Mtazamo wa raia wa nchi za Afrika wanaoishi Ulaya na Marekani juu ya Hayati Rais Magufuli

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,689
2,000
Alikuwa na mabaya mengi kuliko mazuri,na alikuwa mtaalam wa propaganda kuliko hata hitler hao wanaomsifia walijazwa propaganda tu ni kama kagame tu,ana zuri moja tu ila mabaya mengi
Wewe mpuuzi tu
 
Micho

JF-Expert Member
Apr 12, 2009
328
250
Huyo jamaa anafanya kazi ikulu ya moja ya nchi za Africa Magharibi. Nilikutana nae jijini Siem Riep nchini Cambodia.

Anaesema sifa anazopewa Magufuli ni za kutunga basi ajiangalie tena.

Mimi binafsi naamini Mama Samia atafanya pia makubwa kwa upande wake maana yeye ni mwananfunzi wa Marais wawili Bora kabisa (JK & JPM).

Thanx for sharing..

Naona ulikuwa unambishia jamaa km chanjo haitakuja....na ikaja na bado vingine sasa watu wagundue how powerfull Magufuli was..kupambana na pressure za mabeberu si kazi nyepesi
 
Wasomba

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
247
500
Tanzanian President John Magufuli is in the country and working hard in his office, his prime minister said on Friday, squashing rumours that he has contracted coronavirus.
 
nusaki1974

Member
Apr 11, 2019
70
125
Huu upuuzi wa sukuma gang pele chato
Hata Hitler mussoline Amini dada bokasa museveni na madikteta wengine wengi wana watu wanaowaunga mkono na kuwasifia kwa sababu zao wenyewe kwa magufuli kila aliyemtazama kutokea angle ya nje na mbali atamuona kama hao rafiki zako ila njoo mtazame magufuli kama magufuli kwenye angle ya ndani utafahamu jina la kumuita mwenyewe.
 
Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
12,563
2,000
Thanx for sharing..

Naona ulikuwa unambishia jamaa km chanjo haitakuja....na ikaja na bado vingine sasa watu wagundue how powerfull Magufuli was..kupambana na pressure za mabeberu si kazi nyepesi
Mkuu,

Hatari sana. Huyo jamaa yupo njema sana.

He got a contract to work in South Asia and China on something and it was then that we met.

Anajua balaa. Hapo kuna msgs nyengine siwezi kuziweka hapa sababu za kiusalama.

But the guy is genius.
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,730
2,000
Kwenye madini alichofanikiwa ni kuanzisha mineral markets ambazo zimepunguza smuggling somehow
The rest is the same
 
Micho

JF-Expert Member
Apr 12, 2009
328
250
Mkuu,

Hatari sana. Huyo jamaa yupo njema sana.

He got a contract to work in South Asia and China on something and it was then that we met.

Anajua balaa. Hapo kuna msgs nyengine siwezi kuziweka hapa sababu za kiusalama.

But the guy is genius.

Pain...

Mkuu, very painful kumpoteza JPM

Failure isn’t losing its learning...may he rest in peace...
 
fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,952
2,000
Ndugu wana JF nimeona nishare na ninyi kile walichonieleza hawa marafiki zangu niliokutana nao South Africa kipindi nahangaikia ndoto zangu kuhusu mtazamo wao kwa aliyekuwa rais wetu JPM.

Kuna rafiki yangu raia wa Kameruni ila kwa sasa anaishi Marekani. Jamaa ni PhD wa uchumi na amefundisha baadhi ya vyuo hapo Johannesburg kabla ya kwenda Marekani kutafuta maslahi zaidi. Mwezi uliopita alikuja Tanzania baada ya kuzuiwa kuingia Australia ambako pia alikuwa anafanya consultation na makampuni flani yaliyokuwa yanahitaji huduma yake. Alipozuiliwa kuingia Australia kwa sababu ya restrictions za Covid 19 aliamua kuja Tanzania kupumzika hivyo nilipata wasaa wa kuonana na kuongea naye, maana tulikuwa hatujaonana zaidi ya miaka 10.

Huyu bwana alinishangaza sana kuhusu jinsi alivyokuwa anamwongelea JPM. Jamaa alikuwa anasema Tanzania tumempoteza rais bora. Acha ninukuu maneno yake. "Magufuli was the best president in Africa". Anasema "the guy was doing a good job"

Kiufupi jamaa anasema Magufuli alikuwa kiboko, na nchi alikuwa anaipeleka mbele. Nilijaribu kumwuliza kipi kinachomfanya aseme Magufuli alikuwa rais bora. Alisema yeye kama mwanauchumi na mfuatiliaji mzuri wa Siasa za Africa mambo aliyokuwa anayafanya Magufuli ni makubwa sana na hakuna rais yeyote wa Afrika mwenye huo uthubutu. Alitaja issue ya kusimamia madini na kuyabana makampuni ya kigeni kuchota madini ni kitu ambacho marais wengi Afrika kimewashinda.

Jamaa alikuwa anasema Magufuli alikuwa ni rais wa ajabu sana ambaye haogopi wazungu. Nilijaribu kumwambia mbona sisi humu nchini tunaona kama alikuwa anatupelekesha tu, tulikuwa hatuna uhuru hata wa kuongea, hofu imetanda, anaminya demokrasia. Jamaa akajibu hayo mambo ya kuminya demokrasia na kunyima uhuru hayaoni kama ni issue ya msingi ukilinganisha na kazi kubwa ya kuijenga nchi aliyokuwa anaifanya. Anasema huko nje (west Africa) Magufuli ni popular sana. Jamaa anasema Magufuli was the best president in Africa.

Kuna jamaa zangu wengine raia wa Zambia na DRC. Huyu wa Zambia ameoa muaustralia na anaishi Sydney na huyu wa DRC yeye yuko Durban South Africa. Wote hawa nikiwa naongea nao huwa wanasema Magufuli was the best president ever.

Pia kuna kidada flani kizungu kiraia cha Ireland (UK) kinaishi South Africa, ni kisanii yani kinaimba mziki tulikuwa tunasoma nacho chuo kimoja na pia tunasali pamoja huwa kinaniambia Magufuli alikuwa the best president. Kilikuwa very interested na siasa za Tanzania baada ya kumwona Magufuli akifanya usafi kule feri. Kuna picha kilinitumia ya Magufuli anafanya usafi kule feri amezungukwa na wauza samaki.

Binafsi sikuwa mshabiki sana wa Magufuli ila kusema ukweli nimeanza kushawishika na kuamini kuwa jamaa alikuwa rais mzuri. Nikiangalia ile miradi aliyoianzisha kwa muda mchache aliotawala, je kama angeendelea kuwepo kwa mhula mwingine ingekuwaje. Iangalie Morogoro road kutokea Kimara kuelekea Kibaha jinsi inavyopendeza utadhani nipo barabara za South Africa. Ukiweka pembeni mapungufu yake jamaa alikuwa anaipeleka nchi mbali sana.
Tumsamehe kwa mapungufu yake na tumwombee pumziko la amani huko aliko.
Mafisad na wafuasi wao hawatakuelewa,na wanaomchukia nchini ni 5% out of 100%
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
3,891
2,000
Sifa za uchochoroni siyo sifa kwanza hakujulikana Duniani!! Africa, alikuwa anapita ivi!......Mungu alimkasrikia akafa!! angalia clip za south africa kikwete alimfunika mbaya!

sikia weye bana kuba...hata shetani alipendwa sana, na Malaika waasi Mbinguni wkt ana ongoza maasi dhidi ya Mungu, ni wazi theluthi tatu ya Malaika walimuunga Mkono shetani! wakaondoka nae mpaka leo! ni kawaida kwa wapenda maovu wote!!

Hata njia ya kwenda mbinguni ni nyembaba sana wachache tuta pita humo! lkn la kwenda motoni ni kuuubwa sababu lina wafuasi wengi, najua ulifurahia watu kuuawa kwa marisasi mchana kweupee bila uchunguzi!!

sasa iko siku isiyokuwa na tarehe uchunguzi wa haya yooote yaliyo fanywa na huyu jiwe yatachunguzwa kwa kina na Historia itaandikwa upya! kwanza mbinafsi, mpenda sifa! burigi, uwanja wa ndege kijijini kwao wapi na wapi!!

Huyu Jiwe hata km mtamuunga mkono theluthi tatu ya wabongo bado ni mtu mbaya tu ''aliua bila chembe ya huruma kina AZoli Gwanda, Lisu, Ben saa Nane nk, walipotea mazimaaa, mpaka leo hatujui walizikwa wapi! jamani muuaji? unafurahi kabisaa!

tena basi wazi wazi! bila hata huruma? fikiria familia zao!! watoto walikuwa wanasomeshwa na hao Baba zao!! fikiria km Baba kipenzi ako ange fanyiwa hivo! ungekwenda South weye!! kisa Maendeleo?? yapi?

ivi kwanini aliwaua? aligonga mwamba kwa kijana Muhindi! lkn lengo ni ili afe! sasa jamani Roma Mkatoliki nae dogo yule alikosa nini jamani heee! eti unasema huyu wa hivi ni mtu mzuri kweli?

kwanza huko nje Duniani alimjua nani? hkn vyombo vya habari km vya magahribi kusema kwamba vita mtangaza faster nchi yenyewe ulimwengu wa tatu tu!! msijipe sifa kiviile!! huyo rafiki yako alikuwa mnafiki tu ili apate kuishi vyema kwenu!

Sasa ile Dhambi ilimtafuna manake mshahara wa Dhambi ni Mauti!! huyu jamaa alimdhihaki Mungu! kwa sababu alienda kanisani kushikana mikono na wachungaji! kutoa zaka na sadaka!

sadaka gani ya kumtumikia Mungu yenye Damu! za watu wake alio waumba!! hakujua kabisa kuwa ''Mungu hadhihakiwi'' shetani alimpofusha akili na macho! aibu sana kumshangilia muuaji na wewe umeshiriki tayari!

Nashangaa sana mtu una mshangilia mtawala muovu!! angalia kikwete nyerere wao walikuwa wanatubu kwa haki ya moyo kabisaa!! na wanalipia uovu wao!! lkn huyu? hakukumbuka kutubu! amekufa kawaacha kina kabendera!
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
3,891
2,000
Mafisad na wafuasi wao hawatakuelewa,na wanaomchukia nchini ni 5% out of 100%
Sikia dogo sisi kamwe hatumchukii Magufuri! msitulishe maneno ni dhambi pia kwenu km baba yenu huyo! ila tunacho chukia ni vitendo vyake vya kikatili dhidi ya Binadamu wenzake tena wabongo wa chini tu wasiokuwa na hatia, anao paswa kuwalinda,

Yeye angekuwa mbabe angeenda kusaidia nchi jirani zisipigwe na Al shaabab km Somalia na kenya, siyo kukimbizana na vijitu vidogo vidogo hivi !! Nyerere kidume kilikuwa frontline state! dhidi ya kaburu! na kweli ili tick!

afadhali hata angewafunga tu yakaisha lkn chuki za kutaka kuua kwa siri tena kwa risasi za moto bila kujali! km vipi si ange waita tu wampe mshiko! kwani unaona yule kijana muhindi alikwenda kumzika?

alikuwa anaua km anaua nzi! ili apate hela za ziada eti akaishi kwa anasa kijijini kwao tu basi! na kuwapendezesha wapiga kura wake! ni wazi Mungu hakupenda atawale, angesikia sauti ya Mungu nyikani angeishi mpaka leo! lkn kibri!!
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
3,891
2,000
Naona wazee wa legacy mko busy Sana wiki hii na nyuzi uchwara..

Awamu yote hamkuwahi kukanyaga Ulaya na US sasa roho inawauma mkiona mama anachanja mbugha..Ulaya anaenda na Kazi zinasonga..

Huyo jamaa yako kwa nini hakuja japo kufanya Kazi Bongo aone moto wa Dhalimu Jiwe? Au mwambie aende Rwanda alafu aje kusimulia upumbavu wenu hapa.

Jitu liliharibu uchumi,lilikuza deni la Taifa hatari tupu na lilikuwa katili,liongo na jizi afu unasemaje?
AChana nao hao mkuu wana test zari wametumwa na Makonda!! ili atoke chimbo! utawala gani haukudumu huo
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
3,891
2,000
Mere words is equal to rubbish,weka Audi visual sio maneno ya kutunga.

Huyo marehemu wenu mnajaribu sana kumhuisha lakini ni 🚮🚮 tu...decayed and will never come back

😂🙌 kuna siku itakuja hoja kuwa hakufa bali alipaa,mtakatifu n.k. wakati tunajua alikuwa ni shetani ,na msiba wake hakuna rais ata mmoja wa magaharibi aliehudhuria
Ina maana Ma Rais wenzake hawakumjua! labda wale wa EAC tu baasi! tena Musean tu wkt anapita Butiamakwa Mama yetu akasikia
 
Lecheminduroi

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
911
1,000
Ni rahisi sana mtu wa nje kumkubali Magu kuliko wa ndani ya nchi, huwezi sema kuminya democracy sio big deal ikiwa unajuwa wapinzani wapo zaidi ya 10m.

Yani ubomoe nyumba za watu Dsm na kuwaacha Mwanza kwasababu walikupigia kura!

Hao mabwege ni wakuwakutanisha na wazazi wa Ben Saa Nane pamoja na wahanga wa nyumba zao kubomolewa, amini nakwambia watabadili mtizamo wao.

Hayo ni machache tu kati ya mengi ambayo yanamuondolea mazuri ndugu mwendazake
 
Gamboshi 5

Member
Sep 18, 2021
37
125
Kuua na kupoteza watu, kupiga watu risasi, kuteka watu, kutaifisha mifugo, kufuga kundi la kuua watu almaarufu wasiojulikana, kupora uchaguzi kuanzia serikali za mitaa hadi serikali kuu, yeye ndiye chanzo cha kufa kwa soko la mazao mbalimbali n.k kiukweli haya mambo yaliwachefua Sana watz hivyo ukitaka kumpamba kwa hayo mema feki ni lazima utafute msaada kutoka nje lakini ndani ya nchi utapigwa kipigo cha mbwa coco
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
13,562
2,000
Ndugu wana JF nimeona nishare na ninyi kile walichonieleza hawa marafiki zangu niliokutana nao South Africa kipindi nahangaikia ndoto zangu kuhusu mtazamo wao kwa aliyekuwa rais wetu JPM.

Kuna rafiki yangu raia wa Kameruni ila kwa sasa anaishi Marekani. Jamaa ni PhD wa uchumi na amefundisha baadhi ya vyuo hapo Johannesburg kabla ya kwenda Marekani kutafuta maslahi zaidi. Mwezi uliopita alikuja Tanzania baada ya kuzuiwa kuingia Australia ambako pia alikuwa anafanya consultation na makampuni flani yaliyokuwa yanahitaji huduma yake. Alipozuiliwa kuingia Australia kwa sababu ya restrictions za Covid 19 aliamua kuja Tanzania kupumzika hivyo nilipata wasaa wa kuonana na kuongea naye, maana tulikuwa hatujaonana zaidi ya miaka 10.

Huyu bwana alinishangaza sana kuhusu jinsi alivyokuwa anamwongelea JPM. Jamaa alikuwa anasema Tanzania tumempoteza rais bora. Acha ninukuu maneno yake. "Magufuli was the best president in Africa". Anasema "the guy was doing a good job"

Kiufupi jamaa anasema Magufuli alikuwa kiboko, na nchi alikuwa anaipeleka mbele. Nilijaribu kumwuliza kipi kinachomfanya aseme Magufuli alikuwa rais bora. Alisema yeye kama mwanauchumi na mfuatiliaji mzuri wa Siasa za Africa mambo aliyokuwa anayafanya Magufuli ni makubwa sana na hakuna rais yeyote wa Afrika mwenye huo uthubutu. Alitaja issue ya kusimamia madini na kuyabana makampuni ya kigeni kuchota madini ni kitu ambacho marais wengi Afrika kimewashinda.

Jamaa alikuwa anasema Magufuli alikuwa ni rais wa ajabu sana ambaye haogopi wazungu. Nilijaribu kumwambia mbona sisi humu nchini tunaona kama alikuwa anatupelekesha tu, tulikuwa hatuna uhuru hata wa kuongea, hofu imetanda, anaminya demokrasia. Jamaa akajibu hayo mambo ya kuminya demokrasia na kunyima uhuru hayaoni kama ni issue ya msingi ukilinganisha na kazi kubwa ya kuijenga nchi aliyokuwa anaifanya. Anasema huko nje (west Africa) Magufuli ni popular sana. Jamaa anasema Magufuli was the best president in Africa.

Kuna jamaa zangu wengine raia wa Zambia na DRC. Huyu wa Zambia ameoa muaustralia na anaishi Sydney na huyu wa DRC yeye yuko Durban South Africa. Wote hawa nikiwa naongea nao huwa wanasema Magufuli was the best president ever.

Pia kuna kidada flani kizungu kiraia cha Ireland (UK) kinaishi South Africa, ni kisanii yani kinaimba mziki tulikuwa tunasoma nacho chuo kimoja na pia tunasali pamoja huwa kinaniambia Magufuli alikuwa the best president. Kilikuwa very interested na siasa za Tanzania baada ya kumwona Magufuli akifanya usafi kule feri. Kuna picha kilinitumia ya Magufuli anafanya usafi kule feri amezungukwa na wauza samaki.

Binafsi sikuwa mshabiki sana wa Magufuli ila kusema ukweli nimeanza kushawishika na kuamini kuwa jamaa alikuwa rais mzuri. Nikiangalia ile miradi aliyoianzisha kwa muda mchache aliotawala, je kama angeendelea kuwepo kwa mhula mwingine ingekuwaje. Iangalie Morogoro road kutokea Kimara kuelekea Kibaha jinsi inavyopendeza utadhani nipo barabara za South Africa. Ukiweka pembeni mapungufu yake jamaa alikuwa anaipeleka nchi mbali sana.
Tumsamehe kwa mapungufu yake na tumwombee pumziko la amani huko aliko.
Kama vile sisi Watanzania tulivyokuwa tunamuona Mugabe ni Rais bora au baadhi ya watanzania wanaomuhusudu Kagame na Rwanda yake.
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,396
2,000
Offcourse kwa propaganda za Magufuli, yeyote aliye nje ya nchi na si mfuatiliaji wa mambo kwa undani atamuona Magufuli kama hero. Maguguli alijua kucheza na akili za watu, alijua kufanya propaganda.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom