Poa 2
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 1,294
- 1,288
Nawasalimu wote.
Moja kwa moja kwenye mada, Kama kichwa Cha uzi Hapo juu kinavyojieleza kwamba huu Ni mtazamo wangu TU na Kama nimepotoka nitakubali kushauriwa na kukosolewa kwa staha na matusi yote poa.
Kuna Mambo mawili ambayo huwa nayafikiria Sana lakini sipati majibu, na Mambo hayo ni:
(1) Mamlaka makubwa Sana ya RAIS kikatiba.
(2) Mamlaka makubwa ya tume ya uchaguzi ya Taifa
Mambo/ Mamlaka haya ipo siku na mda tutajutia na kujidharau sana watanzania, kwa kuruhusu kuishi juu ya makaburi haya.
Hivi watanzania na watawala wa Sasa mnawaza Nini? Binadamu wa Sasa na ulimwengu wa leo kweli tunaishi kwenye nchi ambayo Kuna watu wanaweza kufanya Jambo lolote bila kuthibitiwa, kuhojiwa Wala kushtakiwa.
RAIS na wale wenye Kinga ya kutoshitakiwa kwa makosa yoyote wafanyayo. Binadamu yeyote wa kizazi si wa kuaminiwa kwa kiwango hicho hata kidogo.
Magufuli alikuwa mfano mzuri Sana kwenye hili, na ccm mnaona hili Ni Jambo jema lakini hili Ni bomu lilikochumbani kwenu wenyewe na litawalipukia siku si nyingi.
Lakini pia tume ya Taifa ya uchaguzi kwamba ikishatangaza matokeo hairuhusiwa kupingwa wa kuhojiwa na yeyote ccm na watawala mnafurahia hili na kuona ndio kete ya ushindi lakini kumbukeni binadamu wa Leo si wa kuaminiwa kwa kiwango hicho hata kidogo,
Hilo Ni kaburi mnalofikiri mmewachimbia wengine lakini mtazikwa wenyewe kwenye kaburi hili siku si nyingi. Ninaomba kumalizia kwa kuweka maswali kadhaa ambayo Mara nyingi huwa najiuliza.
(1) Hivi itakuwaje siku pandikizi au adui yeyote wa Taifa letu akishika madaraka ya uraisi
(2) Hivi itakuwaje siku madaraka haya akipata kichaa,mwendawazimu, adui wa ccm akatumia Mamlaka haya kukifuta chama chenu?
(3) Hivi itakuwaje siku RAIS akaamua kuuza nchi au rasilimali za nchi atakavyo?
(4) Hivi itakuwaje siku mwenyekiti wa NEC kwa bahati mbaya, makusudi ama kwa kuhongwa au vyovyote vile akajitangazia mtu/ chama chochote kisichokuwa CCM kwamba kimeshinda uchaguzi?
Najua wachache watajigamba na kupinga kwamba haya hayataweza kutokea kwa vijisababu Kama tuna polisi majeshi na usalama wa Taifa lakini hoja hii imepungua nguvu Sana siku za karibuni hasa ukizingatia mifumo, miundo na sheria za uundwaji wa taasisi hizi.
Ninawaomba Sana CCM na watawala hayo Mamlaka haya si salama kwa nchi, CCM, watawala na watanzania na tuchukue hadhari kabla ya hatari hakuna aliye salama, kumbukeni maadui zetu wanatafuta mianya na wanaweza kuhonga yeyote tusiruhusu kwa nyakati flani kukabidhi uhai wa watanzania kwa mtu mmoja ambaye naye hajakamilika.
Haya Ni mawazo na mitazamo yangu TU jamani naomba kuelimishwa.
😁😁😁😁Ni mtazamo kutoka jamaa wa ighanuda😁😁😁