Mtazamo: Bado kinachofanyika awamu hii kipo sahihi

MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,826
5,451
Habari wana jf.Niende moja kwa moja kwenye Hoja yangu kuu,Nimekua nikifuatilia hoja mbalimbali za upinzani hasa KUPINGA kile kinachokuwa kinafanyika Tanzania. Lakini katika hoja hizi naweza sema hazina mashiko zaidi ya SIASA UCHWARA au NYEPESI,Hivi mtu anapinga kununua Ndege au ujenzi wa flyovers au SGR kwa kigezo cha kuwa sio hitaji la watanzania anakwambia watanzania wanahitaji madawa,maji,mikopo nk.Hivi Hizi hela zote zitapatikana wapi kama Hatuna miundombinu au vyanzo mbalimbali vya kuwezesha kupata hizo hela tena kwa uhakika kuliko kila siku kukopa au kutegemea vyanzo vichache vya mapato?Ni faida gani itapatikana baada ya hii miradi yote kuwa stable na kuanza kuingiza faida?

Kwa akili ya kawaida ni rahisi sana kuona ni matumizi mabaya ya pesa lakini baada ya muda mapato ya SGR ndio yatakua chachu ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya madawa,Ndege,flyovers nk.Hivi vyote baada ya kukamilika naamini itakua ni vyanzo vikubwa mno vya mapato tena sio vya mda,hivi ni vya kudumu na hii naamini itapunguza hali ya asilimia flani ktk kukopa nje au kuombaomba misaada tena kwa masharti.Naamini hali ni ngumu kweli lakini kwa mtu mwenye akili timamu akiwa na mia na kesho yake haijui basi atashinda njaa kwa kuiwekeza Hiyo mia izae ili kesho awe na matumaini ya kusurvive.

Hela inayopatikana ni inatosha kulipa mishahara,kuajiri na madawa nk,lakini naamini haitoshi kujenga mazingira mazuri ya kufanya hizo hela za mishahara nk ziendelee kuwa stable,so unafanyaje?Hapa ni lazima uache kimoja ili ujenge mazingira ya uhakika.Na hili sio Tanzania tu,ni Kenya,Ethiopia nk.Huko tunakosifia kila siku sio kweli kwamba hawana mattz,Kenya kuna mattz ya Ajira,mishahara,Ethiopia kila siku watu wanakimbia.MAAJABU ni kusifia SGR,flyovers na ndege za Kenya na kuponda za Tanzania. Unaweza jiuliza hivi Kenya walimaliza mattz yote ya wananchi ndipo wakaanza kujenga SGR?au ndipo wakaanza kununua ndege?Au kipaumbele cha wananchi wa Kenya kwa sasa ni SGR?Kama hapana,sasa iweje UPINGE yanayofanyika Tanzania na hayohayo yakifanyika Kenya au sehem zingine na katika mazingira sawa UUNGE mkono?

Mattz ya ajira hayajaanza awamu hii,mishahara kusumbua au mikopo haijaanza awamu hii.Toka nakua naliona hili,Kila awam imepita na strategies zake na imeacha mattz yale yale.Nafikiri Tuache utawala uliopo nao uoneshe uwezo wake.Yeye anaamini ktk njia hii kama sio kutatua basi atapunguza mattz ya watanzania!Kulazimisha mtu kupita sehem ambayo mlikua mnasema jamaa kafeli sifikiri ka ni sahihi.Hadi sasa hakuna kiongozi aliyefanya kitu bora kwa watanzania coz hata huyu akitoka wapo watakaokuja kuimba nyimbo zake na kusema jamaa alikua bora alifanya hivi na hivi.

Ahsanteni.
 
Ujumbe mzuri ila hawawezi kuuelewa kwa sababu wamekaririshwa. Kwa sasa wapinzani wa magufuli nawafananisha na mkulima anayetaka kula mbegu kisha aendelee kuomba msaada wa chakula badala ya kupanda hizo mbegu kidogo kisha avune kingi. Matatizo yanayozungumzwa yamekuwepo miaka mingi sana. Na watangulizi wote wa Rais hawakuweza kuyatatua bali walipunguza kadri ya uwezo wao. Huyu wa sasa amekuja na mkakati mwingine wa kutufanya tuwe na mapato endelevu . Lakini kwa kuwa wengi tunaiangalia leo yetu na si kesho ya watoto wetu tumebaki tukikebehi na kutusi juhudi za Rais wetu. Mwenye macho aone. Go Magu Go. .
 
Kwa hiyo tusubiri flyover na mandege yalete hela ndo tunywe maji safi na kupata dawa...KWELI ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom