Mtazamo wangu kuhusu Mababeru

DAN LOKOMOTIVE

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,503
1,901
Habari wana jamvi poleni na kazi,

Katika harakati za hapa na pale kuhusu mustakabali wa taifa na mambo yote yanayoendelea ningependa kutoa mtazamo wangu kuhusu hawa watu wanaoitwa '' mababeru''. Ni jambo amabalo lianishangaza sana sana watu huku mitaani pia na kwenye majukwaa ya kisiasa kumekua na hii dhana ya kuwa mabeberu wakimaanisha ni wazungu au wachina au watu ambao sio waafrica kwamba wana mpango wa kutuua au kutudhuru sisi watanzania.

Hili kwa upande naona ni jambo la kusikitisha sana kwamba sisi kama watanzania tunashindwa kujifunza mahala tunapokosea na kurekebisha makosa ambayo kwa miaka na miaka watu wachache wankula pesa za wananchi halafu watu wakijaribu kuwarekebisha wantumia kusema '' wametumwa na mabeberu'' ili kuja kuvuruga maisha yetu. Ni jambo la kushagaza sana kwamba wanaovuruga mambo ni sisi wenyewe kwa kukosa uadilifu na kukimbilia kwenye kichaka cha mabeberu

Ukweli uliopo ni kwamba kama mabeberu wangelikuwa wana taka tusiishi au kutuua basi kizazi amabacho sasa kinamiaka kuanzia 30 kisingekuwepo chukulia mfano wa kwanza

1. watoto wote wanapolzaliwa huwa kuna mfululizo wa chanjo za magonjwa kama polio, matone ya vitamini amabayo hupewa na hivi vyote vimetengenezwa na mabeberu

2. Asilimia kubwa ya dawa za mahospitalini pamoja na vifaa amabavyo vinatumiwa kwa watanzania inatoka huko huko kwa watu amabao wanania ya kutuua mfano madawa ya usingizi, tetenus , dawa za ukimwi, machine za MRI, machine za kuchuja mkojo , Dawa za chemotherapy n,k

Ukiangalia technolojia ya hivi leo tunategema hao hao mabeberu, kuanzia vifaa, mpaka wireless systems nakuendelea sasa mimi swali kichwani huwa najiuliza hivi hawa jamaa ''mabeberu'' kama wanampango wa kutuua je wasinge tuua kupitia itu vyote hivyo hapo juu maana kwa asilimia kubwa maisha yetu sisi yanategemea mabeberu.

Cha kushangaza zaidi kila siku serikali inaimba kuita wawekezaji ambao ni hao hao ''mabeberu'' ? sasa hii mtu anayetaka kukumaliza utamwailka kwako aje kufanya shughuli zake je? Pia hao hao mabeberu kila siku wantuletea misaada na kutukopesha pesa sasa swali hivi inakuwaje tena mtu anayetaka kukuua akupe pesa na upokee au uende ku mkopa pesa..

Jambo la kushangaza lingine hawa hawa wanaotuambia mabeberu wanataka kutuua ukiagalia CV zao wengi wameenda kusoma huko huko kwa mabeberu na wanatumia hicho hicho walichokisoma kutuongoza sisi sasa swali hivi mtu amabaye anataka kukuua utawezaje kwenda kuomba elimu kwake , Pia hawa hawa maberuberu ni kwa jina lingine wanaitwa ''NCH WAHISANI'' hapa ndio nachoka kabisa sisi tumeshafahmu kwamba hawa waataka kutuua sasa inakuwaje watupe hisani na tuzikubali?

Watanzania natoa wito tubadilike tuache kuwa na mawazo mgando
 
Kayafa Mwendakuzimu kwa kushirikiana na Prof Majalala waliharibu akili za wajinga wengi kwa propaganda zake mfu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom