Mtazamo wangu juu ya ujio wa TIN kwa Waajiriwa

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
9,699
2,000
TIN yaani (Taxpayer Identification Number) Ikimaanisha namba ya utambulisho wa mlipa kodi.

Namba hii imeunganishwa na taarifa za mtumiaji kama Namba ya NIDA, Passport ya kusafiria, Lesini ya kuendeshea gari, Kitambulisho cha Mpiga kura na sasa itaunganishwa na check namba ya muhusika.

Athari ninayoiona mimi ni kwamba kuna watu walishawahi kumiliki biashara hapo awali ila kutokana na changamoto mbalimbali wakaamua kuzifunga kinyemela bila kutoa taarifa TRA (hapa wapo watu wengi saaana).

Taarifa zao zitakapounganishwa na Check Na. ndio itajulikana huyo mtumishi kumbe anadaiwa mamilioni ya fedha hapo ndio kilio na kusaga meno kitakapowaka, tusubiri Januari.

Wapo watu waliowahi kumiliki magari enzi tunalipa Road license (RL) na wakauza magari yao na mnunuzi hakulipa RL hivyo TIN yako ndiyo itakuwa inadaiwa. Utajuta kutofanya card transfer.

Hapa pia watapatikana watumishi ambao wanamiliki mali/biashara kubwa nao wataanza kuunganishiwa na PCCB wakitaka kujua alizipataje, kiujumla ni full mtafutano.

Anyway mambo ni mengi mda mchache acha tukamuane maana mabeberu wamegoma kutusaidia sasa tukaze mikanda.

Mitano tena,

images.jpg


Alasiri njema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom