Mtazamo kuhusu kupunguza tatizo la ajira kwa vijana

Cobra70

Senior Member
Jan 2, 2020
167
363
Kwanza, napenda kumpongeza mheshimiwa raisi kwa kutekeleza kwa vitendo miradi ya umeme na miundombinu mana vitu hivi ni muhimu ili kufikia nchi ya viwanda.

Ushauri
Ningependa kumshauri mheshimiwa raisi awamu ijayo ajikite katika sekta ya kilimo yaani kilimo cha kibiashara mana asilimia kubwa ya watanzania wanategemea kilimo.

Atafanikiwaje kwa hili?
Kwanza: Atumie wakurugenzi pamoja na timu ya wataalam wa kilimo ili kutambua ukubwa wa ardhi ambayo ni potential kwa kilimo lakini haitumiki ipasavyo na aina gani ya mazao yanayostawi sehemu husika.

Pili: Ajikite sasa kwenye miundombinu ya maji kwa kusambaza maji kila Kijiji na kutengeneza mitandao ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji nchi nzima na kuacha kilimo kinachotegemea mvua za misimu. Hili litafanikiwa kama atatumia vyanzo vya maji vya uhakika ambavyo havikauki.

Tatu: Itengwe budget kubwa
kuliko zote kwenye kilimo kwa kusambaza trekta nyingi kila halmashauri nikimaanisha trekta kwa ajili ya kulimia, kupandia na kuvunia pamoja na pembejeo za kilimo na mbolea.

Nne: Yajengwe magodown mengi kwa ajili ya kuhifadhia mazao kwa usalama na pia viwanda vidogovidogo kwa ajili ya kuchakata na kusindika mazao ili kukuza thamani ya mazao hayo. Jambo hilo lifanyike kila kata katika wilaya.

Tano: Wachukue vijana waliomaliza vyuo vya kilimo waliosoma courses tofauti za kilimo waliopita mafunzo ya JKT waajiriwe kila kata, Majukumu yao;

Moja: Wakisaidiana na viongozi wa kata kubaini na kuwapa mafunzo ya uzalendo na ukakamavu vijana ambao wapo kwenye kata husika ambao hawana ajira rasmi na ambao wamemaliza vyuo lakini hawajabahatika kuajiriwa hii iwe amri ili kuacha kulea uvivu kwa vijana.

Pili; Kufundisha kilimo cha kisasa yaani kwa kufanya kazi kwa vitendo kwa kuingia shambani na kuishi nao hukohuko kma kambi.

Mwisho: Kwa maeneo yenye ardhi kubwa yenye rutuba wachukue vijana waliomaliza vyuo vya kilimo wapite mafunzo ya JKT pamoja na vijana waliomaliza mafunzo ya JKT ambao wapo tayari kulitumikia taifa waende huko wakazalishe na kuondoa dhana ya kuajiriwa maofisini.

Hivi vyote na maeneo yote ya uzalishaji yawe monitored na SUMA JKT

Ahsante.
 
Mtuache tujenge maharaja,mabarabara,tununue mandege sasa ajira inajengwa wapi. Inauma ila.Mungu ni mwema
 
Nakuunga mkono brother!

Wacha nami niongezee kidogo kama mchango wangu kwa mada yako;

WAZO: Hivi serikali inashindwaje kuweka bajeti ya Tsh.1 bilioni kwa kila wilaya hapa nchini tukafanya kilimo cha kisasa kwa kuangalia asili ya kila wilaya kiudongo, hali ya hewa na aina ya mazao yanayokubali.

SERIKALI: Kama Serikali yetu imeweza kujenga Zahanati kila Kata kwa bajeti ya Tsh.1.5 bilioni kwa sehemu kubwa nchini tunashindwa wapi sasa!

NINI TUFANYE: Tuanzishe mfuko wa kilimo kama ulivyo mfuko wa jimbo ambao utasimamiwa na wakuu wa wilaya na utahusika na kufanya uwekezaji wa maendeleo ya kilimo kwa kila wilaya, na kila baada ya miezi 3 pawepo na taarifa ya nini kimefanyika ktk kila wilaya.

NGUVU KAZI: Tuchukue vijana wa vyuo vya kiliomo na ardhi mfano SUA, ARU nk watusaidie na tunufaike na elimu zao na ujuzi pia.

ANGALIZO: Serikali tumieni elimu za vijana maana hawa ni chachu ya maendeleo yenu na yetu kisiasa, kiuchumi na kitehama.

MAONI: Tukiamua kama taifa tunaweza sana.

Cc. Wizara ya Kilimo na Chakula
 
Hapa ndo tunapokwama. Mawazo yale yale ya kijima. Unacho shauri hapa ndo kimekuwa kikifanyika kwa miaka yote na bado kuna matatizo ya ajira ana kuna matatizo ya kilimo.

Infact Tanzania hakuna ukosefu wa ajira. Ila kuna ukosefu wa fikra
 
Back
Top Bottom