G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Kuweka kumbukumbu sawa, jengo la Tanesco Ubungo liligharimu zaidi ya Tshs. bilioni 51 za kitanzania fedha ambazo ni za walipakodi waliowekeza PPF. Kwa sasa PPF wanapata return on investment kupitia Tanesco. Sina uhakika kama mrejesho wa fedha umeshakamilika kutokana na wapangaji hao Tanesco.
Kupanga ni kuchagua, hapa sitaongelea kabisa jengo la wizara ya maji ambalo nalo lina gharama zake
Kupanga ni kuchagua: Interchange vs PPF tower (Tanesco Ubungo)
Kwanza kuna miradi mitatu inayoendelea ya kuhamishia mabasi yote yanayoenda kusini maeneo ya Mbagala, mabasi yote yanayoenda kaskazini kupitia Morogoro yatahamishiwa maeneo ya Mbezi mwisho na mabasi yote yanayoenda kaskazini kupitia Tanga yatahamishiwa eneo la Bunju. Easiest project with minimum initial coast.
Kwa maana hiyo tayari hiyo interchange ya Ubungo hapatakuwa na foleni ya mabasi makubwa ya abiria! Hapatapita basi lolote la abiria baada ya mradi huu wa stand mpya.
Pale sasa patabakia kupita malori yatokayo bandarini +daladala+magari binafsi.
Aibu Aibu Aibu kwa nchi yetu iliyojaa pori lote lile la kurasini na vibanda vile ambavyo ni rahisi sana kulipa fidia, bado tunaruhusu malori yanayoenda Morogoro eti yapitie kurudi Ubungo! Aibu!
Kwa utafiti wangu nilioufanya malori mengi sana yanayotoka bandarini yanaishia ku-divert pale Chalinze kuelekea sehemu nyingine kupitia Morogoro. Kwanini tuyazungushie Ubungo? Vichwa vyetu tumewekeza kwenye "bomoa" yenye gharama kubwa baadaye.
Kama tutafanikiwa kujiongeza kidogo tu kisha tukajenga njia maalum ya malori ambayo kwenye tozo tu tutapata hela nyingi na ukaguzi wa uhakika basi tutakuwa tumeyaondoa barabara ya TAZARA kuja Ubungo kwa gharama ndogo sana. Sasa pale Ubungo patabaki kupita daladala za kwa Kimboka na vijigari aina ya vipasso! Hawa ndo wawekezewe flyover zitakazogharimu mabilioni kwa mabilioni?
Wakati Magufuli akisema "Vunja" Magufuli huyohuyo atakuja na ubunifu mwingine wa kodi za hovyo ili aweze kujenga wizara nyingine ya maji (Hata kama mnahamia Dodoma mnaweza kupangisha pale na bado mkatengeneza hela.
Nilitembelea China mji wa Shanghai juzijuzi, aisee kujenga tena ma flyover ni ushamba kwelikweli. Watu wanajitahidi kutanua miji ili watu wasambae, kujenga metro system ili watu wasafiri mbali kwa haraka na kuwa huru kuishi maeneo ya mbali baada ya kuwa na uhakika wa usafiri wa metro system, nyie mnaenda kwenye fly over za kupigia picha? Kuvunja majengo ambayo mtalazimika kuyajenga upya?
Mbaya zaidi ukitoka tu pale Ubungo unakutana na foleni Magomeni, mita chache tu kutoka Ubungo! Umerahisisha nini?
Tufanye hivi: Tayari tuna mradi wa mwendo kasi (njia za kupita mabasi makubwa ya abiria bila kuchanganywa na usafiri mwingine) Huu ni mradi mzuri ambao unahitaji tu kuongeza network na mabasi mengi. Hapo unaendelea kupunguza idadi ya vigari barabarani kutokana na uwekezaji huo. Mimi niliwasifu China. Huu mradi waliiga kila kitu kutoka kwetu ila wao wameenda mbali kutumia mabasi ya umeme! Ingawa mradi huu kule kwao hauna maana sana kwani wana metro system ambapo mtu anaweza kuingia mjini kwa haraka sana kutokea vijijini ila wao metro system yao pia hawakuhangaika kuvunja towers zenye bado kudai kimuonekano ( zinazouza nyago kama yale ya Tanesco na maji). Wao waliipitisha chini kwa chini na pale walipolazimika kuileta juu basi waliepuka sana vitu vya gharama. Treni moja inaweza kuchukua watu zaidi ya 2000 na kwa uhakika wa safari pia haraka. Huko ndiko kuwekeza (long term project) Siyo kuja kujenga fly over za kuuzia sura tena ukitoka tu mita chache mbele unakutana na yaleyale. Nimekaa nchi za watu, nimegundua kuwa fly overs ni useless na hawawekezi tena kwenye huo upuuzi!
Kuna wadau huko wanasema kuwa kuna mradi wa reli ambapo train zitakuwa zinatoka bandari ya Dar kwenda hadi Kwala ambapo patajengwa Bandari kavu, huo ni mradi mzuri ambao utaondoa malori kuja katikati ha mji. Sasa hiyo interchange ya nini? Itatulipa? Vipi kuhusu junctions kibao kuanzia pale Shekilango?
Daah!