...ni ka swali tu, viongozi wote hasa wateuliwa na wabunge hawavai kabisa barakoa. Iwe kwenye mazishi, mikusanyiko mbalimbali nk hutawaona wamevaa barakoa.

Au watakuwa washapigwa chanjo kisirisiri wanatupoteza maboya wenzao?

...Leaders lead by examples. Wananchi wengi wenye low reasoning capacity wanasubiri leaders wavae magwanda ndo nao watimbe! Please leaders tunaangamizana!

NB: Mie navaa barakoa, wewe je?

Trumpeta kaacha historia duniani!
 
Mbona nasikia tetesi kuwa hii second waive eti yenyewe haisikii limao wala tangawizi.
Watu Wa Kule kwetu Tarime wanamsemo wao,BHUNU MBHUNDI.
Haya malimao sijui tangawizi tununue tu kuchangia uchumi wa wachuuzi, but in real kale kajamaa kakiingia kanakula mpka tangawizi na kanaomba hata ndimu!
 
Haya malimao sijui tangawizi tununue tu kuchangia uchumi wa wachuuzi, but in real kale kajamaa kakiingia kanakula mpka tangawizi na kanaomba hata ndimu!
Ni wakati mashirika ya ujasusi duniani kuwapeleleza walio plant huu ugonjwa maana sio wa mungu, thus why 2nd wave wameutengeneza ili utushambulie hasa waafrika ndio maana ukapandikizwa south afrika na brazil
 
Haya malimao sijui tangawizi tununue tu kuchangia uchumi wa wachuuzi, but in real kale kajamaa kakiingia kanakula mpka tangawizi na kanaomba hata ndimu!
Ndio hivyo,
Ile corona iliyopita ilikuwa nafuu kidogo,hii ya sasa inaitwa pneumonia au changamoto ya upumuaji in hatari.
 
Ni wakati mashirika ya ujasusi duniani kuwapeleleza walio plant huu ugonjwa maana sio wa mungu, thus why 2nd wave wameutengeneza ili utushambulie hasa waafrika ndio maana ukapandikizwa south afrika na brazil
Labda utume wasiojulikana wa huku kwetu.

Hao Wa kimataifa ni sawa na kesi ya kondoo umpelekee chui.

Bill gate alitabiri kuwa Africa maiti zitaokotwa barabarani hii inakuja soon,Hosp zetu vifaa vya kupumulia vingombaniwa havitoshi.

Anguko la mwenyekiti wenu alivyochukulia mzaha swala la korona laja kwa kasi.

Kinachofuata watu watagombania chanjo,ni swala la muda tu.
 
Usipoogopa Malaria haina maana hutaipata hasa kama hujikingi na mbu, kutoogopa ukimwi na kutojikinga unaweza kuupata kirahisi sana, sasa kwa nini hofu iwe shida badala ya sababu ya kujikinga na magonjwa ya maambukizo?

Walipigana na gonjwa hili mwanzoni kwa kusisitiza kujihadhari na kunawa mikono hata kutojumuika kwenye mikusanyiko isiyo na lazima, kuvaa barakoa na kupiga nyumgu, ndiyo maana walishinda ya raundi ya kwanza.

Siyo Mungu pekee bali ni pamoja na juhudi za watu pia ndiyo maana tulishinda raundi ya kwanza ya hili gonjwa.
 
BARAKOA INAVYOONEKANA HAISAIDII KUZUIA MAAMBUKIZI NA NI HATARI KWA AFYA. SOMA HAPA CHINI

Barakoa kiufundi au kisayansi ni hatari sana kwa afya yako na hasa unapoivaa kwa muda mrefu. Inaweza pelekea mtu kupata magonjwa kama kansa ya mapafu kwa mujibu wa tafiti za karibuni. Lakini kikubwa zaidi ni kwamba haisaidii kupunguza maambukizi ya huu ugonjwa wa korona kwa mujibu wa tafiti nyingine ambayo ilitumia emperical data iliyofanyika huko Denmark. Na ndio maana Sweden hivi karibuni wamepiga marufuku uvaaji wa barakoa kwa kuwa hakuna msingi wa kisayansi unaoonyesha unasaidia kupunguza maambukizi. Ni tafiti moja iliyodai barakoa inaonekana inasaidia na hii ilitumia 'Computer Model' ambayo haikuwa na empirical data kama tafiti ya Sweden. Kuhimiza watu barakoa umekuwa ni wa kisiasa zaidi huko Ulaya na Marekani. Kuna madaktari wengi tu wataalamu washazungumzia 'ineffectiveness' ya barakoa kwenye kuzuia maambukizi. Na Dr. Antony Fauci alishasema kuvaa barakoa ni symbolic tu na hakuna scientific data ya aina yeyote. Kimsingi barakoa inavaliwa kisiasa mbele za kamera na hao wenye kulitaka tatizo la COVID-19 lionekane kubwa ili ajenda ya chanjo iende mbele na makampuni makubwa ya dawa ya Ulaya, Marekani, China, na Russia yapate faida kubwa. Lakini agenda ya chanjo ni kubwa zaidi hii ni mada inayoihitaji uzi wake tofauti. Asanteni na Ushahidi wa tafiti kuhusu athari ya barakoa kiafya na kutosaidia kwake kupunguza maambukizi ni huu hapa chini:

1. Effectiveness of Adding a Mask Recommendation to Other Public Health Measures to Prevent SARS-CoV-2 Infection in Danish Mask Wearers - ACP Journals
- Hii paper ndio pekee ambayo imetumia empirical data na kuhitimisha kuwa barakoa hazisaidia kwenye kuzuia maambukizi.

2.A Week After Saying ‘Wear Two Masks’, Fauci Says It ‘Won’t Make A Difference’ - A Week After Saying ‘Wear Two Masks’, Fauci Says It ‘Won’t Make A Difference’
- Hii ni article inayoonyesha duble standanrd kwenye sula zima la mask na kuvaa mask mbili. Antony Fauci mwanzo alisema kuvaa barakoa mbili hakuna tofauti yeyote lakini akaja na kauli nyingine tofauti akihimiza watu wavae barakoa mbili bila ushahidi wowote wa kisayansi na ndio maana nasema suala la barakoa Ulaya na Marekani ni la kisiasa na limebeba ajenda nyingine (watu waharakishe kukimbilia chanjo).

3. STUDY: Long term mask use breeds microbes that infiltrate the lungs and contribute to advanced stage lung cancer - STUDY: Long term mask use breeds microbes that infiltrate the lungs and contribute to advanced stage lung cancer
- Hii ni study iliyochapishwa mwezi ikionyesha hatari ya uvaaji wa barakoa kwenye kusababisa kansa.

4. The Empirical Case For A Mask Mandate Lacks Scientific Grounding - Zerohedge

5. Sweden Bans Masks: ‘No Scientific Evidence’ They Prevent COVID. - Sweden Bans Masks: ‘No Scientific Evidence’ They Prevent COVID | Principia Scientific Intl.
 
Wakuu ,habarini poleni na majukumu poleni pia na hili janga la corona ,kiufupi mimi niseme corona sio tishio kubwa ila limekuwa overrated,

Ebu kumbuka lile janga la dengue ebu assume dengue ingewapata wazungu au wachina wangekuwa katika hali gani?

Katika kufikiri tu mi nadhani hao mabwana wana weak immune system na pia nadhani dengue is more serious than corona.

Kumbuka hata kipindi cha kujenga railway uko marekani walitumia watu weusi maana ngozi nyeupe they are very weak hata malaralia ambayo asilimia kubwa huku kwetu ni kama homa ya kawaida wenzetu wakipata inakuwa tragedy

Yani corona ni ugonjwa ambao unapata nafuu kwa kujitenga mwenyewe ndani ya siku kadhaa !!! Na pia ni ugonjwa ambao unawakumba wazee sana sana 50+

Wanasema watoto na vijana asilimia kubwa wanaweza hata wasioneshe dalili japokuwa ugonjwa huo wanao mimi nadhani ni kwakua tu maambukizi yake niyakasi na haraka ndo maana umepewa promo ila sio janga kubwa kiivyo cha msingi ni kuzingatia kunawa na sabuni mara kwa mara ,kuvaa mask na gloves ,kuepuka misongamano hutaisha fastaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yamezingatiwa?
 
Acha tulipie uzembe uliosabishwa na serikali toka mwanzo ilishindwa kuonyesha reaction yoyote unashindwa funga mipaka kisa watalii nani bora kati ya mwananchi na mtalii pesa ina thamani kuliko uhai wetu

Nb: Serikali imehusika kwa uzembe ktk hili.

Huu ni uzembe wa kufikiri huko walikofunga mipaka mbona idadi ya vifo kila siku inaongezeka nao wafanya uzembe upi?
 
Mods, mabibi na mabwana.

Fursa na riziki si lazima kupatikana leo. Bali mazingira ya fursa hayapaswi kungoja kesho.

Huu ni ushauri wa bure kwenu JF, na hasa MODs.

Corona inauwa. Ugonjwa huu upo hapa nchini kama ilivyo kuwa kwingine. Ugonjwa huu unasambaa zaidi kwenye mikusanyiko ya watu isiyozingatia tahadhari zinazo uhusu.

Kuhamasisha watu kujikinga ili waweze kuendelea kuwa hai na bila ya kujali malipo ya hapa duniani ni jambo la thawabu kubwa mno.

Kwa hakika jitihada za kupigania uhai wa watu hazijawahi kupotea bure.

Ikumbukwe kuwa sote tungalifurahi mno kutokumpoteza mpendwa wetu yeyote kutokana na janga hili ambalo kwa hakika linaweza kuepukika.

Kwamba nyie mko na udhibiti wa forum hii, kuridhia uhimizwaji wa watu kuchukua hatua za kujilinda hakuwezi kuchukuliwa na mtu yeyote kuwa ni kosa au usaliti.

Kwani nani asiyefarijika kuona mja mwingine wa mola akiwa hai na salama?

Kwa kuchukua hatua za kujilinda tu tungeepuka misiba hii inayoendelea kutusononesha sana leo.

Ama kwa hakika kuukimbia ukweli hakusaidii. Kama jamii tunayo nafasi ya kuelezana ukweli na kwa pamoja tukasalia salama.

Tunavyoendelea kumwomboleza mpendwa wetu rais Magufuli (rip) kwa namna ambayo kila mmoja wetu anaiona, tujue kuwa ni suala la muda tu.

Kwamba kwa kupiga kelele tu humu JF, kwa pamoja tunaweza kuokoa maisha ya watu wengi, mbona hili ni wazi mno?

Ni kwa mukthadha huu JF kuwa japo nominee wa tuzo ya Nobeli hakuwezi kubakia kuwa kama ndoto isiyowezekana.

Zitendeeni haki nyuzi zinazoasa na kuhimiza watu kuwa salama ikiwamo katika kipindi hiki cha maombolezo.

Ninawasilisha.
 
Hii Tanzania hii, sisi ni sayari nyingine kabisa, wiki iliyopita nilienda msibani huko Chanika tena watoto wa marehemu walisema kabisa mama yao kafa na CORONA, cha kushangaza mvaaji BARAKOA mie watu walikuwa wanishangaa utadhani mimi ndio COVID yenyewe, wengine wanakuja kukupa pole wanataka na kukumbatia kabisa, shee!
 
Inasikitisha sana.

Kwani hata kuna haja ya kujidanganya?
Ilikuwa ni kwa kuvaa barakoa tu, mheshimiwa Magufuli angekuwa hai leo.

Hii habari ya mapenzi ya Mungu inatubwetesha sana waswahili.
 
Mods, mabibi na mabwana.

Fursa na riziki si lazima kupatikana leo. Bali mazingira ya fursa hayapaswi kungoja kesho.

Huu ni ushauri wa bure kwenu JF, na hasa MODs.

Corona inauwa. Ugonjwa huu upo hapa nchini kama ilivyo kuwa kwingine. Ugonjwa huu unasambaa zaidi kwenye mikusanyiko ya watu isiyozingatia tahadhari zinazo uhusu.

Kuhamasisha watu kujikinga ili waweze kuendelea kuwa hai na bila ya kujali malipo ya hapa duniani ni jambo la thawabu kubwa mno.

Kwa hakika jitihada za kupigania uhai wa watu hazijawahi kupotea bure.

Ikumbukwe kuwa sote tungalifurahi mno kutokumpoteza mpendwa wetu yeyote kutokana na janga hili ambalo kwa hakika linaweza kuepukika.

Kwamba nyie mko na udhibiti wa forum hii, kuridhia uhimizwaji wa watu kuchukua hatua za kujilinda hakuwezi kuchukuliwa na mtu yeyote kuwa ni kosa au usaliti.

Kwani nani asiyefarijika kuona mja mwingine wa mola akiwa hai na salama?

Kwa kuchukua hatua za kujilinda tu tungeepuka misiba hii inayoendelea kutusononesha sana leo.

Ama kwa hakika kuukimbia ukweli hakusaidii. Kama jamii tunayo nafasi ya kuelezana ukweli na kwa pamoja tukasalia salama.

Tunavyoendelea kumwomboleza mpendwa wetu rais Magufuli (rip) kwa namna ambayo kila mmoja wetu anaiona, tujue kuwa ni suala la muda tu.

Kwamba kwa kupiga kelele tu humu JF, kwa pamoja tunaweza kuokoa maisha ya watu wengi, mbona hili ni wazi mno?

Ni kwa mukthadha huu JF kuwa japo nominee wa tuzo ya Nobeli hakuwezi kubakia kuwa kama ndoto isiyowezekana.

Zitendeeni haki nyuzi zinazoasa na kuhimiza watu kuwa salama ikiwamo katika kipindi hiki cha maombolezo.

Ninawasilisha.
Siku covid inakuua wewe brazaj ndio nitaamini kweli covid ni hatari la sivyo nitaishi kadiri ya Imani ya hayati John Pombe Magufuli.
 
Marehemu Rais Magufuli amefanya mengi makubwa kwa kipindi kifupi mno.Amefanya pia mabaya ambayo kwa kanuni za kibinadamu hatuwezi kuyajadili sana kwa kuwa hayupo kuweza kujitetea.

Pamoja na kumpenda sana hii ratiba ya kuaga inawaweka watu wengi katika uwezekanao wa kupata corona.
Ili twende vizuri serikali itusaidie kuweka wazi haya,
  1. Kuwa HAKUNA corona Tanzania
  2. Corona ipo Tanzania ila tumeamua kuchukua mkondo wa kutafuta kinga kwa wengi (Herd Immunity)
Mojawapo kati ya hayo yatasaidia sana katika watu kufikia uamuzi binafsi la sivyo ni kama hatujui tuendako.
 
- Kama tulikosea tukazama katika dimbwi la corona si vibaya kujitokeza Tena bado hatujachelewa kudhibiti Mimi naamini tungeanzishiwa tena ule utaratibu wa kunawa mikono kila sehemu mpaka majumbani kuwe na satinizer naamini mdudu corona asingefika hata kwa nguvu za Giza kwa sababu mikono mi agent mkuu wa kusambaza.

- Wivu au chuki baina yetu au na majirani havitasaidia sote tuungane tujaribu kuzingatia Kama ni kweli tusiishi ki primitive akati tumepewa vichwa ila tusiwe watumwa wa watu kwa sababu hakuna binadamu asiye na uwezo sote tuko matawi ya juu katika classification msifikiri wazungu Wana jua kila kitu watatumia nafasi hio kutusukuma Kama punda.

- Africa tutabaki kuwa Afrika hata tufanye nini asili yetu sisi ni kujiamini tusivunjike mioyo huu upepo unapovuma si mnaona Magufuli alieleweka kwa waerevu toka long time. Magufuli ni kioo Cha jamii; jifunze kupitia yeye. Sawa ana mabaya yake ila kila alilolishika lilikamilika watoto watakaozaliwa wataona manufaa yake.

- Tuchukue tahadhari sana; hatuwezi kuelewa maana ya Vita ya kiuchumi jua linazidi kuchomoza Tanzania itashinda tu japo misukosuko lazima itakuwepo.
 
Wote tunafahamu kile dunia yetu inapitia kuhusiana na janga la Korona au Covid – 19. Naamini tunakubaliana kuwa changamoto ya korona ni kubwa na imeleta na itaendelea kuleta madhara makubwa sana sana kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Kwa sababu ya upya wa janga hili, kila serikali au nchi nyingi duniani zilijaribu kuchukua njia tofauti tofuati kulishughulikia. Wengine walianza na dawa mbalimbali na barakoa ambazo ziliruhusiwa kutumika, kisha baadaye zikatekelezwa mbinu kama za kufungia watu (Lockdown) na sasa mbinu moja inayokubalika na ulimwengu ni Chanjo.

Sasa kuanzia hapa kwenye chanjo ndipo ushauri wangu wa kwanza ulipo.

  • Suala la ugonjwa wa korona ni jambo zito ambalo wangi hawafahamu, lina mambo mengi yaliyofichika ambapo kuanza kuyaeleza inahitaji mada tofauti maana ni kitu kilipangwa kikapangika na kinafata ramani kulingana na ilivyopangwa ila hatima yake ni kutufikisha kwenye chanjo ambayo pia ina malengo mengine ya kutimiza.
  • Hakuna serikali itakayoweza kuepuka suala la chanjo as long as inahitaji kuendelea kuingiliana na watu wengine wa duniani.
  • Yeyote atakayepinga hili atajiweka kwenye matatizo ya kupingana na ‘wenye dunia’ yao.
Ushauri

  • Serikali ijitahidi kufanya uchunguzi wa chanjo ipi ije itumike Tanzania na hili lisemwe wazi ikibidi kwa kurudia rudia ( Wenye dunia yao watafurahi kusikia upo utayari wa jambo hili)
  • Katika utayari huu serikali (kama haina interest na mambo ya chanjo kama ilivyokuwa mwanzoni) inatakiwa kutumia ‘delay technique’ ili kuendelea kuusoma huu mchezo. Hii itapunguza comfontations ambazo sio za lazima na wenye dunia yao. (Mzee Kikwete anaweza kutoa ushauri mzuri hapa).
  • Kama kipo kitu hawakitaki ni bora kuwasiliana ndani kwa ndani bila kuweka msimamo mzito kuhusu jambo hilo.
Kwa kifupi approach ya kutumia hap ani ya kuuma na kupuliza wakati tukifanya maandalizi ya kuruhusu chanjo kwa maana HATUTAWEZA KUIKWEPA japo hatuipendi na kweli kuna madhara kama tunavyosikia habari zake.
 
Back
Top Bottom