Mtazamo: Kuongezeka kwa wimbi la walalamikaji wa mahusiano, hasa wanaume kuumizwa na mabinti

Kuna jamaa aliwahi kuandika uzi humu ndani akihoji wanaume wa Sikh hizi tuna nini? Mfano mwanaume kufanya sherehe ya birthday
Tunapoteza ule ukakamavu/ungangari/uvumilivu sijui tunaelekea wapi
Kama unashindwa kumcontrol mwanamke wako jua fika hakuna utakachomudu kukiendesha
ajabu sana hii

halafu wao wanajiona wako sahihi nani wakileo
upuuzi
 
Kuna jamaa aliwahi kuandika uzi humu ndani akihoji wanaume wa Sikh hizi tuna nini? Mfano mwanaume kufanya sherehe ya birthday
Tunapoteza ule ukakamavu/ungangari/uvumilivu sijui tunaelekea wapi
Kama unashindwa kumcontrol mwanamke wako jua fika hakuna utakachomudu kukiendesha
Tumetofautiana uwezo , unachokiweza wewe mwenzio kwake ni shida. Kukumbushana ni muhimu.
Na kumbuka tabia za wanawake zinabadilika kama kinyonga.
 
Tumetofautiana uwezo , unachokiweza wewe mwenzio kwake ni shida. Kukumbushana ni muhimu.
Na kumbuka tabia za wanawake zinabadilika kama kinyonga.
Mtoa mada kaelezea vizuri sana hapo juu kuwa huyo mwanamke hukuzaliwa naye that means ishi naye kwa akili

Kuna mwandishi aliwahi kuandika kuwa ukimpenda mwanamke mtongoze in a way akupende na asijue kuwa unampenda simply unaweza kusema MTENGENEZE MWANAMKE WAKO AKUPENDE NA SIYO WEW KUMPENDA hapo uta enjoy mahusiano
Mawazo tu
 
Suala hili kwa sasa limekua kama ndio lina trend hapa Jukwaani. Haipiti siku hujasikia hujaona thread tatu au nne Vijana(hasa wa kiume ) wakitoa lawama na kulalamika ni jinsi gani wanaumizwa na mabinti katika mahusiano.

Nimekaa nikjiuliza ni kwanini mabinti wengi sasa hubadili gia angani na kuwaacha solemba wapenzi wao waliotoka nao mbali muda mrefu, wengine tangu O/A level ila binti akifika chuo anambwaga Mpenzi wake huyo. Wengine wanakutana chuoni , wanadumu miaka yao yote ya masomo katika mahusiano ila wanapokaribia kuhitimu mabinti hao huwaacha solemba wanaume hao wakihaha. Wengine wanafanikiwa kumaliza chuo pamoja, ila wanapofika mtaani binti bila sababu yote ya msingi anabwagana na mpenzi wake.

Tumefikaje hapa ndugu zangu na vijana hasa wa kiume ambao ndio wahanga wakubwa wafanyaje ili wasiendelee tendwa na kuwafanya wachukie mapenzi??

NINAVYOLITAZAMA SUALA HILI:

· NIANZE NA MABINTI …. KWANINI NI WASALITI.

1. TAMAA:

Mabinti wengi miaka hii wamegubikwa na tamaa. Kutamani kuishi kisasa na kifahari kunawafanya washindwe kudumu na wapenzi wao wenye kipato kidogo. Mabinti wengi mmekua na tama ya mavazi, simu za bei ghali, kuhudhuria matamasha ya gharama, kuendekeza sherehe ambazo hazina namna i.e birthday parties ; ambao huwalazimisha wapenzi wenu waje na zawadi za bei ghali. Mpenzi wako anaposhindwa yatimiza hayo unambwaga ukifikiri kwamba utaokota dhahabu.

2. KUKOSA UVUMILIVU

Mabinti wengi miaka hii wanakosa uvumilivu, wengi wamekua wakitamani vitu vya harakaharaka toka kwa wapenzi wao. Wengi wao wametoka familia za kawaida kabisa na ni mashahidi jinsi gani wazazi wao walivuliana katika taabu , shida na karaha mpaka wao wakafika hapo walipo. Kwanini wao leo washindwe kuwa na subira. Mabinti jifunzeni vumilia hali duni za wapenzi wenu.

3. KUWA NA MAHUSANO NA VIBABA/VIBABU ;

Hii pia ni changamoto kubwa ya ahusiano ya vijana kutodumu na wapenzi wao. Mabinti wengi sasa huona ni ufahari kujinadi wanatoka na wame za watu; eti kwamba si wasumbufu na huwatatulia shida zao haraka na hawawagandi. Hili lina hasara kubwa kwao kwani licha ya kumuumiza mpenzi wake aliyetoka naye mbali, pia huenda akaishia zalishwa na kulea mtoto peke yake: na fikiri wote hapa ni mashahidi wa ‘single mothers’ wanavyoongezeka mtaani. Acheni kutoka na vibaba na vibabu kwa tama ya fedha.

4. KULETA USOMI WAKO KWENYE MAPENZI

Mathalani mpenzi wako ameishia elimu ngazi ya cheti, na katika njia yako ya masomo amekusaidia sana kufikia hiyo degree yako. Unapohitimu unamuona mpezi wako huyo hafai tena licha ya kwamba amekufadhili sana. Unaanza kumletea dharau na jeuri kana kwamba hiyo degree ndio itakupatia watoto au utafunga nayo ndoa. Mwisho wa siku unamuachia maumivu makali kijana huyu aliyeyatoa maisha yake kwako. Mbaya zaidi laana hii inakutafuna na wewe , unagonga mpaka miaka 35 hakuna mwanaume amepropose kwako. HAPO UNAVUNA MADHAMBI YAKO.

· VIJANA WA KIUME MFAYE NINI…

ISHINI NA WANAWAKE KWA AKILI

Hukuzaliwa nae na hivyo usijikabidhishe mwili na roho kwake. Utakuja vuna maumivu. Baki na hamsini zako mwachie hamsini kwake. Hutayakana mapenzi akikutenda.

1. USIMUHUDUMIE RAFIKI WA KIKE KAMA MWANAO

Kuna vijana wako tayari hata leta shida katika familia kwa kutumia pato la familia kumhudumia mtu ambaye wala huna A B C nae na wala kwao hukujui. Utajifilisi wewe na familia yako pale binti huyo uliyemuokata atakapokuacha solemba.

2. USIMSOMESHE BINTI/MWANAMKE….. SOMESHA MKEO HALALI.

Mtakuja kusaga meno na kutaka kujinyonga bure, usimsomeshe msichana ambae huna uhakika na future nae. Mtaumia.

3. KUWA MKALI KWA MAMBO YA KIJINGA: DON’T BE SUBMISSIVE

Kuna baadhi ya vijana wakisha lambwa genitals basi uanaume wote unapotea, anakua mtu wa kupelekeshwa na kuburuzwa hovyohovyo. Binti anakua na sauti juu ya kila kitu. Huo ni uboya wa hali ya juu. Kuwa mkali na ikiwezekana piga. Usiendekeze ujinga. Mwanamke hawezi kubali olewa na boya, atakuacha ukishangaa mataa na kwenda kwa wanaume walio FIRM ON ISSUES.

4. FAHAMU KWAO, UKOO WAO NA TABIA ZAO

Kuna koo zina lana tu ya kutokuolewa nakutokua na shida na ndoa. Sasa wewe ukiingia kichwa kichwa bila kutafiti,.. mataendelea kulia sana hapa.

HITIMISHO.

Ahsante kwa wewe ulie tumia muda wako kusoma makala hii. Pamoja tunaweza ishi katika mapenzi bila kuumizana tukishirikisha akili na siyo hisia. Kila mmoja kwa wakati wake atumie muda wake kumuelewa vyema mpenzi aliye naye ili kuepusha maumivu pale mnaposhindwa fikia malengo huku muda mwingi mkiwa mmepoteza.

Akina DADA , inaanza na ninyi , mnaweza kufuta maumivu kwa wapenzi wenu.

HAPPY NEW YEAR.
wanaume kutembea na mabinti hui ni ubakaji kabsa.
wanaume kutembea na mabinti kuna utoto Kati ya wawili hao.
binti. .....binti.....bintii.na mwanamme ahahah ubakaji kweli kweli
 
Mtoa mada kaelezea vizuri sana hapo juu kuwa huyo mwanamke hukuzaliwa naye that means ishi naye kwa akili

Kuna mwandishi aliwahi kuandika kuwa ukimpenda mwanamke mtongoze in a way akupende na asijue kuwa unampenda simply unaweza kusema MTENGENEZE MWANAMKE WAKO AKUPENDE NA SIYO WEW KUMPENDA hapo uta enjoy mahusiano
Mawazo tu
Uko sahihi.... ni vizuri kabla ya kuanza kuingia magharama ya ajabu katika mahusiano, kila nafsi ijiulize,.. Je, am I compatible with him/her. ??
 
wanaume kutembea na mabinti hui ni ubakaji kabsa.
wanaume kutembea na mabinti kuna utoto Kati ya wawili hao.
binti. .....binti.....bintii.na mwanamme ahahah ubakaji kweli kweli
he he...... penye kila binti weka 'wadada'.
 
Uko sahihi.... ni vizuri kabla ya kuanza kuingia magharama ya ajabu katika mahusiano, kila nafsi ijiulize,.. Je, am I compatible with him/her. ??
Yeah kweli kabisa.......
Chukua mwanamke Wa class yako atleast uwe umemzidi vitu vyote
Anaweza pia kuwa amekuzidi ila unapaswa kuwa na kitu cha ziada hasa kichwani (smart upstairs)
 
Kila mmoja anaumizwa, sio mwanaume wala mwanamke ila wanawake wanajua kumeza maumivu ndo maana huoni malalamiko yao humu ila kila mtu akifunguka hapa hapatatosha, la mno ni kila mmoja abadilike tu na kujali hisia za mwenzake
 
hahhaahaa........... hao wanaolialia ndio tuna washtua na kuwapa ufahamu. atakae lialia kijanga mwaka huu hatuna huruma nae.
Nime6 kulaiki Thread yako mkuu kwa ingizo#3.
Umepest kaubaguzi ka umri, ni mbaya. Hisia za mtu hunasa popote bila kujali umri wa mzee kwa kijana ama vise versa.
Kwa mahusiano ya kimchepuko, kwetu cc aged tangazo hilo lina malengo ya kutupeperushia ndege.
Ingekuwa unashauri mahusiano ya ndoa ningekuunga mkono kwamba wasichana waolewe na wa makamo yao.
Lakini hili la kuchepuka, ninakukataza usichagulie mtu umri wa kujivinjari nae, atachagua umri atakapotaka kuolewa.
Halafu kimbabu kutoka na bint umri wa mjukuu wake huwa ni tiba ya kuongeza siku na kuondoa stress.
Pia ni matumizi halali ya pesa zake alizosotea sana miaka nendarudi kwa maisha kiduchu yaliyobaki. Mwache ale ahonge, achezee jasho lake.
Utashauri utachoka, vjana wajinga sana, hasa akinyonywa dushelele kwa hadaa ya kula koni! Wanahonga hadi ada!
Halafu hili la eti kusomesha mchumba!
Unamsomesha ulimzaa wewe? Jukumu la kusomesha ni letu cc wazazi, nyie vijana kazi yenu ni moja tu, kula kilichoiva, basi hauna jukumu jingine katika eneo hilo.
Kijana wa kiume utapotezaje future mapema hadi unafikia hatua ya kutamka laana zako kuwa eti "bila yeye siwezi kuishi"!
Hivi una akili kweli wewe! Kufa tuzike na historia yako ikomee hapo *****!
 
data ukiona mwanamke kabadilika jua chanzo n mwanaume sisi wanawake ni wavumilivu sana nyie ndio mnasababisha yote
 
Ahsante mkuu,, wamekuelewa vizurii.......
 
data ukiona mwanamke kabadilika jua chanzo n mwanaume sisi wanawake ni wavumilivu sana nyie ndio mnasababisha yote
Hapana aisee..... sidhani. Na si kila siku ndivyo.
 
lazima utetee upande wako lkn ukweli ndio huo sisi tukipenda tunapenda kweli unaamua kutulia kabisa
Huenda uko sahihi sana kwa umri wako, kwani nafikiri umefikia maamuzi umeamua. Wengi wanaoteswa hapa ni ule umri wa kuanza juana , ambao huitaji uvumilivu mkubwa na kujitahidi mfahamu vizuri rafiki yako. Hapa ndio wasichana wengi hufeli kwani huwa hawaelewi wanataka nini.. wanashindwa tambua nani sahihi nani siyo,,, na hii ni kutokana na kuwapima wanaume kwenya mizani.

kuja kushtuka umri umeshamtupa na kapoteza ma husband material kibao.

Wakiwa na akili ya kutulia, hakika Mungu atawasaidia.
 
Waiii...

Wanaume hawaridhikagi

Unaeza vumilia each and everything

Lkn mwisho wa siku utajuta kuzaliw

Mm hata ctak kukumbuka mambo yaliyonipata..

Maana naeza Lia jf nzima ikalowa machoz..
 
Waiii...

Wanaume hawaridhikagi

Unaeza vumilia each and everything

Lkn mwisho wa siku utajuta kuzaliw
Kumbuka wanaume tumeumbwa hivyo....
Ukweli ni kwamba hata kama mwanaume ni kicheche vipi, ila kama wewe umejiweka kuwa wa thamani kwake atarudi kwako tu,.

Ukianza shindana nae na wewe uanze tangatanga hovyo, utapoteza vyote.

Binti aliyejitunza na kujiheshimu, kuolewa ni lazima.
 
Back
Top Bottom