MTAZAMO WANGU JUU YA FAO LA KUJITOA (Withdraw Benefits)

CHIJANYE

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
347
250
Jana nikifuatilia mjadala wa bunge ikiwa ni zamu ya Wizara ya Kazi na Ajira niliona mvutano juu ya suala la fao la kujitoa ambalo kwa upande wa serikali wanatamani wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kutojitoa na watapeleka mswaada wa sheria kusimamia hili.

Ni jambo lisilopingika kwamba hapa nchini kwetu hifadhi ya Jamii bado haijafanya ile kazi hasa ya kuhifadhi jamii kwa maana ya wanachama na hivyo kubariki watu tupende na kutamani kujitoa. Kama wanachama ambao tunachangia mifuko mbalimbali ya hifadhi ya Jamii bado tunayo matatizo mengi ya kijamii yakiwemo malazi, makazi na huduma nyinginezo za kijamii. Na hakujawa na mchango dhabiti wa mifuko huu kusaidia wanachama wake.

Hifadhi ya Jamii ingekuwa inawawezesha wanachama kupata huduma muhimu za kijamii kulivyo inavyofanya kwa watu ambao wala pengine si wanachama. Hapa kwetu baadhi ya mifuko inadai inakopesha wanachama lakinini kupitia Saccos. Mfumo huu hauna msaada wa kutosha kutokana na kwamba Saccos zinaambiwa kuongeza riba ya asilimia moja hadi tatu katika riba ile inayotakiwa na mifuko kwamaana kama mfuko unatoza 10% basi ukijumuisha na ile ya saccos labda iwe asilimia 13%. Aidha asilimia inayoongezwa na Saccos haiwezi kamwe kuziwezesha saccos kumudu gharama na athari za mikopo yenyewe. Lakini kibaya zaidi saccoss ikishakopa labda millionu 50 mpaka waliopewa wamalize kurejesha ndo inaweza kupewa fedha tena kwa ajili ya wakopaji wengine. Kwa lugha nyingine kama watu kumi wakachukua mkopo huo wote kwa muda labda wa miaka mitatu, itabidi wanachama wengine wa mfuko husika kupitia saccos hiyo kusubiri hadi miaka mitatu ndo wanaweza kujaliwa kukopa.

Lakini wafanyabiashara wakubwa wanapata mikopo ya mabilioni na hata makampuni ambayo pengine hayachangii chochote kwenye mfuko bila masharti kama anayopewa mwanachama ampaye kwa kiasi fulani ni mmiliki wa mali za mfuko husika.

Baati nzuri ninaouzoefu mwenyewe nilienda kuulizia Nyumba zilizokuwa zimejengwa na NSSF kwa ajili ya kuwauzia wanachama wake. Nyumba moja nilikuta iko kuanzia milioni 80 na kkuendelea ambayo ilinitaka ili niweze kuipata kwa mwezi niwe na uwezo wa kulipa kuanzia laki 600,000/- kwa maana nyingine niliambiwa angalau mshahara wangu ukiwa unaanzia 2,400,000/- ndo ninaweza kumudu kuipata. Sasa nikajiuliza kweli wanachama wengi wa mifuko hii wanaweza kuwa na mishahara ya hivyo kwa Tanzania hii. Pengine walikuwepo wengi isipokuwa mimi tu. Lakini ukiangalia hata utoaji wa huduma zake za afya bado si kwa kiwango kile cha practical social security.

Sasa basi baada ya muda mimi niliacha kazi nikaamua kushugulikia cha kwangu ambacho nilikuwa nimeweka kwenye mfuko kwa miaka 3 ambacho hakikuwa kimezidi 15 milioni baada ya kuacha kazi. Kiasi hiki nilichokipata kiliniwezesha kuweza kuweka kibanda kizuru somewhere ambacho kimekamilika kwa kuongezea kiasi kidogo tu vizuri kwa maana ya finishing. Sasa kumbe mifuko ya hifadhi ya Jamii ingekuwa inamjali mwanachama ikamwezesha hata angalau mkopo wa 25 million ambayo wengi wanaweza kuimudu ingekuwa na maana na ingeweza kuwafanya watu wasichukue fedha zao kwani wanakuwa bado wana liability ya kulipa. Lakini ingekuwa inawapa na matibabu bora yenye hadhi wanachama na wategemezi bado yote haya yangejenga mazingira ya watu kutochukua fedha kwenye mifuko.

