Mtazamo: Tundu Lissu atafanikisha Godbless Lema kuondoka nchini Kenya na kupata hifadhi katika nchi mojawapo ya Ulaya au Marekani

Impact gani wakati.kakuta kuna wabunge yeye kawafuta na kupata mmoja?
Sikunakirudi.tena watu watakuwa na hasira nae wasipo mdunda watahama chama wote wamuachie chama yeye mwenyewe.
Wabunge wamefutwa na yale mabegi meusi, msidanganyane kama watoto.
 
Jamaa ameweka heshima hata Nyerere hajawahi kusindikizwa na balozi yeyeto
Wamemsindikiza au wamemfurumsha? Just leave us alone, Mr; nothing to which you come close ever survives! Look at Mr Mbowe and his CHADEMA, now! All because of your uncontrolled, dirty words & untamed, rushy feet!
 
LEMA NA NYALANDU ACHENI KUKIMBIA MADENI,DAWA YA DENI NI KULIPA
Leo imesambaa taarifa mitandaoni ikiwaonyesha wabunge wa Zamani Godbless Lema na Lazaro Nyalandu ambao imeonekana wakijaribu kuvuka mipaka ya Nchi na kukimbilia nchi jirani ya Kenya kwa Mida na Siku Tofauti Huku wakisema Chanzo ni Kutishiwa maisha yao,Lema amekamatwa jana akivuka mpaka wa Namanga Bila Pasi ya Kusafiria huku Lazaro Nayalandu akikamatwa leo akivuka mpaka huo huo wa Namanga bila Pasi ya kusafiria.
UKWELI NI HUU:
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge Job Ndugai,zimethibitisha kuwa Godbless Lema aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Anadaiwa zaidi ya Milioni 330 na ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyodhaminiwa kwa mshahara wake ambazo alichukua kwa ajili ya kufungulia kiwanda chake jijini Arusha kupitia Benki ya CRDB Jijini Dodoma mwaka 2015,pia alichukua Mkopo mwingine wa dharura wa Tsh 442 Milioni alizochukua toka Benki ya Stanbic Bank Jijini Arusha mwezi julai 2020 kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020 na mwisho wa mkopo huo ulikuwa mwezi November 2020 ambazo aliahidi angelipa kwa mkopo mwingine wa bunge aliotegemea angechukua endapo angeshinda ubunge Arusha Mjini 2020 ambapo ameshindwa ubunge hivyo imeonyesha wazi hajalipa deni hilo.

Lazaro Nyalandu rekodi za mabenki toka chanzo chetu kinaonyesha Tarehe 20/3/2014 alikopa kiasi cha Tshs 251 milioni toka Benki ya Standard Chartered ya Jijini Dar es Salaam ambapo hadi sasa imefichuka ana deni zaidi ya Tshs 508 Milioni ambazo zimeongezeka kutokana na deni hilo la muda mrefu na linazidii kuongezeka kwani yeye ameshindwa kulipa deni hilo tangu mwaka 2014 alizokopa akiwa mbunge wa Singida Kaskazini kipindi Hicho akiwa CCM Kabla ya kutimkia CHADEMA ambapo mwaka 2020 alikopa Tsh 204 Toka Benki ya Exim ya Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kampeni za Ubunge Jimbo la Singida kaskazini ambapo hakushinda.
Kwa Taarifa zilizonaswa imesemekana Kabla ya wanasiasa hao wa Kambi ya Upinzani kujaribu kutoroka kumbia nchini inasemekana walipewa Barua kwa nyakati tofauti za kukumbushia Madeni hayo amabyo inaonekana wamekuwa wakipiga kalenda na ndiyo chanzo cha wao kutaka kutoroka kwa kuvuka mipaka ili watimkie Marekani au Nchi moja ya Ulaya kama ambvyo wameshapanga.
Paulo Motika Laizer
Arusha
9/11/2020
Duh!!!
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽 Thank you 🙏🏽
Chadema ni viongozi au wanachama wake? kama unadhani ni viongozi hawa waliopo huwaoni?

Lissu aliondoka then akarudi bado akawa na impact kubwa tu, bado hujifunzi? na Lema pia itakuwa hivyo hivyo.

Chadema ilikuwepo, ipo, na itaendelea kuwepo.

That day hawa watu wakirudi moto utawaka vile vile, spirit never die.
 
Kwa mtazamo wangu, pamoja na Godbless Lema na familia yake kupewa hifadhi ya kisiasa nchini Kenya, Lema na familia yake watakuwa salama zaidi iwapo wataishi nje ya region hii ya Afrika Mashariki na zaidi wakiwa Ulaya,Marekani au kwingineko licha ya ukweli kuwa hadhi ya ukimbizi aliopewa nchini Kenya inatosha kumhakikishia usalama wake.

Hivyo ,ninaamini Tundu Lissu akiwa nchini Ubelgiji, anaweza kufanya mipango/kushawishi nchi za ulaya hasa Ubelgiji atakokuwa anaishi, kuhakiisha Lema na familia yake wanahama nchini Kenya na kwenda kupata hifadhi katika mojawapo ya nchi za Ulaya,Marekani au katika nchi nyingine tofauti na Kenya ambapo anaweza kukaa kwa muda tu.

Ni imani yangu pia Lissu atafanikisha mambo mengi ya kusaidia wapinzani wenzake pamoja na vyama vya upinzani akiwa huko ughaibuni-anakwenda kuanzisha movement za kusaidia mabadiliko akiwa huko Ulaya pasipo kuvunja au kukiuka mashariti ya kupewa hifadhi katika nchi za watu.

Muda utaongea.
Aiseeee !!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom