Mtazamo; Juu ya Hotuba ya Sheni Kuhusu Kuchoma Moto Makanisa

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,397
Baada ya kimya kingi toka makanisa yapigwe kibiriti huko z'bar hatimaye Mhe. Mkuu wa kisiwa hicho ameongea jana. Katika hotuba hiyo alisikika akipinga vikundi vya kidini kutumika kisiasa. Pia alitoa pongezi nyingi kwa jeshi letu la polisi kwa kuleta udhibiti wa machafuko! Hapa ndipo aliponikera mhe huyu. Hivi ni kweli polisi hawa wanastahili pongezi? Ni pongezi kwa lipi walilofanya, wakati tunaambiwa jumla ya makanisa 25 yamepigwa kibiriti toka mwaka 2001? Polisi hawa wamekuwa wapi hadi matukio haya yanatokea? Je ni kweli polisi hawana intelijensia ya kuangalia viashirio vya uvunjifu wa amani? Au wanasubiri hadi waone moto unawaka ndio wanachomoza na kurusha moshi wa machozi?

Kinachonikera zaidi katika hili ni kitendo cha serikali ya smz hasa viongozi wake wa juu kutokuwa wazi kulieleza hili moja kwa moja umma uelewe. Tunajua ni wazi hawataki muungano! Wawe wazi basi! Waliweke hilo bayana, tujue badala ya kuendelea kunyanyasa wabara waishio huko visiwani. Mbona wao wamejazana bara na hakuna anayewabugudhi? Nenda dsm, mbeya, songea, tabora n.k utakuta waz'bar tele! Wanafanya mambo pasipo bugudha yoyote! Hivi Tunafaidika nini na muungano huo, zaidi ya makelele ya kila siku eti tunawanyonya waz'bar. Tunawanyonya vipi? Haileweki!

Kwa upande wa bara pia, ni wakati viongozi wetu wachukue hatua tumechoka na haya matusi na manyanyaso wanayopata hawa wenzetu waishio visiwani. Viongozi wetu acheni siasa chukueni hatua kabla hatujashuhudia mambo mabaya (mungu aepushie mbali) yakitokea! Uongozi unapaswa uchukue hatua ngumu kuhusu muungano badala ya kusema tu mambo ya muungano hayapaswi kujadiliwa. Matokeo yake ndio haya.

Wote tumekuwa mashahidi wakati wa utawala wa mhe. Karume. tulikuwa tukimsikia shamuhuna na bwana himid wao walikuwa wazi kuelezea wanavyokereka na muungano. Japo litabaki swali je walikuwa wanawakilisha mawazo ya nani, je ni msimamo wa serikali yao au ni mawazo yao binafsi? Kwa kiasi kikubwa naamini huo ndo msimamo wa smz kwa sababu hakuna aliyekuwa akiwapinga watu hawa! Kauli zingine chafu za kupinga muungano na kuvunja heshima zilitolewa na bwana jussa, tena hadharani na media zilimrekodi, Lakini hakuna mamlaka yeyote (si z'bar wala bara) iliyotoa tamko lolote kuhusu kauli hizi za huyu mheshimiwa. Leo hii tunaaminishwa eti wale walochoma makanisa ni wahuni wachache, kweli? Kitakwimu ni zaidi ya makanisa 25 yamechomwa toka mwaka 2001 huko z'bar, hawa wanaachwa na kupuuzwa kwa kauli nyepesinyepesi tu eti ni WAHUNI!
 
Dk. Shein kamwaga MBOGA. Ngoja niende kwa Mangi nikanunue unga Nisonge ugali chakula kinoge.
 
Back
Top Bottom