MeinKempf
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 11,094
- 7,225
Define Density....
Define History....
Wakuu Mimi ni mpenzi wa mitandao mbali mbali ya kijamii (ya ndani na nje ya nchi) ikiwemo baba lao JF, Millard Ayo.com, Nairaland forum- hii iko kama JF kwa kila kitu ni ya wa Nigeria, kuna Issa Michuzi, saleh jembe,bin zubery, eddo kumwembe, Le mburulaz le Mutuz, ikulu blog, etc.
Pia naomba Ku declare interest kuwa Mimi ni mfuasi wake mzuri sana (Millard Ayo .com ) nimekuwa addict fan wake . hivyo nitayo yasema hapa ni kwa kumpenda na.kumshauri mdogo wangu na mtangazaji na mwandishi wangu ninaye mpenda Millard Ayo a.k.a chuganian HB.
Leo naomba nijikite kwa Millard Ayo.
Huyu bwana mdogo kwanza nampongeza sana kwa juhudi za kutumia kipaji chake vizuri katika tasnia ya habari. Nakumbuka kipindi kile miaka ya nyuma kidogo akipita mitaa yetu ya kujiachia Mwenge akienda ITV ...aisee bwana mdogo alikuwa na mapenzi na kazi yake kweli kweli.
Alitangaza vituo mbali mbali Na kipindi tofauti tofauti mpaka alivyofikia hatua ya kujikita katika kazi zake za kuendesha blog yake na TV yake ya mtandaoni (online "Ayo TV").
Aisee mwanzoni blog yake ilikuwa inajaa habari kede kede tena zilizochambuliwa kwa kina na kuandikwa vizuri sana Kiasi kwamba msomaji ukiisoma habari husika basi wewe umemaliza hata utamu wake hata gazeti au RTD habar saa mbili unatupa kule.
Ilifikia hatua mpaka ikasemekana bwana mdogo ndiye mtangazaji kijana na mwenye haiba ya kuvutia makini ya watu kwa kiasi kikubwa hapa bongo na anapiga hela ya kutosha " google addens" na matangazo ya wadhamini wake kama tigo ,GSM, NHC,NMB, etc kwa hilo nami nililiona na Nina mpongeza sana
Hakika blog yake ilitisha sana na kupendwa na Mimi na wewe unayesoma Uzi huu (kwani Nina Hakika lazima ushawahi peruzi habari kwa Millard Ayo. Com. Ni mashuhuda wa namna Dogo alivyokuwa akibamba.
Kifo cha mende kinacho mnyemelea huyu bwana mdogo na blog yake ni kama ifatavyo:
01. Kujaza ma video kibao kwa kila habari yake huku akijua fika kuwa bando la Ku download video hizo ni shida kubwa kwa watu wake wengi. Bando la kuunga unga jombaaa.
Na pia mitandao mingine network zao sio stable (more than 95% ni 3G, H,E...hapa 4G ni wa kubahatisha esp wa dar) hivyo watu wengi kuishia kusoma heading tu na kushindwa kupata kile walichokitarajia kwa kuwa video zinakuwa nzito Ku play on time na pia kuhitaji chaji ya kutosha kwa tendo hilo.
02.Kujikita kupewa habari na maripota uchwara. Zamani ulikuwa una zileta wewe mwenyewe au unatuma vijana wako wenye weredi na kazi, matokeo yake siku hizi unaokota okota tu habari za makanjanja mitandaoni na kutubandikia.
Badilika na tafuta habari nzuri tena za kitaifa na kimataifa Hasa zile zenye tija, na sio kuweka breaking news za hovyo hivyo (hizo ilibidi ziwe kwenye chitchat na sio kwa kwako,
Mfano: Flora mbasha apata mchumba...aagggghhhh., wasafi walivyosherekea happybirtdhday ya chibu, shilole na snura waeleza siri ya misambwanda yao, etc
03. Kujaza habari udaku na ki shigongo shigongo kama habari za kina Walper na WCB utafikili watu wote tunaotembelea blog yako ni team bongo movie na team bongo fleva au team shilawadu.
Kipindi cha magazetini una jitahidi sana na zile habarinza amplifaya.hongera kwa hilo.
Tunapenda utuwekee habari mchanganyiko, za siasa, michezo, kimataifa na sio kujaza habari za watoto wanaoishi maisha feki tu (celebrities wengi wa bongo ni feki feki tu). Zamani ulijitahidi na kila mtu alipotembelea blog yako alifaidi habari za upande wake au azipendazo.
04. Tafuta namna bora ya kuweka matangazo yako (mfank: jifunze JF wanavyoweka matangazo yao,) ikibidi Punguza utitiri wa matangazo kwa kila habari ..matangazo kama mkutano wa nzito....yaani nusu ya blog na habari zako zote umejaza matangazo utafikili Yale machata walioyopaka kwenye gari la miss Tanzania Diana Eddo au ule ukuta wa EATV kwenye kipindi cha Friday night walichokuwa wanapiga chata na sahihi kila mtu Kiasi kwamba hata hujui kilichoandikwa.
05. Punguza vile vihabari unavyo okoteza (Kama habari za kwenye blog ya Le mbebezi ) anavyo okoteza toka kwenye vi-blog vya Nigeria na marekani. Huwa unaandika (Je wajua au Je wafahamu....) Sijui jamaa anayeendesha gari akiwa kafumba macho, mjue kimbau mbau anayetafuna Bonge nyanya la 150kg bila kuishiwa pumzi, wanawake waliovunja rekodi ya kuwa na sura ngumu, ufahamu Nyumba za gharama kubwa duniani, binadamu mwenye kucha ndefu, mtoto mwenye kitambi kuliko wote dunianj, cheki Floyd M.anavyokula bata mpaka dollar zinamshangaa, bata kavaa raizoni, giggy money na msambwanda wa mchina, etc.
Kwa mtizamo wangu hizo ni habari za kitoto sana, weka habari za kitu uzima na sio kufanya kama blog ya watoto wa Sunday school. Angalia brother Michuzi, haweki vituko vituko vya majuu kwani vingi ni uzushi (with much more hyperboles) na kutufanya wasomaji wako kama wote ni watoto.
06. Kuwa unaondoa front page au kwenye interface ya blog yako habari za nyuma, yaani unakuta habari inakaa zaid ya miezi 4 mfano, miss Tanzania afunguka kilichojili miss word, kila siku ipo hapo, saa hizi umeweka mume wa flora afunguka, etc yaani ina kera, kuwa kama wengine Dogo, habari ikipita ina kaa archives huko (tupa kapuni) na sio mtu anafungua mi habari la kitambo kirefu lipo tu utadhani ni current news. Za zamani atazisaka kwenye maktaba.
So make sure you update your news accordingly and with time in order to cutter the needs of your fans. Hapo uta win mdogo wangu.
07. Pia kujaza video nyingine inatulazimu kuwa kama wasanii yaani kutembea na headphone muda wote ili kusikikiliza kilichomo wakat ungeandika walau ningepakua habari yangu kimya kimya na kusepa zangu hata bila watu wa pembeni kujua Nina Fanya Nini na kilonga longa changu (kumbuka ofisini au kazin aunkwenye kada mnasibya watu kama kwenye dala dala) huwezi vaa ma headphone (utaona noma kuvaa headphone) na kusikiliza habar ya majambazi ya kibiti au tamko la Lowasa kunyimwa ukumbi wa mikutano. Ila ingekuwa imeandikwa kwa Maneno ningeperuzi kimya kimyanna kupata nondo zangu. Ajifunze kwa JF mambo mengi tunasoma hata kama tupo kazini au kwenye dala dala , ila JF wangejaza ma video Hakika habari zao nyingi zingekosa wasomaji na wachangiaji pia. Mwandishi yana mvuto bana maana unasema kilichonlengwa tu kuliko kusikiliza video mzima ya DK 20 mpaka ukapate point , bodi kakuona au bado limekata (ref tangazo la joto juu ya bando kisha ).
Kwa leo ni hayo tu mdogo wangu Millard Ayo, nimeamua kukushauri. Yafanyie kazi blog yako itapendwa sana kama zamani ila ukipuuza blog yako inaenda kufa kifo cha mende kama zingine zilivyokufa mfano kina mpekuzi blog, blog ya wananchi ya Le mutuzi, etc