msaada ktk shule mkoani Singida akazuiliwa? Na misaada ikakataliwa?
 
Linabaki pale pale upinzani ingeweza kuleta maendele kupitia wananchi, hawakuwa na haja ya kutumia pesa zao ila kwa kuchangisha pesa za wananchi
Najua unanielewa sana ila unataka kunibishia
Umeamini katika upinzani mda mrefu kupinga hili ina maana umepinga imani/hisia zako kwa mda mrefu
Nimekupa mfano wa Mbunge wa viti maalum CDM aliyepeleka sare za shule kwenye shule moja Singida but akakatazwa kuzigawa kwa wanafunzi, sijui bado unataka nikwambie kitu gani tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la Lissu kuanza kusakamwa anaichafua Tanzania ni baada ya yeye kuwa nje ya nchi na kuanza kuelezea madhila aliyofanyiwa, sasa kumbe na wewe ni miongoni mwa wale wachache mliomezeshwa sumu na CCM mkaamini Lissu anaichafua Tanzania.

Lissu sio kichaa atoke tu aanze kuisema vibaya serikali ya Magufuli ( tena hapa unielewe vizuri, serikali ya Magufuli sio Tanzania kama wewe na wenzako mnavyodhani) kama mkitaka kusifiwa watendeeni wengine vile mnavyopenda kutendewa nyie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Lisu sio kichaa mbona kasema mashoga wananyimwa haki zao Tanzania. Anasema ingetakiwa serikali itambue ushoga, hilo mbona hujibu????

Tanzania’s opposition leader who was shot 16 times and had 22 surgeries opens up about gay rights in Tanzania and challenging Magufuli
 
..hujasikia Mh.Kishoa [ mbunge viti maalum] alikwenda kutoa msaada ktk shule mkoani Singida akazuiliwa? Na misaada ikakataliwa?

Sijasikia ndo nasikia kwako
Ila wakikataaa si ndio vizuri wapiga kura wamepata taarifa kuwa misaada imekataliwa? Na watajua mbaya kwao?
Ila si kimefanyika au hakijafanyika???
 
Nimekupa mfano wa Mbunge wa viti maalum CDM aliyepeleka sare za shule kwenye shule moja Singida but akakatazwa kuzigawa kwa wanafunzi, sijui bado unataka nikwambie kitu gani tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijasikia ila nitaifatilia hiyo habari kiundani nijue siasa yake ilikaa vipi
Ila wapiga kura si wanajua mbunge wao anafanya jitihada gani kuwaletea maendeleo
Ila nafikiri tu kuna cha ziada mpaka akakataliwa na nitakujibu baada ya kukicheki
 
Sijasikia ndo nasikia kwako
Ila wakikataaa si ndio vizuri wapiga kura wamepata taarifa kuwa misaada imekataliwa? Na watajua mbaya kwao?
Ila si kimefanyika au hakijafanyika???

..sasa kitendo hicho siyo sawa kuwawekea VIKWAZO hao wananchi?

..Je, kitendo hicho siyo siasa chafu ambazo wewe unasema ni mbaya kwa nchi yetu?

..Je, waliofanya hivyo hawaichafui nchi?
 
Ni kweli unachosema ila nabaki na msimamo ule ule kila mtu hata mtoto mdogo anajua ile kesi ilikuwa ya kutengenezwa na ndivyo nilivyosikia kwenye media. Nakumbuka Lowasa akiwa anagombea alihaidi kuwa atamtoa mzee seya na wanae

Ila kilichooneka ni kuwa mzee seya alishindwa ku prove kuwa hakufanya hivyo na ndicho kilichomfunga ila sio kuwa lifungwa kwa sababu amefanya hivyo. You get it?
Kwahiyo unakubaliana na wapinzani, kuwa viongozi walioko madarakani wanawabambikizia wasiowapenda kesi ?! Kama umekubali ya babu Seya, unakataaJe kuwa wapinzani wa serikali hawabambikiwi ma vyesi vya uchochezi ?!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mtu ana uhuru wa kuwa na mtazamo na labda kwako umeona nimekuwa upande wa raisi Magufuli, ila ukisoma kichwa cha habari ni utaelewa ni juu ya mtazamo wangu binafsi juu ya siasa ya Tanzania na raisi Magufuli na nimeandika kama kichwa kilivyojieleza. .

Ila umehisi nimeandika kumponda Mheshimiwa Tundu Lisu, na hicho ndio ulichokiona ila la msingi wewe huyaoini, je ni kitu gani ambacho nimezungumza juu ya mheshimiwa Tundu Lisu?? Ila hujajibu hata hoja yangu moja ila kwa kuipinga kwa Hoja au kubisha tu. Kwa mtazamo wangu tu umeandika hoja nyingine ambayo pengine ungeweza kuwa uzi mwingine unaohusu safari ya Tanzania kwenye mikono ya raisi Magufuli na pengine ningekujibu ila unanitoa ndani ya mada husika. .

