Mtazamo wangu kuhusu mwenendo wa tanzania

chazymseri

Senior Member
Oct 28, 2010
139
28
Wananchi walio wengi wamekuwa wakiangalia mwenendo wa nchi yetu kwa upande mmoja tu
pasipo kuangalia huyu mungu aliyeiumba Tanzania na watu wake na kuiwekea vivutio vingi madini ,bahari
milima mbuga na mambo mengi yenye kutujengea uchumi anamakusudio gani na Tanzania.

Ukweli ukiangalia kwa mara moja tu utaona miundo mbinu ya nchi ukilighanisha na thamani tulizo nazo
kama nchi haviendani na hali halisi.

Tukianzia na utawala wa kwanza kweli utawala ule ulikuwa na mazuri mengi sana na yanakumbukwa mpaka leo
bandari,reli,ndege na mambo mengine mengi tulimiliki wenyewe leo hii viko mikononi mwa watu wachache lakini je
ni kwanini?

Katika utawala huo wanachi walikuwa hawana fedha zakuanzisha shule binafsi,hospital binafsi,viwanda binafsi,mashirika ya ndege binafsi
nyumba asilimia kubwa nchini zilikuwa niza udongo ukihesabu wananchi walioweza kumiliki mabasi nchi nzima huenda walikuwa
hawazidi mia ukiwa na duka la kuuza mafuta ya taa na mikate ndio ulikuwa unaonekana tajiri, wananchi walikuwa maskini sana na tulitegemea
wageni waje wafungue biashara tuajiriwe huko hakika tulikuwa ni wenye nchi lakini hatukuwa na kauli kushindana na wageni katika nchi yetu.

Tuje katika utawala wa pili hapa tulipewa kiongozi ambaye walio wengi waliuona kama ni uongozi dhaifu pamoja na kuwa alipitia kwenye
chekecheke la mwalimu na akatuambia huyu ndiye bora nasi tukamkubali kwa dhati lakini kumbuka hakuna ajuae makusudio ya
mwenyezi mungu kwa mara moja pia kumbuka mambo mengi yatokeayo katika dunia hii ni kwa makusudio ya mwenyezi mungu
uongozi huo tuliouona dhaifu ulitoa fursa za biashara mbali mbali na kulegeza mashari ya biashara yaliyokuwepo awali fedha zili hama nyingi kwenye mikono
ya serikali na kuhamia kwa wananchi,taratibu wananchi walianza kuanzisha biashara za mashule zahanati usafiri wa mabasi mahotel radio tv nk uwezo wa wananchi
kupata elimu ya juu uliongezeka wanachi waliweza kushika maeneo makubwa kama mashamba na vitu vingine vikubwa kumiliki migodi na mambo mengine
ambayo hapo awali tulikuwa hatuna uwezo nayo

Utawala wa tatu ulirekebisha yale kibinadamu tuliyoyaita makosa ya utawala wa pili serekali ilirudisha nguvu zake fedha zikarudi serikalin
i lakini ikiwa imewaacha wananchi na misingi mikubwa sana ya kibiashara japo mingine ikiwa inakufa lakini inakufa huenda kwasababu fulani
ambazo kibinadamu sisi ni vigumu kujua kwa haraka lakini kiukweli wananchi waliweza kuingia kwenye mchakato wakuchukua tenda zozote
ambazo zingeshindaniwa na makampuni ya njee kama wakati ilivyokuwa ikitaka kuuzwa kilimanjaro hoteli mengi alijaribu kutaka kuinunua
lakini ikashindikana tulianza kuwa na sauti na nchi yetu kwakuwa tuna pesa lakini hapo hapo ukitaza hizo fedha zimetokana na nini utakuta zimetokana
na ubadhilifu wa mali za umma je hao wanaoziiba wanakula na nani utakuta wanakula na sisi sisi kwa njia moja ama nyingine kwani akijenga kiwanda hapa
nchini akaajii watanzania 500 si amekula na sisi nasio wawekezaji ambao faidayote wanapeleka nje ya nchi yetu, nimechambua kidogokiogo ili isikuchoshe msomaji

tuje utawala wa nne utawala wa nne japo walio wengi tuliona utawala wa tatu ulikuwa na makosa tuliuamini sana utawala wa nne wakati tunauchagua
nakuona huu ndio utakuwa bora kuliko yote na uliokuwa na damu ya kizazi cha karibuni lakini sivyo ilivyokuwa kibinadamu tumekuwa tukiona mambo
yakienda ndivyo sivyo na kuulaumu uongozi uliopo madarakani kwakuwa dhaifu kiutendaji lakini huenda tunawaza kibinadamu tu.
Binadamu anapaswa kujua sisi nikama makasha ya computer tu vipo vitu vilivyoko ndani mwetu ambavyo vinatu comand kufanya mambo ya maendeleo ya
dunia hii na kwa makusudio fulani wewe kama nanafsi unanafasi fulani ndogo tu pasipo wewe kujijua hivyo tunafikiri tunaiendesha dunia lakini sio kwel dunia
inaendeshwa kwa utaratibu fulani ambao nivigumu sisi kuuelewa na ndio maana unakuta tunatofautiana kutokana na comand ambazo tunapewa tuzitekeleze
pasipo sisi kujua leo tunamshangaa mtawala wetu haendi sawa huenda tutakuwa hatusomi alama za nyakati na kumshirikisha mungu hivi nyerere angeendea
kuwepo na kung'ang'aniza siasa za ujamaa na kujitegemea leo ungekuta bado dar es salaam imezungukwa na nyumba za udongo ukiangalia sana maendeleo
yaliyopo yametokana na yale tunayoyaita makosa yaliyotokea katika tawala zilizopita hivi kusingekuwa na makosa yaliyotokea kama hayo kungekuwa na hospital
binafsi kungekuwa na shule binafsi tungekuwa na mashirika ya ndege binafsi boat za kwenda zanzibar za kisasa tungekuwa nazo? kweli fedha zinapotea serikalini
zinaingia mikononi mwa watu lakini hao watu ndio watajenga kiwanda watajenga mahoteli mungu alishatuona tulivyokuwa na shida katika utawala wa kwanza
asingeweza kushusha fedha kuwapa wananchi ambao walikuwa hawanauwezo wowote wa elimu wakulipa hata wakikopa amefanya utaratibu wakutupatia fedha
katika njia ambayo kibinadamu sisi tunaona sio sahihi hayo hayo makosa yaliyofanywa serikali pesa nyingi zikaingia mikononi mwa watu ndio leo hii tunaona
kabisa tunaweza kununua ardhi kubwa watanzania kwa sasa wameshika maeneo makubwa kariibu nchi nzima sasa iko mikononi mwa watanzania wenyewe
lakini bila makosa yaliyotokea wageni wangekuja wangenunua ardhi na tusingekuwa na sauti katika nchi yetu tuangalie ilivyokuwa zimbabwe (rhodesia)

Namalizia kwakusema kimtazamo wangu mungu anatupenda sana watanzania ametafuta namna ya kutuwezesha kuiweka mikononi nchi yetu wenyewe leo
mgeni akija anatukuta tumeishika nchi yetu wenyewe hata miradi mikubwa ikitokea wapo watanzania watakaoweza kuiomba kufanya na wakaweza.

Bado kunatatizo kama la umeme na maji matatizo kama ya umeme ndio tunateseka lakini wakati wawekezaji wakisema tanzania sio mahali pazuri pakuwekeza
kutokana na tatizo la umeme watanzania wenyewe wanawekeza na wanaendelea kujishika vizuri na nchi yao hata umeme utakapokuwa
umekuwa imara wakija wanakuta nafasi zimebaki finyu na watanzania wenyewe wana nguvu katika nchi yao

kama tanzania ingekuwa kama new york katika miaka 5 iliyopita basi ungekuta hata ardhi yakununua tanzania hakuna wageni wangesha ilamba yote.

Hao mafisadi kwani wanakula ngombe nzima kwa wakati mmoja si wanakula kinyango kimoja au viwili katika milo yao hayo mabiloni waliyoiba na kuwekeza
mahali ndiko mjomba wangu anafanya kazi mtoto wa shangazi anafanya kazi dada anafanya kazi na watoto zao wanakula na kwenda shule hata kama
hizo pesa ziko bank basi ndiko nami nitaenda kukopa maana pia bank haitakubali kukaa na fedha bure bure bila kuzifanyia kazi watatukopesha watanzania

jamani nimewasilisha kwa mtazamo wa kibinadamu utaona ni mtazamo potofu lakini kimungu ndivyo ilivyo na tunapaswa kumshukuru mungu kwa kila jambo mbele
ya safari ndio unakogundua kumbe mungu alikuwa na maana fulani
 
Back
Top Bottom