Mtazamo:Wanachoweza kufanya CHADEMA ni kumvua Lowassa ujumbe wa kamati kuu lakini sio kumfukuza uanachama

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Iwapo Lowassa ataonyesha mwnenondo wa kutia mashaka ikiwamo kutohudhuria kikao cha kamati kuu cha leo bila kuwa na sababu za msingi au za kueleweka au mienendo mingine yoyote ile ya kutilia shaka katika siku zijazo, wanachoweza kufanya CHADEMA Kwa sasa,kulingana na mtazamo wangu,sana sana itakuwa ni kumvua ujumbe wa kamati kuu na si kumfukuza uanachama moja kwa moja.

Huu ni mtazamo wangu lakini pia unaweza ukawa ni ushauri wangu hasa endapo mzee huyu ataonenyesha mwenendo wa mashaka kwa siku zijazo ila natural justice ni muhimu sana hapa kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule.


Binafsi siwashauri CHADEMA kumfukuza huyu mzee iwapo tu atakuwa amekwenda Ikulu kwa mambo yake binafsi unless mmebaini ana agenda ya siri lakini msikilizeni na mjipe muda wa kutafakari kabla ya kuchukua maamuzi yoyote yale.

Hili la kusifia tulivumilie tu maana binadamu tunatofautiana uvumilivu na mitazamo ingawa kwakweli kusifu katika mazingira kama haya tuliyonayo sasa kunataka uwe na moyo wa chuma kutokana na huu unyanyasaji na ukandamizaji wa wapinzani unaoendelea.

Tusifanye dhambi ya kufukuza mtu waacheni waondoke wenyewe unless mnabaini kuna hujuma wanataka kutufanyia ingawa hata hii hamahama ni aina fulani ya hujuma ila tuipuze kwasababu katiba inawapa haki hiyo.

Tuonyeshe mfano wa uvumilivu tofauti na wengine ili mradi tu tuna hakika hatuhujumiwi.

Tukumbuke huyu mzee amekwenda Nairobi kumuona Lissu karibu mara mbili kama sikosei hivyo kama ni kupongeza tu basi tunaweza kumvumilia unlesa mnagundua jambo la tofauti.

Tukimfukuza kwasababu ya matamshi yake tu dunia haitatuelewa na tujiandae kwa propaganda nziti sana kutoka upande wa pili kuwa sisi ni madikteta,hatuheshimu uhuru wa mawazo kama tunavyolalamika sisi wenyewe,n.k.

Na kama sababu za kumfukuza zipo basi ziwekwe wazi na hakikisheni anapata nafasi ya kujitetea tofauti na hapo tutachafuliwa sana na tutaambiwa hatuna haki ya kulilia uhuru wa kutoa mawazo na kukosoa na huu ndio mtego unaotukabili katika kushughulikia hii issue

Tusisahau maadui zetu wanapenda kuona tunafarakana na watafanya kila juhudi na kutumia kila mwanya kufanikisha azima yao hiyo.

Vile vile,tofauti na mtazamo wa watu wengi,kikao hiki cha dharura huenda kimeitishwa mahususi kwa yeye kutoa taarifa ya nini hasa aliongea akiwa Ikulu na nini walikubaliana iwapo hakwenda kwa agenda binafsi ingawa alienda kimya kimya bila kutoa taarifa kwa wenzake na atapaswa kueleza sababu ya kushindwa kuarifu chama.

Pia, kikao hiki cha dharura kinaweza kuwa na agenda ya kumaliza au kuzika dalili ya mivutano iliyotaka kuanza kujitokeza baina ya wanachama na wajumbe wa kamati kuu baada ya Lowassa kutoa matamshi yale na pengine kuweka mikakati ya kuepuka hali kujirudia tena katika siku zijazo.

Tusubiri.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Huyu mzee bhana kaniboa vibaya sana, Ameshachoka ashauriwe tu apumzike siasa kabla Mambo hayajaharibika zaidi, ametukosea sana, SINA IMANI NAYE TENA.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Afukuzwe bila kusita. Utamfanya mwanachama wa kawaida lakini akatumia uzito wake kutoa kauli ambazo zitatafsiriwa kama kauli za chama,halafu tunabaki kujitetea badala ya kufanya mambo ya maana
 
Kama watu walivyotabiri kuwa alichoongea Lowasa sio walichojadili kuna kitu wamajadili ambacho ni siri, Labda yalikuwa yakuomba uzoefu wa nini kifanyike katika hali kama hii tuliyokuwanayo sasa Tanzania
 
Afukuzwe bila kusita. Utamfanya mwanachama wa kawaida lakini akatumia uzito wake kutoa kauli ambazo zitatafsiriwa kama kauli za chama,halafu tunabaki kujitetea badala ya kufanya mambo ya maana
Tukimfukuza kwa kosa la kupongeza tu dunis haitatuelewa kabisa na tujiandae kwa propaganda nzito sana iwapo atafukuzwa kwasababu hiyo tu.
 
Wengi hamuwezi kumuelewa mzee Lowasa, huyu ni bingwa wa siasa kuliko mtu yoyote Tanzania, mtakuja kumuelewa baadaye sana na siyo leo.
 
Tukimfukuza kwa kosa la kupongeza tu dunis haitatuelewa kabisa na tujiandae kwa propaganda nzito sana iwapo atafukuzwa kwasababu hiyo tu.

Salary slip una ushauri mzuri sana kwenye post namba moja. Cdm wala wasimfukuze bali wampe nafasi ya kueleza kile alichoongea na rais. Kisha wamueleza kutokana na nafasi mambo ya kufanya kama yeye binafsi inabidi awe makini kwani kinakiingiza chama kwenye malumbano yasiyo ya lazima. Cdm kama chama wakubali pia wakati ule walikosea sana kumuacha yeye akaenda Kenya kuhamasisha wamasai wa Kenya kumchagua Uhuru. Matokeo yake hata wanacdm wakaingia kichwa kichwa kumsupport Uhuru, baadaye uchaguzi ukaingia vituko vya ajabu.

Huyo Lowassa ni dhahiri hana mapenzi na cdm, na sidhani kama hata anajua chama kina wanachama wangapi, na lengo lake ni kuendelea kugombea urais kupitia cdm. Kuanzia sasa ni kumuonyesha na kumuweka wazi tu hyo nafasi ikifika 2020 hatoipata. Akishanyimwa hiyo nafasi atachapa mwendo mwenyewe. Kumfukuza kisa kamsifia rais sio haki, lakini kwa umri wake hawezi kwenda na kasi ya cdm. Ikumbukwe hata huko ccm aliondoka kwa kukosa nafasi ya kugombea urais, hivyo hata akikosa nafasi hiyo akaondoka ni rahisi kupangua propaganda zozote kwani itaonekana anahama vyama kwa kukosa nafasi kugombea urais.
 
Hii ndo nafasi pekee ya chadema kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Wanaweza kumwacha lakini akawa ndo mwiba zaidi hapo baadae na kupelekea chadema wakaanza kujilaumu kwamba wangechukua maamizi ya kumwondoa wakati uleule yote hayo yasingetokea.
Lkn pia wanaweza wakamwondoa kwenye nyadhifa zote au kumwachisha uanachama kabisa na chadema wakabaki salama japo kuna kamtikisiko katatokea wachukulie ni mambo tu ya kisiasa.
Mi nawashauri chadema anzeni muda huu kujipanga vizuri, kuandaaa strategies nzuri za hapo baadae, kuandaa kiongozi mzuri ambaye atakuja kupeperusha Bendera wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Achaneni kabisa na wazee hawa wa kuhamia. Mna watu wa kutosha kuwakilisha upinzani popote pale. Na la kuwakumbusha ni kwamba msiweweseke upinzani duniani kote huajwahi kuisha ila huwa unashamiri kila Siku ya mungu. Hata magufuli afanye mazuri mengi lakn upinzani utaendelea kuwepo. Upinzani ungekuwa unakoma baada ya nchi kuendelea basi sshv ulaya, afrika kusini au hata Libya wakati wa Gaddafi tusingekuwa tunaongelea upinzani, maanayake ungekuwa umefutika kabisa lakini ndo kwanza huko unazidi kushika mizizi.
Ko chadema fanyeni maamuzi kama chama na so kuangalia uwezo au sura ya mtu.
 
