Mtazamaji (observer) katika uchaguzi ni nani, ana majukumu gani na yana faida gani kwa nchi?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
624
934
Cj7QjnEUUAEw-69.jpeg


Mtazamaji wa Uchaguzi ni Nani?
Katika chaguzi zote Duniani huwa kuna watu wanaitwa WATAZAMAJI(OBSERVERS) hawa wanaweza kuwa watu Binafsi kutoka ndani na nje ya Nchi.

MAJUKUMU
Jukumu kuu la watazamaji ni kutazama matendo na shughuli zinazoendelea katika mchakato wa Uchaguzi na kuhitimisha shughuli yao katika siku ya kupiga kura yenyewe au zaidi.

Jukumu lao ni kuangalia katika mchakato mzima uwanja wa ushiriki na utekelezaji wa matakwa ya kila mmoja unakuwa sawa kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi. Hapa ni lazima tukumbuke na kuzingatia kuwa matendo, shughuli na wajibu wa kila mmoja katika mchakato wa uchaguzi unasimamiwa na Sheria na Kanuni zake.

WAJIBU MAHUSUSI
Mtazamaji atatazama na kuandika maoni yake juu ya masuala yanayotendwa kwa uzuri na ubaya katika mchakato mzima na maoni hayo yakizingatia matakwa ya sheria atayawasilisha kwa Taasisi iliyomtuma ambayo itaandaa taarifa ya jumla na kuikabidhi kwa Tume ya Uchaguzi. Endapo ni Mtazamaji huru atakabidhi maoni yake moja kwa moja kwa Tume.

HAKI
Mtazamaji ataruhusiwa kuingia katika vyumba vya kuhesabu kura na kutolea matokeo. Ataingia pia katika vyumba vya kupigia kura vilivyopo katika eneo lake la utazamaji, na muda wote atatakiwa kuwa katika sare inayomuonyesha na kumtambulisha kuwa ni Mtazamaji na sare hiyo itakuwa na nembo ya Tume na kitambulisho chake kitakuwa na jina lake halisi na Nembo ya Tume ya Uchaguzi.

Kama atakuwa na chombo cha usafiri lazima kiwekwe stika na maandishi makubwa yanayosomeka kuwa ni Mtazamaji.

FAIDA YA KAZI ZA MTAZAMAJI
Mtazamaji hutoa maoni ya mambo mazuri yaliyofanywa katika mchakato wa kupiga kura na kuyawasilisha Tume ili waweze kuyazingatia katika chaguzi zijazo. Pia mtazamaji hutoa maoni ya mambo mabaya yenye kuleta kasoro katika uchaguzi ili Tume pia iyarekebishe katika uchaguzi ujao ili kuendelea kudumisha Demokrasia na kuhimiliza ustawi wa nchi katika amani na umoja.

Nimalizie kwa kuishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kulipa shirika letu FAIDIKA WOTE PAMOJA(FAWOPA TANZANIA) majukumu mawili Makubwa katika Uchaguzi huu wa 2020. FAWOPA imeaminiwa na kupewa vibali viwili na Tume ya Uchaguzi NEC; kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga kura na kibali cha Kutazama Uchaguzi Katika Mikoa mitatu ya Kusini mwa Tanzania (Lindi, Mtwara na Ruvuma). Kwa imani hiyo ya Serikali dhidi yetu tunasema ahsante sana nasi tutaitendea vema imani hii kwa kuonyesha Uzalendo wa hali ya juu na kutanguliza Maslahi mapana ya wananchi wa Tanzania na zaidi sana kuiletea heshima kubwa sekta yetu ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Tanzania.

Mwandishi Komba BB
Mkurugenzi
FAWOPA TANZANIA
 
Tafuta ripoti za waangalizi wa uchaguzi za 2015 na 2010

Angalia mapendekezo waliyotoa na hatua zilizochukuliwa na Serikali kuzifanyia kazi

Then niambie wakija tena 2020 watakuta some recommendations have not been implemented because the receiving country is obliged to adhere to their recommendations.

That is why the developed countries do not need as to observe their elections. its just a game of intelligence collection nothing else.
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom