Mtazamo: Je Lema aendelee kubaki nje ya bunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtazamo: Je Lema aendelee kubaki nje ya bunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bilionea Asigwa, Apr 20, 2012.

 1. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  Kwa wale waliopata nafasi ya kumsikiliza GODBLESS LEMA hata mara moja watakubalina na mimi kuwa jamaa ni mtu makini mno hasa anapopanda jukwaani kunadi chama na sera zake..Lema ni mtu mwenye mvuto mno hasa kwa vijana machipukizi walioko mikoani ambao hawapati nafasi ya kufuatilia siasa kwa undani; Kwa vijana wa kawaida Lema anaonekana kama JEMBE hasa nadhani ni kutokana na umri na style yake ya kuwa MSIKIVU na INTERRACTIVE PERSON..

  HOJA YANGU
  Tangu alipokabidhiwa chopa kukinadi chama kule kanda ya ziwa inaonekana watu wamevutwa sana kupenda kumsikiliza potelea mbali kutaka kumwona tuu.. SWALI ni je uongozi una haja ya kumbakiza nje ya bunge ili kuendelea kukijenga chama hasa kule vujijin ambako bado CCM INA MASHIKO KIMTINDO?? akisaidiana na DR SLAA?? au arudi ndani na yeye aongeze nguvu bungeni??

  Nnachojua mimi wabunge wengi wa MAGAMBA kwa siasa zao huwa hawarudi majimboni mpaka muda wa uchaguzi ukifika.. sasa je kama hili jembe litatumia muda mwingi kupita pita huku na kule kukinadi chama vijijin hatuoni kuwa itakua na tija zaidi kwa chama kama ilivyokua kwa DOCTA kukaa nje ya bunge??

  ni mtazamo wangu tu..

  NAOMBA KUWASILISHA...
   
 2. Nduka Original

  Nduka Original JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 753
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari bwana,
  Mimi namjua Lema vizuri sana na yeye pia ananijua. Lema ni mzuri sana jukwaani kwenye kuhamasisha.
  Na ninafikiri ni mbunge pekee ambae amekiingizia chama wanachama wengi sana. Hivyo chama kinamkubali.

  Nashauri aendelee kubaki nje ili aleteee chama wanachama. Kwa bungeni Lema hana uwezo na ninahisi ni kwasababu tu ya elimu yake kuwa ndogo.

  Unajuwa huwezi mfananisha Lema na Zitto ila wote ni muhimu sana kwa chama na taifa kwa ujumla.
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapana asibaki nje ya bunge kwani mchango wake ndani na nje ya bunge ni muhimu sana. Naamini kabisa Magamba watakuwa wanajutia sana kumsimamisha ubunge kupitia mahakama zao na sasa matokeo yake wanayaona.

  Kipindi ambacha atakuwa yupo nje ya ubunge kinatosha kabisa akirudi bungeni nako kunachimbika tena.
   
 4. M

  Martin Jr JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lema anauwezo ndani na nje ya bunge , na hata elimu yake ni kubwa tu : ADVANCE DIPLOMA HR , certificate EFFECTIVE MANAGEMENT OF LEADERSHIP , NA pia anachukua BBA NA diploma ya Project managent , nimeona nikusaidie ujue wewe amabe humjui Lema, Maoni yangu Nje ya Bunge au ndani ya bunge huyu kamanda sio mnafiki
   
 5. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Lema ameonyesha nuru kwa vijana. Amekuwa sio mwoga kueleza ukweli na kuwapa elimu ya urai wananchi wanyonge.

  Binafsi naona kazi hii kwa sasa inahitaji mtu aina ya Lema. Kwa sasa wampe hili jukumu na baada ya kukamilisha ukombozi wa kweli arejee kwenye ubunge ili kuendeleza mapambano!
   
 6. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tuwaachie CCM wachague wenyewe wanakoona itakuwa ni nafuu kwao. wao ndo wameshikiria ubunge wake hivyo wataamua either kubaki nje ya bunge na kuiua CCM huko vijijin ni nafuu kwao au arudi bungeni aendelee na kuwawasha wizara ya mambo ya ndani?

