Mtazamo wa mapenzi pesa unatufanya wanaume tusio na pesa tukose kujiamini katika mahusiano

Socw

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
1,304
2,583
Habari wakuu

Niko kwenye mahusiano na binti mmoja hivi. Huyu binti kiukweli anaonekana ni mstaarabu na mpole. Nipo naye kwenye mahusiano kwa muda wa kama miezi minne hivi. Huyu binti kiukweli si mtu wa kuomba pesa kabisa. Hajawahi niomba pesa kabisa, japo maisha yake ni anayoishi haingizi pesa kwa kuwa hana kazi na anaishi kwa ndugu huku akifanya harakati za kupata kazi.

Kitu pekee alichowahi kuniomba ni kuna siku nilimpigia simu akaniambia kuwa chaja yake imeharibika so anaomba nimsaidie chaja nyingine. Hata hiyo chaja yenyewe alipokuwa anaomba alikuwa anaomba kwa kujistukia sana, ni kama vile alikuwa anajisikia vibaya/aibu kuomba. Basi chap kwa haraka nikamtafutia na nikampelekea. Baada ya hapo ikawa kimya zaidi ya mawasiliano ya kawaida tu, hadi nikawa najistukia na kuanza kumnunulia vizawadi vidogo vidogo vya hapa na pale.

Kwa sasa niko naye mbali, halafu pia nimeyumba kidogo mfukoni. Kuna wakati nataka kumpigia niongee naye ila nakuwa najihisi vibaya kwa kuwa nampigia simu kila mara ilhali sim'support kifedha. Nadhani nimeathiriwa na mtazamo kuwa mapenzi ya sasa bila pesa hayaendi. Kuna ka hali ka kutokujiamini kanakuwa kananinyemelea. Nawaza kwa hali aliyonayo akitokea mwamba akaingia kwa gia ya pesa anaweza kumbeba huyu mtoto.

NB 1: Vijana tutafute pesa, pesa haleti mahusiano, ila inafanya ujiamini kwenye mahusiano.

NB 2: Ni jukumu la asili kwa mwanaume kumhudumia mwanamke wake.
 
Kabisa dingi,hitaji kubwa la mwanaume ni kusaidia wale wanaokuhitaji
 
Back
Top Bottom