Mtazamo wa jaji warioba na jaji mkuu kuhusu chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtazamo wa jaji warioba na jaji mkuu kuhusu chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Far star, Nov 21, 2010.

 1. F

  Far star Senior Member

  #1
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wale mnaofuatilia habari, jana warioba alipoulizwa kuhusu mtazamo wake juu ya chadema kutoka nje ya bunge alisema'' kutoka nje wakati MTU mmoja anaongea siotati'' na hata hivyo chadema hawajakiuka kifungu chochote cha kanuni za bunge,vile vile Jaji mkuu nae alisema kwa jinsi anavyo fahamu hakuna kifungu kilichokiukwa ispokuwa ni swala la ustaarabu.pia wakubwa hao walisema haya mambo yanaweza kujadiliwa tu kwani katiba ni kitu kinachoishi hata hivyo katiba imeisha badilishwa mara kibao tangu kutungwa kwake 1977,pia warioba alisema ni swala la kuangalia kwamba katiba ilele iendelee kuwekewa viraka au itungwe mpya na wananchi wataamua wenyewe.sasa ccm wanalalamika nini,chadema imewakosea wapi na kwa kukiuka kifungu gani ambacho wao wanakijua ambacho Jaji mkuu mstaafu pamoja na Jaji mkuu wa sasa wasichokifahamu.Jamani mambo haya hayaendeshwi kwa hisia tu,yanataratibu zake.Mtu hawezi kukurupuka na hoja zake binafsi ambazo hazijulikani, tatizo ccm wamezoea kupeleka washangiliaji bungeni kama vile wanaenda nje ya nchi kucheza mpira na hivyo kwenda na washabikiaji na washangiliaji, mtu ukimuuliza chadema wamevuja kanuni gani ,hajui lakini anashangilia tu ccm ccm ccm ccm sasa jamani wana ccm bungeni sio mpirani ambapo unaweza kushangilia tu hata timu yako ikifungwa,na ndio maana ccm walikuwa wana shangilia na kupiga mafoki wakati chadema walipokuwa wakitoka nje bunge.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Point of correction, Warioba ni Waziri Mkuu mstaafu, si Jaji Mkuu mstaafu.

  Pili, walichosema hapo, kwa mtu anayefuatilia mantiki, ni sawa na kusema CHADEMA wamefanya show tu isiyo na kina, kama wangetaka kuchukuliwa seriously wangekataa kuapishwa au kupigia kura mapendekezo ya rais.
   
 3. F

  Fareed JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wakatae kuapishwa ili wapoteze Ubunge wao? Huo ungekuwa ni ujinga. CHADEMA wamefanya kitendo cha kishupavu kutoka nje ya Bunge wakati Kikwete anaongea. Hii ni mara ya kwanza kutokea Tanzania ndiyo maana watu wanashangaa sana na wasiojua sheria wanasema eti CHADEMA wafukuzwe Bungeni. Wacha wafukuzwe Bungeni kama alivyofukuzwa Zitto na ukawa ndiyo mtaji wake kisiasa.

  Walkout ni jambo la kawaida sana kwenye demokrasia, walikuwa wanatimiza haki yao. Nchi nyingi sana duniani jambo hili linatendeka.
   
 4. D

  DENYO JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Chadema ni chama makini sana kina wabunge makini kina vichwa makini -mbunge mmoja wa chadema mfano tundu lissu au vicent nyerere au mdee ni sawa na wabunge 50 wa ccm wanaoshangilia na kusinzia bungeni bila kujali nini wanashangilia. Chadema imeleta vizazi vipya sugu, wenje, lema, mnyika, silindi, prof. Kahigi wakiongozwa na kamanda wa anga hon freeeman mbowe kiungo mchezeshaji ni sawa na barca au madrid
   
 5. F

  Far star Senior Member

  #5
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AAAA Denyo we ni noma jo, unajua Denyo humu JF kuna watu wanashabikia vitu kwa sababu wazazi wao ni ccm ,lakini ukweli siokwamba hawaujui,wanajua kila kitu kabisa.sasa waache ''wajifanye'' hawajui ukweli jo.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Hakuna legal strategy, ni show tu. Hata ukitaka kusema wametaka kushinda in the court of public opinion utaona wamewagawanya watu tu zaidi, miongoni mwao wakiwa supporters wao. Kwa sababu kitendo hiki hakina mantiki zaidi ya show na PR.

  Mimi nataka kujua strategies zao za kubadili katiba na sheria za uchaguzi, hizi habari za kutoka bungeni hazibadilishi kitu kama walivyosema hao washua.
   
 7. K

  Kasesela Member

  #7
  Nov 21, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jaji Warioba alikuwa ni Mwamasheria Mkuu kabla ya kustaafu na kugombea ubunge ambapo aliteuliwa na Raisi Mwinyi kuwa Makamu wake wa Raisi na Waziri Mkuu kabla ya Mh. Malecela. Aidha ni Jaji wa kuteuliwa katika maswala ya bahari chini ya Umoja wa Mataifa. Naamini swala la maana hapa ni kwamba utaratibu wa kutoka nje wakati kiongozi msiyempenda akiongea ni wakawaida duniani kote penye demokrasia. Utaratibu huu upo mabunge yote huru, ulifanyika sana wakati wa Mh. Moi wa Kenya, umefanyika na wafuasi wa Mh. Besigye kweye bunge la Uganda kumpinga Mh. Museveni, umefanyika India sana, wakati wa General Musharaf ulikuwa wa kawaida Pakistan, nako Iran baada ya uchaguzi wa mwaka huu, Ireland, Philipines, na hata kwenye general council ya Umoja wa Mataifa. Ni mwaka huu tu viongozi wa Marekani na Ulaya waliondoka ukumbini wakat Raisi wa Iran anaongea. Jipya ni kwamba Tanzania Bara tangu Uhuru hili halijawai kutolea. Watu wameamka, tutaona mbinu nyingi za wanaowapinga watawala waliopo zikitumika kwa mara ya kwanza.
   
 8. F

  Far star Senior Member

  #8
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huna jipya ww nyiendio mafisadi wenyewe
   
 9. M

  Mpendagiza Member

  #9
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa na ma-jaji wanawaambia jamaa wlikuwa right so mnaendelea kubisha nini hapa,tafuteni mbinu mbadala ya kulipa kisasi na ndiyo maana aliyesusiwa kakaa kimya
   
Loading...