#COVID19 Mtazamo hasi juu ya chanjo ya Korona ni matokeo ya kivuli cha Hayati Magufuli kinachoishi

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Tukubali tukatae Sumu aliyoacha amepandikiza mwendazake ndiyo inayolitafuna taifa kwa Sasa kuhusiana na mtazamo hasi juu ya chanjo ya Korona. Kila mtu anakumbuka jinsi Magufuli alivyokuwaga na ushawishi.

Hivyo Msimamo wake juu ya chanjo ya Korona kabla ya kifo chake umebaki mioyoni na akilini mwa watu kiasi kwamba hadi leo asilimia kubwa ya Watanzania hawana Imani na chanjo hizi.
 
Kwani kuna shida gani kuwaaminisha watanzania kuhusu Jonson Jonson vaccination,na sio chanjo zingine , na Kwa nini uwasainishe form kwamba likitokea la kutokea wasikuhusishe ..!! Hii ndo inafanya gwajima ajichukulie credit , badala ya kujibu Kwa hoja mnaishia kumchimba mkwara na kumtukana
 
Tukubali tukatae Sumu aliyoacha amepandikiza mwendazake ndo inayolitafuna taifa kwa Sasa kuhusiana na mtazamo hasi juu ya chanjo ya Korona. Kila mtu anakumbuka jinsi Magufuli alivyokuwaga na ushawishi, hivyo Msimamo wake juu ya chanjo ya Korona kabla ya kifo chake umebaki mioyoni na akilini mwa watu kiasi kwamba Hadi leo asilimia kubwa ya watqnzania hawana Imani na chanjo Hizi.
Wewe ndo umenena sahihi,maana watu wengi wanakzana kuwaona watanzania wabishi au akili wamekopesha kumbe shida ni serikali iliyopita,hata baadhi ya viongozi walioko sasa na wenyewe walikuwa na msimamo huo huo,leo tunalaumu watu haiwezekani
 
Hebu fuatilia mbona sehemu mbalimbali duniani wametokea wanozipinga.

Mpaka imefikia viongozi kuwapiga mkwara wasiotaka kuchanja kama ilivyo huko ufilipono.

Hili suala limetugawanya makundi mawili kama sio matatu, haijalishi rangi wala utaifa.

Na hii ni kutokana na unyeti wake hakuna anayekubali kuamuliwa katika suala linalohukumu hatma ya uhai/afya yake.

Kila mtu inabidi ajiridhishe/aridhie.
 
Mkuu hii issue ya watu kutopenda kuchanjwa siyo ya Tanzania peke yake, hata ulaya na marekani bado wanahangaika kuwashawishi watu wakubali kuchanjwa.

Japo waswahili wanasema mzigo mzito mbebeshe mnyamwezi, kwa hili Magufuli mnamuonea bure. Ingawa ni kweli kwamba misimamo yake imechangia kwa kiasi fulani, lakini karibu dunia nzima inahangaika kushawishi watu wazikubali hizo chanjo.
 
Tuliwaambia magufuli alikuwa nabii mnagoma.

Leo hii ulimwengu wote umefarakana kuhusu hii takataka,nayeye alizungumza haya mwaka na miezi iliyopita.
 
Mkuu hili suala ni kweli Ila hata Kama Magufuli angesema chanjo zinafaa, bado Kuna watu wengi wangezikataa.
Nakupa mfano. Marekani na Europe Kuna watu wengi sana wanazikataa chanjo, hapo napo utasema walimsikiliza Magufuli?
Hili suala naona watu wanampaisha tu Magufuli
Kama angekuwa ameamua watu wachanjwe, wangechanjwa tu watake wasitake, alikuwa ana njia zake za kutimiza analolitaka...JWTZ wangeanza kupita nyumba kwa nyumba kuchanja🤣
 
Tukubali tukatae Sumu aliyoacha amepandikiza mwendazake ndo inayolitafuna taifa kwa Sasa kuhusiana na mtazamo hasi juu ya chanjo ya Korona. Kila mtu anakumbuka jinsi Magufuli alivyokuwaga na ushawishi, hivyo Msimamo wake juu ya chanjo ya Korona kabla ya kifo chake umebaki mioyoni na akilini mwa watu kiasi kwamba Hadi leo asilimia kubwa ya watqnzania hawana Imani na chanjo Hizi.
Swala la chanjo halijakaa sawa kuna maswali mengi yanayohitaji majibu,
  • Unaambiwa kuchanjwa hakukuzuii kupata Corona bado kuna uwezekano wa kupata. Sasa swali ni kwanini tuchanje?
  • Hata baada ya kuchanjwa unashauriwa kuvaa barakoa - why?
  • Chanjo uliyopewa haizuii new variants wa Corona kukudhuru. So inamaana kila strain mpya ya Korona inabidi upate chanjo yake?
Naamini Serikali ya awamu ya tano ilikuwa inatupeleka katika kujenga herd immunity na ndio iliyotuvusha awali.
 
Tukubali tukatae Sumu aliyoacha amepandikiza mwendazake ndiyo inayolitafuna taifa kwa Sasa kuhusiana na mtazamo hasi juu ya chanjo ya Korona. Kila mtu anakumbuka jinsi Magufuli alivyokuwaga na ushawishi.

Hivyo Msimamo wake juu ya chanjo ya Korona kabla ya kifo chake umebaki mioyoni na akilini mwa watu kiasi kwamba hadi leo asilimia kubwa ya Watanzania hawana Imani na chanjo hizi.
Sayansi gani hiyo inashindwa na maneno tena ya marehemu. Sayansi ijipiganie kwa ufanisi. Vinginevyo maneno ya marehemu ya ujasiri ni chanjo tosha
 
Tatizo lilianzia hapa na ilikuwa ni matokeo ya wizi wa kura.
 
Tuliwaambia magufuli alikuwa nabii mnagoma.

Leo hii ulimwengu wote umefarakana kuhusu hii takataka,nayeye alizungumza haya mwaka na miezi iliyopita.

Hamna nabii dhalimu, tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule mtu muovu bila damu kumwagika.
 
Swala la chanjo halijakaa sawa kuna maswali mengi yanayohitaji majibu,
  • Unaambiwa kuchanjwa hakukuzuii kupata Corona bado kuna uwezekano wa kupata. Sasa swali ni kwanini tuchanje?
  • Hata baada ya kuchanjwa unashauriwa kuvaa barakoa - why?
  • Chanjo uliyopewa haizuii new variants wa Corona kukudhuru. So inamaana kila strain mpya ya Korona inabidi upate chanjo yake?
Naamini Serikali ya awamu ya tano ilikuwa inatupeleka katika kujenga herd immunity na ndio iliyotuvusha awali.

Ilikuvusha ww uliyekuwa hai, lakini iliua watu kadhaa kama ifanyavyo sasa. Kilichofanyika kipindi cha utawala wa yule mtu muovu ni kuficha data fullstop.
 
Back
Top Bottom