Mtazamo wangu: CCM itakuwa CHADEMA na CHADEMA itakuwa CCM ni suala la muda tu.

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,668
2,000
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda katika taifa letu tutegemee CCM itageuka kuwa CHADEMA kwa kuwa watetezi wa wanyonge kama walivyofanya CHADEMA miaka miwili au mitatu nyuma kisha CHADEMA itakuwa CCM kwa kukataa kutekeleza mambo ambayo ni zahiri ni tunu kwa taifa hili.

Pia tutegemee kubadilishana wanachama wakongwe na wakubwa ndani ya vyama hivi viwili. Kuna watu, hasa wenye kashfa mbali mbali za ufisadi ndani ya nchi, watahama kutoka ccm na kuhamia CHADEMA. Pia wapo wa CHADEMA wenye uchungu wa dhati na taifa hili watahamia ccm kwenda kuongeza nguvu katika vita dhidi ya ufisadi, ambayo ndiyo hoja ya CHADEMA halisi.

Ni suala la muda tu, usikimbilie kusema hili haliwezekani.
Nawasilisha.
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda katika taifa letu tutegemee ccm itageuka kuwa chadema kwa kuwa watetezi wa wanyonge kama walivyofanya chadema miaka miwili au mitatu nyuma kisha chadema itakuwa ccm kwa kukataa kutekeleza mambo ambayo ni zahiri ni tunu kwa taifa hili.
Pia tutegemee kubadilishana wanachama wakongwe na wakubwa ndani ya vyama hivi viwili. Kuna watu, hasa wenye kashfa mbali mbali za ufisadi ndani ya nchi, watahama kutoka ccm na kuhamia Chadema. Pia wapo wa chadema wenye uchungu wa dhati na taifa hili watahamia ccm kwenda kuongeza nguvu katika vita dhidi ya ufisadi, ambayo ndiyo hoja ya Chadema halisi.
Ni suala la muda tu, usikimbilie kusema hili haliwezekani.
Nawasilisha.

Ndiyo sababu CCM imeamua kuwanunua Madiwani na wabunge wa Chadema?
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,408
2,000
Si kusubiri muda tena....2015 ndio iliyobadili upepo wote ...pengine wengi bado hamjajua nini kinatokea nchi hii ...mtaelewa tu ...wengine hatukupenda kumpigia kura JPM lakini tulilazimika kuokoa taifa kwanza baada ya wenzetu kuamua kuwa vipofu ....sasa Taifa lipo salama pamoja na changamoto zake ....
 

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,500
2,000
Sijui unaizungumzia ccm gani! Lakini kama unaizungumzia hii ya mwenyekiti asiye na busara kwa wenye mitazamo na fikra tofauti na zake utachekwa na wafu
 

tusionacho

JF-Expert Member
Nov 23, 2016
274
1,000
Tatizo umeandika pumba kwa confidence kweli kweli ccm wamefeli ila maigizo kibao ndio maana wamewabana wapinzani wasifanye mikutano sababu hatujawahi pata kiongozi wa hovyo kama huyu hata bunge live analiogopa jinsi wanavyomvua nguo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom