Mtazamo wangu kuhusu kauli ya zito kabwe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtazamo wangu kuhusu kauli ya zito kabwe.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NGOWILE, Sep 30, 2012.

 1. N

  NGOWILE JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 454
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MTAZAMO WANGU KUHUSU KAULI YA ZITO KABWE KUHUSU URAISI 2015.
  Zito yupo sahihi kuweka wazi ndoto yake katika maswala ya kisiasa. Kiuhalisia kila mtu siku zote huwa anatamani kuwa katika nafasi ya juu kabisa kulingana na anachokifanya kwa mfano muuguzi hospitalini anatamani siku moja awe daktari mkuu, kondakta wa basi nae anatamani siku moja nae awe dereva, kibarua wa ujenzi nae anatamani siku moja kuwa fundi mkuu nk.Vivyo hivyo nafasi ya juu katika siasa ni uraisi kwa hiyo ni haki kabisa kwa mwanasiasa kuwaza kuwa raisi wa nchi kwani ndiyo nafasi ya juu kabisa kwenye siasa ambayo kila mwanasiasa anaitamani.

  OMBI LANGU KWA ZITO.
  Ni kweli umeonyesha dhamira yako kwa watanzania. Tumekusikia na tumekuelewa. Katika swala hili vikao vya chama vitaamua kidemokrasia kuwa ni nani atakaegombea uraisi mwa...ka 2015.Kama itakuwa ni wewe tutakuunga mkono kabisa na kama atakuwa mtu mwingine aliyepatikana kidemokrasia basi nawe umuunge mkono katika kufanikisha mabadiliko ya kweli ndani ya taifa letu.

  CHA KUFANYA SASA.

  Kikubwa cha kufanya kwa wakati huu sio kupoteza au kutumia muda mwingi kuitangaza ndamira yako.Kikubwa kilicho mbele yetu ni kujiunga na jeshi la ukombozi M4C kwenda kila kona ya Tanzania kukijenga na kukiimarisha chama katika ngazi za chini pamoja na kuwaelimisha watanzania ili waelewe nia na madhumuni ya CHADEMA kwa Taifa letu. Tumia muda wako mwingi kushirikiana na viongozi wenzako kukiimarisha na kukisimamia chama Muda ukifika utatekeleza dhamira yako hiyo njema.
   
 2. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 190
  Trophy Points: 60
  Labda ukisema wewe atakusikia vinginevyo si rahisi kufanyia kazi kwa kuwa ushauri kama wako manacdm wengi wamemshauri ndo kwanza anatafuta maneno mengine ya kuendeleza kauli zake mwanzo ilikuwa kanda ya magharibi,sijui kigoma mara kijana mara mtu aliyezaliwa baada ya uhuru ndo mwenye uwezo wa kujenga uchumi lakini binafsi naamini kipo kitu nyuma yake na sio dhamira ya kweli bali tamaa tu ambayo imepiliza na kwa kweli time will tell the truth.Vinginevyo my regards to you!
   
Loading...