Mtazamo: Tanzania haina wafanyabiashara wa Petroli

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,580
4,262
Kwa mtazamo wangu Tanzania haina wafanya Biashara wa Petrol bali ina wasambazaji wa Petrol

Hii ni kwa sababu, Petrol inanunuliwa kwa usimamizi wa serikali, inapangwa bei na Serikali, wasambazaji wanachukua kupeleka vituo vya mafuta kuisambaza kwa bei waliyo pangiwa na Serikali (kama MSD inavyo fanya kazi)

Kwa mtazamo wangu;

Serikali ingefanya kazi yake ya msingi ambayo ni kusimamia viwango (ubora wa Petrol inayo ingia Nchini) na kukusanya kodi, Iwaachie wafanya Biashara wafanye kazi yao ya msingi ambayo ni kutafuta Petrol ya bei nafuu huko masokoni na hivyo kuleta Ushindani wa bidhaa hiyo hapa nyumbani

Lakini pia huwa siwaelewi kabisa EWURA kuzuia wafanya biashara wa Petrol wasishindane?

Ningetamani EWURA waweke bei moja ya juu wanayo ita ya soko la dunia mf: bei ya petrol isizidi shs 3000 kwa lita, mengine wawachie wafanya biashara washindane
Tanzania hatuna uhaba wa vituo vya mafuta, vingine huku mjini vipo umbali wa meta 20 (vimetenganishwa na ukuta) sijui wanaogopa nini?

Muhimu: Serikali inaweza kuendelea na utaratibu wake wa kuagiza mafuta yake kwa bei ya soko la dunia, wafanya biashara wanaotaka, watanunua kwao
 
Back
Top Bottom