Mtazamo wa ligi ya uingereza kuelekea msimu wa 2018/19

thanos

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,108
1,158
MTAZAMO WANGU KATIKA LIGI KUU UINGEREZA MSIMU HUU


Ligi kuu ya uingereza inazidi kua bora kila mwaka. Vilabu vina wekeza pesa nyingi kupata wachezaji wazuri pamoja na benchi la ufundi bora ili kupata matokeo yalio bora.... imekua sio ajabu kuona klabu kama wolves iki fanya usajili mkubwa kuliko vilabu vikubwa kadhaa vilivyopo kwenye ligi kwa mda mrefu.... tumeona karibia vilabu vikubwa vingi viki fanya usajili na kuboresha maeneo au nafasi zilizo onekana kua na mapungufu msimu ulio pita... leo nita ongelea vilabu vya top 4 msimu ulio pita kwa kuanzia...

MANCHESTER CITY
Tuanze na mabingwa awa wa msimu ulio pita... kikosi chao hakina mabadiliko makubwa na kilicho chukua ubingwa wachezaji wengi ni wale wale isipo kua wame fanya usajili mbili kwa kuleta winga kutokea klabu ya Leicester mabingwa wa epl mwaka 2015/16 na kumsajili beki kinda philipe sandler kutokea klabu ya uholanzi pec zwolle... uyu kinda tunajua ni kwa ajili ya mipango ya baadae na hatu tegemei kupata nafasi sana kwenye kikos cha kwanza na kama hato tolewa kwa mkopo basi uwenda akawa kwenye ile team ya vijana ya man city... na kuhusu mahrez wengi tunajua uwezo wake jamaa ana techique ana creativity mzuri akiwa na mpira mguuni ana dribbling ya hali ya juu.. msimu ulio pita kafunga goal 12 na assist 10... pamoja na uzoefu wake tuna tegemea ata ongeza kitu kwenye safu ya mashambulizi ya man city... tatizo linalo wakabili awa jamaa ni eneo la kiungo wa chini au mkata umeme... mchezaji pekee walie nae apa ni mbrazil fernandinho ambae umri ume mtupa mkono na kiwango chake kime anza kutetereka na ilo lili anza kuji onesha toka msimu ulio pita na pep guardiola aka ingia sokoni na kutaka kusajili viungo kadhaa lakin haku fanikiwa kusajili na ame nukuliwa kuwa uwenda hasi sajili kiungo dirisha ili na apo uwenda likawa tatizo kwa kikosi chake lakin uwepo wa watu kama gundogan na fabian delph una weza kidogo kusaidia japo sio viungo wakabaji halisia....

MANCHESTER UNITED
Awa ndio walio shika nafasi ya pili msimu ulio pita na ni moja ya timu zenye kikosi kizuri sana kwenye makaratasi.... msimu huu wamekua awapewi nafasi sana ya kufanya vizuri uki zingatia na pre season yao kutokua nzuri... timu hii imekua iki angaika sana kwenye dirisha la usajili kwa kukosa zile target zao... wame fanikiwa kumsajili mbrazil fred kiungo alie kuwa akiwaniwa na majirani zao man city pia wame msajili diogo dalot kinda kutoka fc porto pia waka msajili golikipa mzee grant kutokea stoke city... awa jamaa wana upungufu katika beki za pembeni kutokana na kukosa walinzi wa pembeni halisia na wengi tulitegemea kuona waki sajili beki za pembeni msimu huu lakin haijawa ivo... mbinu za kocha wao zimekua sio rafiki na wachezaji kiasi kwamba baadhi ya wachezaji wame onekana kushuka viwango vyao na wengine kutokua na mahusiano mazuri na mwalimu lakin kama waki jirekebisha mahusiano mazuri katika vyumba vya kubadilishia nguo na mwalimu aka jaribu kutafuta mbinu zitakazo endana na wachezaji alio nao basi uwenda waka fanya vizuri pengine kulitwaa kombe la epl ambalo ni misimu kadhaa sasa wamekua wakiona liki wapita.... usajili wa fred uta ongeza kitu kwenye eneo la kiungo la man utd jamaaa ana kaba vizuri ana passing ability nzuri pia ana uwezo wa kuanzisha mashambulizi pia ni moja ya wachezaji wenye uwezo wa kupiga mipira ilio kufa na hii ita ongeza kitu flani kwenye kikosi cha man utd....

Tottenham hotspur...
Washindi wa tatu hawa chini ya kocha kijana mauricio pochetino wamekua wakicheza kwa kiwango kikubwa kwa misimu kadhaaa lakin awaja fanikiwa kuchukua kombe la epl na kikosi chao hakina mabadiliko sana na ni moja ya timu zenye vikosi vipana na vikubwa.... hii ita saidia spurs kushiriki michuano mingi wanayo shiriki... kama beki wao mbelgiji toby alderweireld hata hama kikosi icho basi itakua ni vizuri zaidi kwao... kikosi chao kime kamilika kuanzia nafasi ya golikipa adi forward iki ongozwa na muingereza alie bora kwa misimu kadhaa harry kane...kurudi kwao kwenye uwanja wa white hart lane kuta changia kitu katika mechi za home... tatizo la spurs limekua ni kukosa consistency katika matokeo yao na kama waki jirekebisha basi uwenda wakafanya vizuri zaidi msimu huu..pia spurs ina kabiriwa na kua na wimbi la wachezaji walio na majeruhi ya mara kwa mara na hili uwa tatizo sana kwenye mashindano wanayo shiliki... na team ime tengenezwa kumzunguka harry kane pale anapo kosekana basi team uwa ina tetereka kupata matokeo..... uwenda huu ukawa mwaka wao...

LIVERPOOL
majogoo wa jiji hawa ndio team ilio pewa nafasi zaidi ya kubeba kombe la epl msimu huu na kukata ukame wao wa miaka mingi... team ime sajili usajili bora kabisa katika ligi wame ziba mapengo na nafasi zilizo kua na mapungufu na wame boresha baadhi ya maneno pia... wame fanikiwa kuvunja rekodi ya dunia kwa kusajili golikipa bora kabisa kutoka as roma ya italia kwa kiasi cha paun 66 million na moja ya maeneo yalio onesha mapungufu katika kikosi chao ni pamoja na eneo la golikipa hivyo wame tibu tatizo lao la kwanza pia walikua waki kabiliwa na tatizo katika kiungo hasa hasa kiungo cha chini na wame fanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kusajili mbrazil kutokea klabu ya as monaco ya ufaransa kwa kitita paun million 37... na hakuna shaka wengi tuna utambua uwezo wa fabinho katika kiungo... jamaaa ana kaba sana pia ni mzuri kwenye ku intercept mipila ya wapinzani na kufanya clearance katika lango lake pia ni mzuri katika passing ambapo msimu ulio pita ali kua pass acurracy 87% ambayo ni nzuri sana pia uwezo wake wa kucheza beki ya kulia uta ongeza kitu kwenye defence ya liverpool... Liverpool awakuishia apo waka mleta kiungo bora kabisa kutoka klabu ya ujerumani nae uyu nik kijana wa ki africa naby keita.. liver wamekua waki muwinda kwa muda kidogo na sasa wame kumsajili... moja ya vitu bora kabisa vya uyu jamaa ni lile jicho lake...jamaa ana penyeza pass katika maeneo muhimu na kwa muda sahihi pia jamaa ana fighting spirit ya kipekee kabisa itakayo fanya aweze kwenda sawa kabisa na ligi ya uingereza.... pia ana dribbling nzuri kabisa na ana uwezo wa kuanzisha mashambulizi pia ana changia kwa kiasi kikubwa katika safu ya ulinzi... nafikiri ukitoa allison becker basi hii ndo sajili bora zaidi kufanywa na Liverpool... box to box mid ya nguvu kabisa... na kapokea baraka za kutosha kabisa ikiwa pamoja na legend wa liverpool steven gerrard kumruhusu muafrica uyu kuitumia jezi ya heshima namba 8.... klop aku ishia apo aka ongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji kwa kumsajili winga matata kutoka klabu ya stoke city nae uyu ni xherdan shaqir... kwa uwezo wa shaqiri na pamoja na ule utatu mtakatifu wa salah mane na firmino tuna tegemea kuona mabao mengi zaidi msimu huu... kutokana na mfumo wa gegen pressing klop ali hitaji wachezaji wengi kwa ajili ya back up na ame wapata na wenye ubora .... tatizo la Liverpool ni kupata majeruhi ya mara kwa mara kwa baadhi ya wachezaji lakini mambo mengi yapo sawa na uwenda ika timiza ndoto yake ya kukata ukame wa miaka mingi....

Huu ndo mtazamo wangu msimu huu.. naomba kuwasilisha....

Kwa yoyote alie na blog na ana hitaji kupata makala kadhaa kuhusu soka ndani na njee ya nchi ana weza kuni PM au kutuma ujumbe katika email yangu [email
 
Kwa iyoo liverfool ndo anabeba ndoo msimu huuu,, ubingwa unabaki man city,,,,, mengine dakika 90 zitakuwa zinaamua
 
Kwa iyoo liverfool ndo anabeba ndoo msimu huuu,, ubingwa unabaki man city,,,,, mengine dakika 90 zitakuwa zinaamua
Kwa hii comment inaonyesha dhahiri shahili unatokea mtaa wa unyumbuni
IMG-20180610-WA0016.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom