Uchaguzi 2020 Mtazamo: Tunakoenda watu watakuwa tayari kujitokeza na kuitikia wito wa maandamano ya amani kuliko kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,486
2,000
Kwa yanayoendelea,wananchi wanapata picha kuwa hakuna tena uchaguzi na hivyo hakuna maana yoyote ya kushiriki mikutano ya kampeni kwani hakuna tena kinachoitwa uchaguzi kwa maana ya uchaguzi kwa sifa zake.

Hivyo, wananchi hawa wataamasika zaidi kuitikia wito wa maandamano ya amani kuliko kwenda kwenye mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa kwasababu mpaka sasa mikutano hii imeshapoteza maana kutokana na idadi kubwa ya wagombea wa upinzani katika ngazi zote isipokuwa uraisi kuenguliwa, huku zoezi hilo likionekana kuendelea licha ya muda wa kufanya hivyo kisheria kuwa umepita.

Wananchi hawatakuwa na hamasa ya kuhudhuria mikutano ya kampeni bali mioyo yao itaguswa zaidu na wito wa kuandamana kwa amani kudai uchaguzi ulio huru na wa haki na kudai wagombea wa upinzani walioenguliwa warudishwe.

Kwa mtazamo wangu,huku ndiko tunakoelekea kutoka na ukweli kuwa mpaka sasa swala la uchaguzi limeshapoteza maana na hamasa miongoni mwa wananchi.
 

voicer

Senior Member
Jul 13, 2020
169
250
WATU WANATAKA SERA SIO MATUSI NA KEJELI KWA YALE YALIYOFANYWA NA SERIKALI.

AHADI CCM IMETIMIA SASA TUNAENDA KUTEKELEZA OCTOBER 28
JPM AMETOSHA

FB_IMG_1592381992236.jpg
 

Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,739
2,000
Vipi mmeandamana leo?., Wabunge mnalipwa milioni 12 kwa mwezi na marupurupu kibao na hamkumbukagi mnakotoka nani wa kuandamana apigwe kwa ajili yenu?.. Huwa sielewi nani anawadanganya upinzani mnakubalika kwa wananchi.

Watanzania ni watu tofauti na mnavyodhani. Waweza kuongea pumba wakashangilia Ila siku ya kuandamana huwaoni. Yote aliyofanya JPM yanaonekana nyie endeleeni kupiga kelele mitandaoni, mtaandamana kwenye Keyboards tu na vi smart phone vyenu.
 

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
5,508
2,000
Ngoja tusubiri tume watoe majibu ya rufaa wakileta ubabaishaji tunaingiza raiya rodini kwa amani.
Mnasubiri majibu gani wakati jana lissu kasema maandamano yanaanza leo? Au hujui kuwa tune imeshatangaza majina ya wabunge 18 wamepita bila kupingwa.
 

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
5,508
2,000
Vipi mmeandamana leo?., Wabunge mnalipwa milioni 12 kwa mwezi na marupurupu kibao na hamkumbukagi mnakotoka nani wa kuandamana apigwe kwa ajili yenu?.. Huwa sielewi nani anawadanganya upinzani mnakubalika kwa wananchi. Watanzania ni watu tofauti na mnavyodhani. Waweza kuongea pumba wakashangilia Ila siku ya kuandamana huwaoni. Yote aliyofanya JPM yanaonekana nyie endeleeni kupiga kelele mitandaoni, mtaandamana kwenye Keyboards tu na vi smart phone vyenu.
Pamoja na kulipwa hiyo mil 12 bado wanataka kutuchangisha fedha. Mwaka huu hatutakubali kuchangaboesa yoyote
 

niachiemimi

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
2,977
2,000
Chadema tuliwaonya humu kua siasa za uzushi,chuki na kupinga kila jambo hazitawajenga kwa muda mrefu. Jana mumeanza kuipata kali ya uchaguzi.

Maandamano alishindwa mange, ukashindwa ukuta, sijui munajipya gani. Bungeni mhe msigwa alipata kusema maana ya neno insanity.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom