Mtazamo wa Samuel Sitta kuhusu Zanzibar

Gogle

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
1,495
867
Naomba mumsikilize mheshimiwa akiongelea Zanzibar

kisha tujadili,
Yaani anamaanisha kwamba hata kama wazanzibari kwa wingi wao wakiukataa muungano basi Tanganyika haiko tayari?
Ni kweli zanzinbar haina uwezo wa kuzalisha Umeme wake?
Mengine nawaachia
 
sisi kina gogo la shamba tunamshangaa sana sita,ina maana tanzania bara na Zanzibar na Tanzania bara na Kenya wapi mbali?
 
Huyu mzee anazungumzia imagination story akijaribu kuchanganya na udini

Lakini anashindwa kueleza ukweli kwamba endapo demokrasia ya vyama vingi itashindwa kufata mkondo wake inaweza kuzalisha huo ugaidi anaouzungumzia

Nasikia anaandija vitabu kwa sasa ila nadhani main story ya hivo vitabu itakuo ndio hiyo story ya zanzibar kwamba ikipata uhuru wake itaivamia tanganyika na kuitawala .

Haya ni mawazo dhaifu yenye kupotosha .hii maanayake ni kua 'bora punda afe (wazanzibar) ila mzigo ufike (muungano ulindwe) .bila ya kujali wanzibari wanamaendeleo au hawana au wanaumoja au hawana .wanazikana au hawazikani ili mradi amani ipatikane tanganyika .zanzibar amani na umoja sio lazima

That is a typical figure of divide and rule in zanzibar
 
Sita ameliongelea hili swala kwa jujuu sana. Unapozungumzia umbali kwa kuzingatia kilometer, hutokuwa na sababu za kuwatenga wakenya, waganda warundi, nk... na wao pia wataongelea wasudani,waethiopia nk.. Muungano ni jambo jema ila linahitaji utayari wa wananchi kwa wakati huo. Ilikuwaje huko nyuma kabla ya muungano? Haya ya umeme na hizo power station zilikuwako? Mbona leo,Tanzania na Kenya wanauziana umeme (Taveta na Longido)? Sita atoe sababu zinginezo kubwa... na si hizi nyepesi nyepesi tu.
 
Kikubwa kinachoisumbua Zanzibar ni dini yao, isingekuwa hivyo CUF wangelishapewa mamlaka zamani sana
Kwa maoni yangu Sitta yupo sahihi kuweka hofu kwenye masuala ya usalama, wazanzibar si watu wa kuamini sana pamoja na kuipenda sana UKAWA ila kwa hili mtanisamehe.... hoja za currency, umeme na undugu hazina mashiko , kwani tuna ndugu wengi sana waliotapakaa duniani kote na wala hatuna uhusiano nao acha wa muunguno pengine hata wa kidiplomasia hatuna.
Suala la Kwamba Muungano hauwezi kuvunjwa kisiasa sidhani kama ni kweli, wazanzibar wakamua kuukataa muungano kwa ujumla wao wanaweza na hatuwezi kuwazuia... ni suala la muda tu, lakini ni vyema pia wakawa na uhuru wa kujiamulia mambo yao kama taifa, ikiwa ni pamoja na viongozi wanaowataka....
 
Kwa maelezo ya huyu mzee, zanzibar wasahau kujitawala kabisaaa. Maana sitta ni mtu mzito sana Tanzania ambae amesevu karibu serikali zote mtazamo wake ni lazima ndo mtazamo wa, chama na serikali.
 
Maneno yake huyu punguani mzee huyu, unganisha na yule waziri lukuvi Ndio utaona ccm walivyo majuha, zanzibar ni koloni la Tanganyika na viongozi wa ccm znz wanaendeshwa na remote ya ccm Bara
 
Nshu ya zanzibar Mimi sioni sababu ya kuyakuza
Kama wakiona wajitenge Poa maana sioni nachokipata kule
 
Duu kama maoni ya wazee wengi wa ccm ila ukimtoa Mzee Warioba yapo hivi basi sina budi kupasuka kichwa na kutokwa mishipa bure na swala la Zanzibar ni ndoa ya kikiristo hii
 
Babu anayo hamu ya kushuhudia intifada Zanzibar. Walk peacefully into the sunset mzee. Zanzibaris have God given right to determine their destiny. Hili halina mjadala.
 
Suala la kiusalama ndio hoja hapo mengine ni zuga tu, Ni suala zito lazima liangaliwe vizuri, Sitta anawakilisha mawazo yaliyopo serikalini.
 
Nafikiri upeo wa kufikiri wa mzee Sita umefika kikomo! Anashindwa kujiuliza kwanini Somalia ilikuwa nchi moja lakini mpaka leo wao kwa wao wanagombana? Hoja yake ya udini ni mufilisi.
 
Sema ukweli tatizo bundle huna.. Mnakaa mnatukana serikali kutwa nzima umu kumbe ata bundle ya kutazama youtu.be hamna mnatumika tu na matapeli wa ufipa.. Shame on you.
Wewe unashida sana, hivi ndicho ulichokiona u-share na waungwana humu jamvini? Jaribu kuwa na punje ya busara kwa jamii yako ndugu
 
Naomba mumsikilize mheshimiwa akiongelea Zanzibar

kisha tujadili,
Yaani anamaanisha kwamba hata kama wazanzibari kwa wingi wao wakiukataa muungano basi Tanganyika haiko tayari?
Ni kweli zanzinbar haina uwezo wa kuzalisha Umeme wake?
Mengine nawaachia


Nathani hiyo chupa hapo mezani ina viroba vya kutosha na ndio vilivyokuwa vinazungumza, sio rahisi mtu mzima kutapika utumbo namna hii, noti zenye picha ya madevu.... mzee pumzika salama ...
 
Back
Top Bottom