ShalomP
Member
- Jun 14, 2019
- 97
- 154
Katika Taasisi za Elimu, taasisi za afya, kwenye mashirika binafsi na mashirika ya kiserikali na makampuni mbalimbali, kuna baadhi ya vijana ambao wapo wanafanya kazi kwa kujitolea (volunteering).
Tena wanafanya kazi kwa moyo wa uzalendo unaweza ukadhani tayari wameajiriwa kumbe bado. Taasisi za elimu na afya kuna walimu, manesi na madaktari wanafanya kazi kama volunteer ili kutopoteza ujuzi wao na taaluma yao.
Pia hujijengea uzoefu wa kutosha hasa katika soko la ajira na wanajifunza jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali eneo la kazi. Wapo waliojitolea kwa muda wa miaka miwili, mitatu na minne. Lakini zinapotoka nafasi za ajira hawapewi kipaumbele, tofauti na miaka ya nyuma volunteer walikuwa wanapewa kipaumbele kwenye nafasi za ajira pindi zinapojitokeza.
Mamlaka zinazohusika, ni maombi yangu hawa volunteers waliojitolea kwenye taasisi za elimu na afya kwa miaka miwili, mitatu wapewe vipaumbele. Pia, wangeruhusiwa hata kupeleka maombi kwenye vituo vyao vya kazi kwa wakuu wao au halmashauri wanazotokea. Wengi wao wanafahamika kwenye vituo wanavyofanyia kazi.
#Kuwa mzalendo, ipende nchi yako. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania .
Angalizo: Mtazamo wangu hauna uhusiano na itikadi ya chama chochote. Lugha za kumkashifu mtu yeyote au kiongozi yeyote au mamlaka yoyote haziruhusiwi.
Nawaheshimu wote, nawapenda wote. Peace and love!
Sent using Jamii Forums mobile app