Mtazamo wangu juu ya hii misaada tunayoendelea "kuzawadiwa"

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Wakati nikiwa mdogo enzi hizo niliamini kabisa katika kupewa kitu bila kudaiwa na mtoaji hasa pale mtoaji anapokuwa na uwezo ki uchumi

Hii imani niliijenga kwa sababu ndugu zetu waliobahatika kuwa na kazi huku mijini, kila walipokuja kutembea kijijini ilikuwa lazima waje na vizawadi vya nguo zilizotumika na watoto wao au wao wenyewe, mikate ambayo huko kijijini ilikuwa ni kama lulu, na zawadi nyingine ambazo kule kijijini hazikuwepo! Ki ukweli familia nyingine zilikuwa zinatuonea wivuuuuu kwa "tuzawadi hutwo twa" karibu kila mwisho wa mwaka!! Waimba kwaya ya shule waliokuwa hawana viatu na yuniform safi walikuja kuazima kwetu siku za mashindano!

Kiukweli nasi tulionekana tumo tumo kati ya wale waliokuwa angalau familia zao zinaonekana pale kijijini! Hapa naongela familia za walimu, manesi na watumishi wengine.

Baada ya kuwa na ufahamu wa kuhojiana na akili yangu, niligundua kuwa kulikuwa na mchezo wa nipe nikupe ambao ulijificha kwenye kivuli cha ukarimu Kwa pande zote mbili.,za wale ndugu zetu wa mjini na familia zetu za kijijini!

Wao walikuja na zawadi za nguo ambazo wao kwa asilimia kubwa hawakuzihitaji tena sana! Huku kwetu kijijini, walichinjiwa mbuzi, kuku na wazee walijinyima kadiri wawezavyo kuwaandalia vyakula na mapochopocho ambayo kwa pale kijijini vilikuwa na thamani kubwa ambapo sisi tuliishia kuvitumbulia macho tu siku zote hadi siku za sikukuu au ugeni kama huo!!

Si hayo tu, safari ya kurudi kwao ilipowadia, walifungashiwa vitu kibao hasa mazao yaliyolimwa pale kijijini! Hivyo kwao vilikuwa vya thamani kwani hakuna asiyejua bei ya vyakula ilivyo juu huku mijini!!?

Najaribu kuoanisha jambo hilo na namna hawa wageni wanaotutembela hapa Tanzania na mara tu wanapokaribishwa Ikulu, Mkuu wetu huja haraka haraka kwenye vioo vyetu vya sebuleni kutueleza msaada waliotuachai!

Juzi Bilgate katuachia mabilioni ya pesa! Jana Rais wa Misri kaahidi kumwaga mabilioni kuboresha hospitali yetu ya Taifa na kujenga kiwanda cha nyama!

Hao ni wachache tu ukianza kuhesabu tangu tulipoambiwa ni bora kula mihogo kuliko kupewa mkate wenye masimango!

Ni kweli kabisa wao wanatukarimu tu na hakuna chochote tunachowakarimu sisi!? Kwanini inaposemwa misaada tuliyopewa visisemwe na sisi tulivyowapa kama sehemu ya "kukarimiana "!?

Ni kweli sisi siku hizi hatuna ukarimu kiasi hicho!? Ni kweli kabisa wao (foreigners) wamekuwa wakarimu kiasi hicho!?

Mtazamo wangu ni kwamba, mamlaka zinaposema tulichopewa au kuahidiwa sio dhambi zikasema na sisi tulichowapa au tulichowaahidi! Isionekana kwamba vyao kwa sababu vinatoka ulaya na Marekani au Uarabuni vinathamani kuliko vyetu wanavyopewa!

Ni hayo tu, na wewe unakaribishwa kusema yako! Karibuni sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulisha ambiwa mkuu. There is no free lunch, hiyo kauli ina maana kubwa sana
 
Back
Top Bottom