Samahani ila nachokiona ni public sympathy, kama kupigwa risasi kwa mheshimiwa Tundu Lisu kinakunyima chuki yake binafsi dhidi ya raisi Magufuli inajikita mpaka kwenye kutaka kuboamoa Tanzania. Leo hii mheshimiwa Tundu Lisu anaomba publicly Tanzania inyimwe misaada, Je hiyo misaada anakula raisi Magufuli na familia yake? Hiyo misaada ni kwa ajili ya kila mTanzania ikiwemo mimi na wewe. Leo naona mheshimiwa Tundi Lisu anakubali kushikana kabisa mikono na mabeberu ili kusupport ushoga, kitu amabcho ni kinyume na maadili yetu, ambapo unampelekea chuki raisi Magufuli, wakati hoja ni kuwa chuki yake haileti maendeleo kwa Tanzania. .

Sipingi kama wana chuki ziwepo ila zisiwe kuiathiri Tanzania na waTanzania. Ila kipindi kile nilikuwa napata majibu mengi sana wakati Lowasa kasimama kugombea uraisi "kwani ikulu kuna kazi ya kubeba mawe". Ila nadaharia yako uliojiwekea ni kuwa nchi hii inaendeshwa na mtu mmoja tu anayeitwa 'Magufuli'. Ila nchi hii inaongozwa na viongozi wengi kuanzia ngazi ya kijiji mpaka ngazi ya nchi ambao sio CCM wala si kwa mawazo ya Magufuli. .

Raisi Magufuli kwenye uongozi wake kuna madhaifu mengi nimeandika moja ni kuharibu taaluma, sijaundika kumfagilia raisi Magufuli ila kwa kuwa nimeandika neno Tundu Lisu, basi nachoandika hata kama cha maana unakiona si kitu. Nachotaka tujibiane hoja kwa hoja na si kufanya siasa, na kama nimeandika umeona mtazamo finyu nielimishe nini kifanyike. Nadhani hujasoma vizuri hakuna sehemu nimeandika kiongoze chama kimoja unaweka maneno kinywani mwangu, nimesema natamani sana upinzani utawale siku moja ina maana hukuona???. .

Waliotoka utumwani ni wana wa Israel na sio Tanzania. Usitufananishe sisi na wana wa Israel wala utumwa wa Misri, sawa sawa na kuchanganya maziwa na tui la nazi. Tuache ya kwenye Biblia yabaki kwenye Biblia naomba unijibu au upinge hoja zangu kwa mifano au hoja. .
Wewe kwa kifupi umekuja na njaa njaa zako kumtetea jiwe, japo unazinguka zunguka tu lakini ukweli ndiyo huo, chanzo cha chuki yote hii na matatizo tuliyonayo umeshaelezwa nani ni chanzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..sasa kitendo hicho siyo sawa kuwawekea VIKWAZO hao wananchi?

..Je, kitendo hicho siyo siasa chafu ambazo wewe unasema ni mbaya kwa nchi yetu?

..Je, waliofanya hivyo hawaichafui nchi?
Nimeshaona tatizo kumbe alienda kazungumza na walimu kisha kapeleka misaada na waandishi wa habari huku akiwa hajamuona mkuu wa shule (hakuwa na taarifa).

Habari yake hii hapa na sababu za kukataliwa kutoka jeshi la polisi.

Swali langu je baada ya kukataliwa na kupewa njia za kupita ili kuwasilisha msaada wake, kwa kuwa kila kitu kinafuta utaratibu wa sheria. Je alifuata hizo taratibu ambazo zipo kisheria ili kufikisha msaada wake?
 
Wewe kwa kifupi umekuja na njaa njaa zako kumtetea jiwe, japo unazinguka zunguka tu lakini ukweli ndiyo huo, chanzo cha chuki yote hii na matatizo tuliyonayo umeshaelezwa nani ni chanzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alafu hunijui tu kama ungenijua ungejua kuwa mie sina njaa mie niweka hoja mezaki huna ulazima wa kuargue au kukubaliana nayo, yote sawa ILA fedheha za nini?

Siasa sio ugomvi, tunajadiliana tu kwani mie na wewe tuna ugomvi? Chuki ya Lisu na Magu sie tutoke povu usiku huu..

Alafu mie simtetei myu nimeweka mtazamo wangu tu
 
Kwahiyo unakubaliana na wapinzani, kuwa viongozi walioko madarakani wanawabambikizia wasiowapenda kesi ?! Kama umekubali ya babu Seya, unakataaJe kuwa wapinzani wa serikali hawabambikiwi ma vyesi vya uchochezi ?!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mahaka ya Afrika and ICC wanaoona wanabambikiwa kesi kuna ulazima wa kwenda kupeleka ushahidi huko kama wanavyofanya wenzetu
 
Nachokisema kinajidhihirisha hapa
Wengi waliokuwa upinzani ni kama hawana hija
Kilichobaki ni fedheha, kukufanya ujisikie kilaza, na kukutukana

Hawakatai na wala hawapingi so simple minded hawa watu sijui kwa nini
Na wanadhani watatuletea maendeleo kwa matusi na kejeli
Ulipoanza kuleta ishu za uzalendo uchwara na kutumia neno beberu nimekudharau sana. Ila naamini iko siku Mungu atafanya yake na mkoloni mweusi tutamtoa tu. Sorry kama lugha yangu imekukwaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom