Mtazamo Mpya wa Uwekezaji Kwenye Mali Asili

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,556
1,383
Afrika imejaliwa mali asili nyingi na uwekezaji kwenye hizo mali umefanyika kwa miaka mingi (kwa nchi nyingi, hii ni angalau miaka 50 baada ya uhuru), lakini umasikini wa kukithiri bado ni tishio kubwa. Uwekezaji Congo na Tanzania ni mfano mzuri. Dhahabu, almasi, tanzanite na madini mengine vimevunwa na wawekezaji. Kilichobaki sehemu zinazohusika ni uharibifu wa mazingira na sumu (kama mercury) kwenye mito ya maji.


Mfumo wa uwekezaji uliotumika, na unaondelea kutumika, umependekezwa na wawekezaji wenyewe. Mwekezaji anatoa fedha za kununulia mitambo ya uvunaji na kuajiri wataalamu, na serikali inapata mrahaba (royalty) au share ambao inakuwa ni asilimia fulani ya FAIDA. Tatizo kubwa kwenye mfumo wa aina hii halikuwa udogo wa hiyo asilimia ya mrahaba au share bali ni udanganyifu. Wawekezaji walitaja kiasi kikubwa kwamba ndicho walichowekeza, na kuweka pia gharama kubwa za uendeshaji kiasi kwamba FAIDA aidha inakuwa kidogo sana au haipo kabisa. Matokeo yake mali asili inakwisha na mgao kwa nchi ni kidogo au sifuri.

Ubaya wa aina ya uwekezaji tulioelezea hapo juu ni kwamba unaweza kuwa na mali asili kama chuma au dhahabu ambayo makisio ya dhamani yake ni $10 billion na ikavunwa bila wewe kupata chochote kwa madai kwamba gharama ya kuivuna ilikuwa $10 billion pia, kwa hivyo hakukuwa na faida ya kugawana!

Tubadilike, tuwe na mfumo ambao unatuwezesha KUUZA mali asili zetu. Mwekezaji anayependa kuvuna dhahabu yetu, mkaa wa mawe, chuma, na mali asili yoyote analipa asilimia fulani (eg 50%) ya kila kilogram au tani inayouzwa. Au akipenda basi anunue kila tani ya udongo, mchanga au mawe yenye hiyo mali asili kwa bei tutakayopatana.

Kwa hivyo basi, mazungumzo na mwekezaji yasiwe “what percentage of the profit are you going to give us” bali yawe “how much are you going to pay us per unit weight?”

“Tumenyonywa vya kutosha, tumedharauliwa vya kutosha. Unyonge wetu ndiyo umefanya tunyonywe, tudharauliwe na kupuuzwa. Sasa tunataka kufanya mapinduzi; mapinduzi yatakayotuondolea kunyonywa, kudharauliwa na kupuuzwa” – Julius Nyerere (an approximate quotation).
 
Hoja Nzuri,ila Jambo hili kwa Serikali hii lawezekana?

Isipowezekana kwa "serikali hii" ya Magufuli basi itakuwa shida kwa wengine. Magufuli ana uthubutu wa kufanya mapya. Hili jipu sugu la uwekezaji unaotunyonya kishenzi kama halitumbuliwi na Magufuli litatumbuliwa na nani?

Tatizo la elimu ya kukariri limefanya viongozi tangu enzi ya uhuru (ukiondoa Mwalimu Nyerere) kutojiuliza imekuwaje ivunwe kwetu dhahabu ya mabilioni mengi, almasi ya mabilioni mengi, magogo ya mabilioni mengi, na sasa gesi ya mabilioni mengi kisha tuwe masikini wa kutisha?
 
nakubaliana na wewe mkuu
Naomba umpe hii hoja mtu mkali bungeni aikomalie. Mtu kama Halima Mdee au Lema.

Mwanzoni tulikuwa na dhahabu na wao walikuwa na fedha. Sasa wana ile dhahabu yetu, na fedha zao bado wamezishikilia maana tulikubaliana tutagawana faida baada ya wao kurudisha fedha zao. Wamerudisha fedha zao na kuzalisha nyingine nyingi za "kazi za kifundi", na sisi tumebaki tunatafuta wawekezaji wengine tuwape mkaa wa mawe na machimbo ya chuma. Wakimaliza watakuwa wamerudisha fedha zao, na kuchukua chuma chetu, na sisi tutabaki na nini? Hakutakuwa na faida ya kugawana (they cook the books).
 
Back
Top Bottom