Mtazamo: Mwenge unachangia maambukizi ya ukimwi, ni nini faida yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtazamo: Mwenge unachangia maambukizi ya ukimwi, ni nini faida yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Nov 17, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kutumia gharama kubwa na pesa nyingi za walipa kodi wa nchi hii. Mwenge una madhara makubwa kwa jamii hasa katika suala la maambukizi ya ukimwi. Katika vijiji ambavyo mwenge unapolazwa huwa kuna matukio mengi ya ngono nzembe kutokana na wakimbiza mwenge kuchangamkia wanawake katika vijiji hivyo. Sasa hapa tujiulize, mwenge huu hulala vijiji vingapi tangu unapowashwa mpaka unapozimwa. Nimewahi kukimbiza mwenge katika wilaya ya Manyoni. Hali ilikuwa mbaya sana, kila mtu aliona ufahari kulala na mwanamke katika vijiji ambavyo mwenge ulilala. Naona mwenge umepitwa na wakati. Ni nini faida yake kwa sasa?
   
 2. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hasara na janga
   
 3. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwanza nakushauri usitoe hukumu kabla ya kujiuliza masuali haya yafuatayo
  1. Lengo la Mwenge wa Uhuru kukimbizwa nchi nzima ni nini?
  2.Je, hayo malengo yanafaa(yana manufaa kwa Taifa?) usiangalie manufaa yake kwako. Angalia katika ngazi ya Taifa
  3. Je, hayo malengo bado tunayahitaji kwa muda huu?
  4.UKIWI unasababishwa na nini?Je, Mwenge ni miongoni mwa majiubu yako?
  5. Je, nchi zisizo kimbiza Mwenge, kuna UKIMWI?kama upo sababu ni nini?
  6. Je, Wakimbiza Mwenge unao "watuhumu" ni waathirika wa UKIMWI na ndiyo wanao eneza UKIMWI?
  7.Tukiacha kukimbiza Mwenge leo, UKIMWI utaisha Tanzania?

  Naomba uchambue hayo masuali, then, utaamua kuukimbiza au kutokuukimbiza Mwenge. Kwangu mie ni wa Manufaa saana tu ila hatuutumii unavyotakiwa!
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  upo sawa kabisa kinachonishangaza wanakesha ili iweje
  kwa mtu mwenye akili hawezi kukesha kisa mwenge huku wakitunia fedha nyingi
  kunannchi gani duniani wana ujinga kama huu kama sio Tanganyika pekee??
   
 5. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hivi ww kwa akili yako huu mwenge tangu umeujua umeleta maendeleo gani?
  kama kuzindua miradi hata mkuu wa wialaya husika atazindua sio lazima mwenge
  tunaendekeza umaskini kwa kuabudu dude lisilosema.wauweke makumbusho
   
 6. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wewe unaonekana ni mchambuzi mwenye maslahi na mwenge. Naomba unipe faida za mwenge tangu ulipowashwa kwa mara ya kwanza mpaka leo. Then ndiyo ntatoa mchanganuo wa hoja yako.
   
 7. dwight

  dwight JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Katika mwenge hasa pale unapolala,kunakuwa na mkesha wa muziki,na watu hu2mia nafasi hiyo kufanya mapenzi ktk na hii huchangia maambukizi.
  Kwa faida hata mie siioni zaidi ya kuandika mamilioni ya shilingi ktk bajeti na kuyatafuna!
   
 8. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wewe usiyeona faida ndo utoe hasara kwanza za Mwenge toka Uhuru. Halafu nitakupa shule baadaye. Mie sina maslahi yoyote na Mwenge kibinafsi ila ninayo Kitaifa.
   
 9. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #9
  Nov 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Aaa! Shit, unataka hasara gani tena? Kusambaza na kueneza ukimwi ni moja ya hasara hizo. Unajua kuwa pesa nyingi sana inatumika katika zoezi zima la kukimbiza mwenge? Je, pesa hizo unaweza kulinganisha na majiwe ya msingi ambayo kiongozi wa mbio za mwenge huweka kwenye miradi ya kichovu? Viposho hivyo vinakudanganya ndugu yangu.
   
 10. s

  sara amos New Member

  #10
  Sep 12, 2017
  Joined: Sep 12, 2017
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Daaah nimekukubal kwa hzo facts

  i phone-6
   
 11. magige Dm

  magige Dm JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2017
  Joined: Jul 17, 2017
  Messages: 424
  Likes Received: 758
  Trophy Points: 180
  Kuna mtendaji alikuja kwenye biashara yangu kuniomba mchango wa mwenge nilimtoa mbio.

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 12. magige Dm

  magige Dm JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2017
  Joined: Jul 17, 2017
  Messages: 424
  Likes Received: 758
  Trophy Points: 180
 13. francis bakari

  francis bakari Senior Member

  #13
  Sep 12, 2017
  Joined: Aug 1, 2017
  Messages: 136
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Sijui tutapata lini kiongozi atakae ondoa huu mwenge,binafsi sioni kama kuna faida labda tuwaulize wakurugenzi kama wanaweza kutupatia hizo faida

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 14. Maxmizer

  Maxmizer JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2017
  Joined: May 22, 2017
  Messages: 2,362
  Likes Received: 1,829
  Trophy Points: 280
  dili la wapigaji tu

  /Akifa shekhe kazi ya Mungu/
  /Akifa mlevi sababu ya Pombe/
   
 15. Ki Mun

  Ki Mun JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2017
  Joined: Oct 6, 2014
  Messages: 3,210
  Likes Received: 3,411
  Trophy Points: 280
  Hicho chama kinachopenda mwenge ni wazinzi kupindukia, hawawezi kuelewa kuufukia makumbusho!
   
Loading...