  Nadhani Lema au Chadema hawana cha kupoteza katika hili maana vyovyote itakavyokuwa wao kwao ni neema tupu. Hata kama CCM watajaribu kuchelewasha rufaa bado itaendelea kula kwao!
   
 7. i

  israel s. malekela New Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Lema abaki 2 nje ya bunge ajenge mazingira ya ushindi mkubwa kwa chadema kitaifa ili ifikapo 2015 chadema tuchukue nchi. Jamani chadema mbona hamji kwetu moro?
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ndioooooooo oooooooo ooooooo ooooo abaki nje ya bunge.

  sauti inakwama nadhani nimeeleweka
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wewe ni mnafiki wa kutisha, hatutaki mambo ya bi. kiroboto hapa.
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kama alivyosema Ngonini, Hili issue anayeweza kuitolea clarification ni CCM. Na ninawahakikishia kwamba muda si mrefu wataanza kulaumiana kwa maamuzi yao ya kumfanya atange tange huko majimboni.
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mh. Lema kwa sasa aendelee kutoa elimu ya uraia kwa umma. Uchaguzi mdogo wa Arusha mjini ukiitishwa agombee tena kumbukeni yeye ni chaguo la umma.
   
 12. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Wanalaumiana sasa,..lema chanja mpaka uvinza.
   
 13. M

  Malova JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Maamuzi baada ya rufaa kusikilizwa ndio yatasema kama Lema aendelee kukijenga chama au arudi kuongeza nguvu mjengoni
   
 14. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lema mimi namkaubali sana manake anajua kujenga ushawishi kwa rika zote na anafaa popote ndani ya bunge na nje pia anatisha na huku Arusha uchaguzi mdogo ukija agombee tena maana haina hata haja ya kukampaini
   
 15. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Mchango wake bungeni sijauona,ila nje ya bunge ktk kukinadi chama chake namkubali sana.
   
 16. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Ila unatakiwa ujue yeye kuwa ndani au nje,hakuna unafuu kwa CCM!
   
 17. dallazz

  dallazz Senior Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lema jenga chama dunia ikutambue
   
 18. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Yote kwa yote Lema ni Jembe na kiunganisha kwa chama na wananchi. Vyovyote vile Lema awe bungeni au nje ya bunge ushawishi wake ni nyenzo tosha kwa kuleta mabadiliko. Kwa kuzingatia haki na utawala wa sheria Mh. Lema arudi bungeni akawatumikie wanajimbo wake wa Arusha mjini.
   
 19. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,316
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kaka, kwasasa Lema naye ni msomi, watu wengi bado wana mawazo ya kizamani, huyu jamaa amekuwa akisoma with Correspondent Cambridge Internatinal College na kufikia level hiyo na also hajaridhika, bado anapiga shule ili apate Degree, anyway, hii sio topic, ukweli ni kuwa Magamba lazima wanajilaumu kwanini walimnyang'anya huyu Ubunge wake, hi kifaa inafaa kote, kuwepo kwake nje tayari wenyeviti kadhaa wa magamba wameisha sariti chama chao, na hi kumbuka ni muda wa nusu mwezi tu, hizi mpaka hiyo rufaa yao itakapo jibu huo mwaka 1 si ndio chama chote kitakuwa kimeliwa, naomba tu connect dots hapa, hivi mnadhani huko kuamka kwa wabunge wa magamba Bungeni hakuna uhusiano wa kile alichokifanya Millya na wenzake? kama kina connection, je hayo sio madhara ya kunyang'anywa Ubunge bwana Lema?


  Mwendo mdundo, watanzania tupo nyuma yako, komaa hadi kieleweke.
   
 20. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Lema kwa hapa arusha si mtu wa kawaida,. Katushika wana arusha yani watu huku hawambii kitu kuhusu lema,. Lema twanga kotekote mjengoni hadi uraiani,. Nenda mbinga kwa komba, ileje,mtera, uyu had mafia bila kusahau chakechake
   
Loading...