Hapa ndipo naiona hoja ya Mh. Machali Moses ni ya Mashiko makubwa kwani alieleza vizuri japo alipuuzwa kwa sababu ya kasumba ya bora liende. Sheria inasema niweze kuwa na sifa ya mafao lazima uwe umechangia miaka 15 na kuendelea. Sasa Mimi nimechangia zangu labda miaka nane na tuchukulie nina balance ya michango labda million zangu 80. halafu sitaki kuendelea kuajiriwa hivi hii pesa nikiichukua sipati mradi mzuri wa kukuza kipato. Lakini je siwezi kuwa na mradi mkubwa na nikaajiri wengine na pia wakachangia kwenye hifadhi ya jamii na hivyo kuongeza wigo wa wanachama lakini na rasirimali michango?

Aidha hoja ya Waziri ilikuwa ni kwamba fao la kujitoa halifai kwa kuwa sisi tumeridhia mikataba ya ILO kwa hiyo hatutakiwi kuweka hilo fao kwani tutakuwa kinyume. Sasa je Waziri mambo hakueleza kwamba kwa kuwa hatutoi fao la unemployment benefit basi tumekiuka mikataba hiyo ya kimataifa na hivyo tungetakiwa kuwajibika. Ninachoona ni kitu kilekile kwamba tunaridhia kila kitu ambacho hatuendani nacho kwa Mazingira yetu. Lakini sisemei tusiridhie ila tunaporidhia mambo ni vema tukayalocolize ili yaendane na Mazingira yetu. Ninachokiona kwa sababu hatuna uwezo wa kufanya unemployment pay ambayo ingemsaidia yule anayekuwa hana ajira pindi anapokuwa amekosa ajira jambo ambalo lingelimfanya mtu huyu kumudu maisha ili mpaka apate kazi nyingine au afikie ule umri wa kuchukua fedha yake.

Lakini unaweza ukajiuliza masuala kadhaa mfano life expectancy ya watanzania ni kweli ni rahisi mtu kufikia umri wa kuichukua fedha yake akiwa bado ana nguvu ya kuzifurahia na kuzitumia kiuendelevu? Lakini imetokea labda nimekosa kazi na nimepigika kiasi cha kwamba ninakula mlo mmoja na familia ikitegemea huduma itakuwa ni busara kuziacha labda tuchukulie milioni 30 kwenye mfuko ati mpaka nifikie umri wa kuzichuku? je katika hali kama hiyo nitafika au nitakufa nitaziacha na hivyo zitakuwa hazikunisaidia na kupoteza dhana ya hifadhi ya Jamii? Kwa hiyo nikiangalia yote haya bado naona umuhimu wa mtu kuruhusiwa kuchukua chake anapokosa Ajira au akiamua asiendelee kuajiriwa ili azitumie kujiendeleza na kujiajili mwenyewe na kuajiri wenzie. Nitakubaliana kuondolewa kwa fao kama kweli hifadhi ya jamii itakuwa ni ya wanachama kwa manufaa yao na kuwasaidia practically kama ambavyo nimeeleza kwa kiasi.

Lakini kama sheria hiyo inayokuja itapita kwa mfumo mbovu wa hifadhi ya jamii uliopo hivi sasa basi nami zamu hii nitatafuta na wenzangu tugeuke mtikila na kuipinga sheria mahakamani na pia kutengeneza umoja wa wanachama wa mifuko yote kusema NO unless social security is real social security na si kwa faida ya watu wasio hata wanachama au wachangiaji.
 
Hifadhi ya Jamii ingekuwa inawawezesha wanachama kupata huduma muhimu za kijamii kulivyo inavyofanya kwa watu ambao wala pengine si wanachama. Hapa kwetu baadhi ya mifuko inadai inakopesha wanachama lakinini kupitia Saccos. Mfumo huu hauna msaada wa kutosha kutokana na kwamba Saccos zinaambiwa kuongeza riba ya asilimia moja hadi tatu katika riba ile inayotaki
 
House of Commons

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,860
2,000
Good thread, naomba ufute zile post zingine ulizopost kwa makosa ili tread yako ipendeze, otherwise you have a nice idea
 
CHIJANYE

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
347
250
Machali kama upo kwenye jukwaa jua kwamba waliowengi huku nje tuliunga mkono hoja yako kwani uchache weni ni sawa na Nyuki Bungeni na Wingi wao ni sawa na Nzi
 
CHIJANYE

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
347
250
Tushirikiane tu kwenda mahakamani watakapo tuletea sheria kandamizi ambayo inawapa rungu la kuzitafuna fedha za watu
 
CHIJANYE

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
347
250
Wanaojiita wengi bungeni tatizo lao ni kulala wakisikia tu mwenyekiti anasema wasioafiki waseme Ndiyo, ndo utasikia wameshtuka ndiyoooooooooooooooo. Imeshakuwa classical conditioning kwao
 
Muk

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
551
195
Mkuu naitaji nikutafute. So nikupateje maana nimependa jinsi ulivyosema hayo mambo
 
kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,929
2,000
Kwa huu ujinga, nipo tayari kuuza roho yangu. Serikali kwa nia yake ya uroho wa kutuzulumu jasho letu la mateso yetu tupatayo wafanyakazi tufanyao kazi katika mazingira magumu. huu ujinga wa uwache na wala wasiufikirie kabisa. Maisha yenyewe yako wapi? Maisha magumu yaliyo fanya maisha ya kuishi kuwa mafupi. Ufisadi upo kila kona, leo tuwaachie pesa zetu wagawane kiulaini. Kodi yenyewe imekuwa mzigo kwetu, maendeleo hatuyaoni. Barabara kila mwaka zinakarabatiwa kutokana na ujenzi duni. Aki anani risasi halali yangu, ujambazh wa serikali hauvumiliki.
 
Possibles

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
1,523
2,000
Inauma sana.
Tunafyonzwa nguvu zetu kwa malipo kiduchu na bado wanadhamiria kutufyonza hata akiba zetu!!!!!
Inauma sana.
Kwa malipo haya hafifu wafanyakazi wengi wanashindwa hata kupata mlo kamili na bora, hivyo kupunguza miaka yao ya kuishi sasa iweje serikali take mtu huyu afikie kustaafu ndiyo adai chake!!!!!

Tatizo umoja hatuna. So bure tu kusema
 
CHIJANYE

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
347
250
Pesa zetu zinawafaidisha tu wafanyabiashara wakubwa kina Manji na makampuni yao. Hatukatai wasikopeshwe kwa maana ya kuongezea thamani tunachotaka na wanachama wawe na haki ya kukopesha kujiendeleza bila milolongo na mizunguko
 
CHIJANYE

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
347
250
Mara saccoss saccos zenyewe wanazipa mashart huku nazo zina masharti yako so tunakuwa na mashart extra mashart ukijumulisha ya saccoss na ya mifuko yenyewe
 
CHIJANYE

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
347
250
Gharama zenyewe za ujenz wa nyumba za mifuko ziko juu wakati mimi niliwithdraw nikapata 15 million nikajenga nyumba nzuri kwa kuongeza vipesa kiduchu
 
CHIJANYE

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
347
250
Aidha mimi niko saccoss ambayo hunipa mkopo kwa riba ya 5% kama mwanachama kwa nini sasa nichukue huo wa NSSF?
 
Wimana

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
2,450
2,000
Niliamua kuacha kazi ili niweze kukomba mafao yangu ya NSSF baada ya kufanya kazi miaka minane, maana sikuona faida yoyote ya pesa yangu kuwaneemesha wachache na kutuacha wachangiaji hohehahe ati hadi tustaafu.

Niligundua yafuatayo yaliyonifanye niache kazi ili nikombe akiba ya uzeeni nikiwa kijana mwenye nguvu kwa sababu zifuatazo:
1. Kuwa NSSF hawaweki interest ya kutosha kuwaongezea wachangiaji.
2. NSSF hawa-maintain hata thamani ya pesa kwa wakati husika; yaani kadiri michango yako inapokaa NSSF ndivyo michango yako inazidi kushuka thamani.

Kwa hiyo kama Serikali na Mifuko ya hifadhi za Jamii haitakuwa na sheria za kumlinda mchangiaji na kumnufaisha kwa mafao yenye faida; ni wazi wachangiaji wataendelea kubaki kuwa wanachama kwa lazima tu badala ya kuvutwa na mafao na faida za mafao.
 
Wimana

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
2,450
2,000
Pesa zetu zinawafaidisha tu wafanyabiashara wakubwa kina Manji na makampuni yao. Hatukatai wasikopeshwe kwa maana ya kuongezea thamani tunachotaka na wanachama wawe na haki ya kukopesha kujiendeleza bila milolongo na mizunguko

Angalau wangelipa interest za kuweza ku-cover inflation na kuongezea kafaida kidogo, vinginevyo ni bure tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom