Mtazamo wangu: Chongolo na Shaka wameonesha kushindwa kabla ya pambano, tunakusihi na kukuomba Mwenyekiti wa CCM uwaondoe

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Tukio la kuchapishwa kwa habari ya Uzushi kwenye ukurasa wa mbele kabla wa gazeti la Uhuru iliyosema"Sina wazo kuwania Urais 2025-Samia" limenifanya nitafakari sana Uwezo na Umakini wa Katibu mkuu wa CCM Ndg Chongolo na Katibu wa Itikadi na Uenezi ndg. Shaka. Naamini CCM ni chama kikubwa sana hivyo kinahitaji watu makini wa kukisimamia na kukiongoza.

Kwenye wasifu wake Ndugu Chogolo anaonekana ni mtu aliyekulia kwenye mfumo wa vyombo vya habari vya CCM kwa muda mrefu hivyo habari kama hiyo inaleta ukakasi mkubwa ambao unatupelekea tujadili uwezo alionao katika kukisimamia Chama.

Kitu kingine ninachojiuliza, kwa miaka mingi gazeti la Uhuru limekuwa ni chanzo cha kuaminika kwa taarifa muhimu za chama na za serikali na limekuwa kichochea kwa magazeti mengine ila cha kusikitisha leo ndio kinara wa kutunga uzushi. Sifa hizo zimeendelezwa vema na viongozi wetu waandamizi wa chama, kwa nini sasa ? Nani yupo ya hayo yote?

Je, umakini wa shaka upo wapi? kwa nini shaka asiwajibike kwa kushindwa kusimamia idara ya habari?
 
Kwani hilo gazeti haliko huru kufanya kazi zake japokuwa ni mali ua Chama?

Ni vipi Shaka na Chongolo wanaweza kudhibiti habari potofu zinazochapishwa na chombo chao cha habari hali ya kuwa si wahariri?

Aakh!! Wacha nijiunge banchback kuangalia comment za waja!
 
Back
Top Bottom