Mtazamo: Afadhali wangeanzisha mahakama maalumu ya makosa ya "Uchochezi" kuliko kuanzisha mahakama ya mafisadi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Nikijaribu kuangali idadi ya wanaoshitakiwa kwa makosa ya uchochezi alafu nikilinganisha na wale wanaoshitakiwa kwa makosa makubwa ya ufisadi,nashawashika muamini ni bora wangeanziha mahakama maalumu ya makosa ya uchochezi na si ufisadi kama walivyofanya.

Katika mahakama hii ya mafisadi sijui kama kuna mtu hata mmoja ambae mpaka sasa ameshashitakiwa kwa ufisadi (grand corruption) lakini orodha ya wanaoshitakiwa kwa uchochezi mpaka sasa hakika inajitosheleza na pengine ni wakati muafaka sasa tukawa na mahakamu maalumu ya kushugulikia makosa haya ya uchochezi.

Tafsiri ya hali hii ni kuwa kwa sasa tatizo letu kubwa ni "uchochezi" na wala si ufisadi.

Ni mtazamo tu jamani na wala si uchochezi.
 
Hivi hujaenda tu kujionea kweli kesi huko zipoje ukatuletea habari au unasubiri ruzuki uende kufatilia kiudaku?
Nenda utuambie maana na mimi nasubiri kuzisikia kesi za hiyo mahakaka mpya maana hata mapaparazi hawataki kuziandika.
 
Afadhali leo angalau umekuja na mada tofauti.........sio kila dakika kumuwaza TL tu.
Hongera kamanda.
 
Hivi hujaenda tu kujionea kweli kesi huko zipoje ukatuletea habari au unasubiri ruzuki uende kufatilia kiudaku?
Nenda utuambie maana na mimi nasubiri kuzisikia kesi za hiyo mahakaka mpya maana hata mapaparazi hawataki kuziandika.
Hata aibu huoni!!
 
Hata hueleweki umeandika nini ?
 
Back
Top Bottom