Tukimfukuza kwa kosa la kupongeza tu dunis haitatuelewa kabisa na tujiandae kwa propaganda nzito sana iwapo atafukuzwa kwasababu hiyo tu.
Kwa kitendo chenu cha kumsakama mara tu baada ya yeye kukutana na rais wa nchi, dunia tayari imethibitisha nyinyi ni akina nani! Yaani hadi mgonjwa ambaye yuko kwenye intensive rehabilitation unit huko Ubeligiji, akasahau ugonjwa wake na kuandika waraka mkali. Mmemwita msaliti kama mlivyomwita Zitto na wengine wengi huko nyuma. Mmemporomeshea matusi kibao na hadi mkaotisha kikao cha kamati kuu cha dharura kama mlivyofanya kwa Zito Kabwe wakati ule. Sababu tu kuwa ametumia uhuru wake wa kueleza yale anayona yanafaa hata kama ni tofauti na yale ambayo viongozi wakuu wa chama chake wanayoyaamini. Kwa hiyo dunia imeshathibitisha kuwa ndani ya chama chenu hakuna uhuru wa kujieleza (freedom of expression) kinyume kabisa na kile mnachokilalamikiaga kutoka serikali ya JMT.

It is too late as severe damage has already been done to the party. Huo uwezo wa kumfukuza kwenye kamati kuu hamnao. Kwanza ni nani huwa anachagua wajumbe wa hiyo kamati kuu? Tulimwona Nyarandu akihudhuria hiyo mikutano ya kamati kuu mara tu baada ya kuhamia huko toka ccm kama ilivyokuwa kwa Lowassa? Na Lowasa wala hatahudhuria huo mkutano wa kesho kama ajenda yake ni kumjadili yeye na kile alichoongea na JPM. Lowasa lazima atakibadilisha chama hicho kutoka kuwa cha wanaharakati wa haki za binadamu kuwa chama kistaraabu cha siasa chenye lengo la kukamata dola kwa njia ya kistaarabu. Watakaoshindwa kwenda na midundo yake ndiyo watahama au kufukuzwa kutoka kwenye chama. Just stay tuned till 2020.
 
Mange huko alipo haja post kitu... au haja pelekewa taarifa..... au na hili lina husiana na lile jengo pale... jirani na kwa gwaji... mkoromije....
 
Lowassa ahojiwe kama mleta post alivyoeleza. Tunatamani sana kama wanachama kujua zile sifa kwa rais zilikua zikimaanisha nini katika kipindi hiki kigumu kuliko vyote katika vyama vya upinzani nchini. Wakati huu washindani wakuu wa chama tawala hawakushiriki uchaguzi kukwepa mapanga yaliyoridhiwa na ofisi kuu ya nchi na dolla ndiyo yeye anaenda kusifu? Anamsifu aliyeruhusu mapanga kutumka katika chaguzi? Anamsifu aliyenyamazia chief whip wa upinzani bungeni kushambuliwa kwa bunduki za kivita? Anasifu watu kubomolewa nyumba brutally bila fidia? Anasifu uchumi hewa?
Nafikiri atakua na majibu kwa hiyo wananchi tutatamani kuyasikia. Vinginevyo achepe zake lapa akaanzishe chama kama ana ubavu huo, sio kupewa lift kwa gari lenye wenyewe na kuanza kuwafanyia vurugu.
Lowassa tulimpenda ila atambue tunaipenda nchi kuliko yeye na haki yetu ya ushiriki wa masuala yatuhusuyo kama raia huru kuliko maslahi yake binafsi. Watu tunawahitaji ila sii wao mbele ya chama bali chama juu ya yeyote.
 
FB_IMG_1515606353700.jpg
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom