Mtazamo wa Raia Mwema kuhusu Nyerere na Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtazamo wa Raia Mwema kuhusu Nyerere na Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Feb 4, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hali ya mambo inavyoendelea hapa nchi hasa kwenye nyanja ya siasa imewalazimisha waandishi mahiri wa Gazeti linaloheshimika nchini mwetu "Raia Mwema", kuandika makala za uchambuzi wa kina ambazo kwa nyakati tofauti zimemtaja Mwalimu Nyerere Kama ni kiongozi maalum sana tuliyewahi kuwa naye kama Nchi. Sijui kama walipatana kumsifia Nyerere au ilitokea kwa bahati nasibu tu!!

  Maneno haya yako kwenye makala iliyoandikwa na Johnson Mbwambo!!

  Nyerere Alikataa NBC isiuzwe Mkapa akaziba masikio akaiuza kwa Shilingi Bilioni 15 kwa kampuni ya ABSA ambayo wakati huo huo ilikuwa imkopeshe Mkapa shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kuanzishia Kampuni yake Binafsi na Mkewe, ANBEM.

  Tunahitaji Rais Mwenye sifa kama za Michael Sata wa Zambia ambaye atakuja kurudhisha mali zote za Umma zilizouzwa kwa bei ya kutupa ama kwa mafisadi wa humu nchini au kwa wanyonyaji kutoka nje.

  Maneno haya yako kwenye makala iliyoandikwa na Ahmed Rajab

  Sina dhamiri ya kumpa Nyerere cheo cha uungu. Alikuwa binadamu na kama tulivyo wana wa Adamu alikuwa na makosa yake; makubwa na madogodogo. Mengine hayawezi kusameheka, mengine hayawezi kusahaulika.

  Hadi sasa Taifa hili halijapata kiongozi mithili ya Kambarage. Mithili yake kwa namna alivyoweza kulidhibiti Taifa, kwa kipaji chake cha kufikiri, kwa ulimi wake, kwa nadhari yake, kwa busara zake, kwa haiba yake na hata kwa ujanja wake.

  Simpambi bure. Miongoni mwa viongozi walioliendesha Taifa hili ni Nyerere pekee aliyekuwa na nyingi ya sifa za uongozi zinazohitajika. Waliomfuatia hawamfikii hata ukucha, seuze udole. Naweza kula amini kuwa hakuna hata mmojawao anayethubutu kujigamba kwamba ana uwezo wa kumpiku Kambarage. Si kwa hili si kwa lile.

  Pamoja na kuwa kiongozi wa chama, wa watu na wa Taifa Nyerere alikuwa hali kadhalika kiongozi wa viongozi. Hivyo, si ajabu kwamba aliwaweza Watanzania.
  Ndiyo maana miaka 13 baada ya mwili wake kulazwa kaburini bado tunamsikia kila siku akiukaripia ukabila, udini na ulaji rushwa.

  Maneno haya yako kwenye makala iliyoandikwa na Jenerali Ulimwengu

  Bima pekee inayoweza kuikinga nchi na maafa ninayoyajadili ni kujenga misingi ya uongozi unaosimamia haki kwa wananchi wote, uongozi usiovumilia matendo ya uonevu, dhuluma, wizi na ubabaishaji wa aina yo yote, uongozi ambao nimesema, na sina shida kurudia tena, tumeshindwa kuujenga tangu alipotutoka Mwalimu Julius Nyerere.

  Kama tunasema tutamuenzi Baba wa Taifa, hebu basi tumuenzi katika jambo hili tulilo nalo. Tukubali kwamba baadhi ya madai ya madaktari yanaweza kuwa ya msingi, lakini si yote. Waelezwe kwamba hata kama ni haki yao lakini madai hayo hayatekelezeki kwa sababu Serikali haina uwezo huo.

  Papo hapo, Serikali ifanye kazi ya kuonyesha kwamba ni Serikali isiyokuwa na uwezo, kwa kukomesha matendo yote yanayoashiria ni Serikali nono iliyovimbiwa, ikiwa ni pamoja na kukomesha mara moja posho zisizo na maelezo za wabunge; magari-viwanda yanayowabeba watendaji wa serikali; tiketi za daraja la kwanza kwa mawaziri; posho mbili mbili wanazolipwa mawaziri wakisafiri nje na ndani ya nchi… na kadhalika. Kwa ufupi, maofisa wa Serikali waache kuwaibia wananchi wao, matajiri wao.


  Baada ya kuzisoma makala hizi nikajiuliza ni kwa nini kama taifa tusikubali kutumia maono ya Mwalimu kama ndiyo Falsafa ya kuendeshea nchi yetu?


   
 2. Hercule Poirot

  Hercule Poirot JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Falsafa kuu ya Mwalimu Nyerere ilikuwa Ujamaa na Kujitegemea kama alivyoainisha ktk Azimio la Arusha 1967 na kufuatiwa na utekelezaji wake......Ajabu ya Musa ni kuwa Chama kilekile chenye katibaq ileile yenye kuabudu itikadi ya ujamaa na kujitegemea kinatupeleka kusiko julikana chini ya viongozi mufilisi walokosa dira wala nira ya maendeleo tunaenda tu kama twachukuliwa na mafuriko....Kuhusu ujamaa utatufaa nyakati hizi katika baadhi ya sekta haswa afya...elimu na makazi sekta nyingine twaweza achia uchumi huru ufanye kazi yake
   
 3. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mzee user name yako imenikumbusha Agatha Christie!!
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  That is Nyerere ambaye record ya mazuri na mabaya yake inajieleza wazi, wapi anastahili kukaa ukifananisha na hawa waliomfuatia. Kama tungepata watu wa kurekebisha makosa yake na kufanya zaidi ya pale alipotufikisha, naamini leo hii ingekuwa ngumu kumjengea hoja kwamba he was the man!
  Tumejiangusha wenyewe na tamaa zetu...kutojari kwetu....kudharau kwetu....na kubeba ego zetu juu kuliko maarifa yetu.
   
 5. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye Red:Ndiyo tofauti yetu na yeye!!
   
Loading...