Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,883
MTAWALA AZIBAYE MIDOMO WATU NI MBAYA KAMA SHETANI
Kwa Mkono wa Robert Heriel.
Mtu yeyote anayependa kuziba watu midomo wasimseme jua huyo ni kama shetani, hivyo ndivyo andiko hili ninavyoanza nalo.
Shetani ndio anapenda mambo ya sirini, kuficha ficha, kuziba watu midomo wasiseme mabaya yake. Kuzuia uhuru wa watu kwani katika uhuru shetani anajua ubaya wake utadhihirika.
Kwenye uhuru kuna ukweli, penye ukweli kuna uwazi, penye uwazi kuna haki, kwenye haki kuna amani, kwenye amani kuna furaha.
Mtawala yeyote hata afanye mema gani lakini kama ataminya Uhuru basi ameminya haki ya msingi ya mwanadamu, uhuru ndio maendeleo, ndio maana kila taifa kuna siku ya kusherekea uhuru wao kila mwaka. Uhuru ndio maendeleo. Sasa mtu anapoziba watu midomo ni kwamba hataki watu waongee pale anapokosea, ni kama shetani tu.
Watu wa namna hii hutumia nguvu kubwa kwenye propaganda za kujisifia na kuponda wale wote wanamkosoa ikiwezekana kutaka kibali cha kuweza kuwaua hata kama sheria haziruhusu.
Kwa vile jamii yetu wengi wa watu ni wajinga wasio na akili ya kuchambua mambo ni rahisi kwa kiongozi wa namna hii kuchota akili zao.
Huwaga nasemaga Ujinga ni upofu, hivyo watawala wa namna hii hutumia ujinga wa watu wengi kuwalaghai kwa propaganda za hovyo ili aonekane mwema.
Hatukatai mtu kuwa mjinga hilo hatuwezi kukataa, hiyo ni haki ya mtu kuchagua ujinga au werevu, tunachokataa ni kuvunja sheria na haki za binadamu kwa kisingizio cha ujinga au werevu. Tunachopishana na watawala madikteta ni kuvunja haki za watu kwa kukandamiza uhuru wa watu hasa wale werevu watakaompinga kutokana na matendo yake maovu
Madikteta huwatumia zaidi watu wajinga na masikini katika kujizatiti kushika dola. Madikteta hawawezi kushikamana na watu werevu na matajiri kwani utawala wao utakuwa mashakani. Werevu na matajiri wanajua umuhimu wa uhuru katika maisha yao. Lakini masikini na wajinga wao hawana tofauti na wanyama, wao lolote kwao ni sawa ilimradi maisha. Ni kama kuku au mbwa wa kufuga, hata uwafunge bandani wao hawaoni shida ilimradi wajipatie chakula hata kama sio mlo kamili. Lakini Watu werevu na matajiri wanajua maisha ni zaidi ya chakula, maisha ni uhuru wa kuishi bila kuathiri wengine.
Ndio maana madikteta wote wawapo kwenye majukwaa hujifanya kuponda matajiri kwa kusema ni wezi na wanawadhulumu masikini, lengo lao ni kupata wafuasi kutoka watu masikini, na kwa vile masikini wengi wao ni wajinga hujikuta wakimpenda Dikteta zaidi kwani wanaona yupo upande wao ilhali uchumi wao bado unakuwa dhoofu.
Madikteta pia, huwaponda werevu na wasomi kama vile maprofesa, na watu wote wenye vipaji vya muhimu wenye kutetea haki. Dikteta asimamapo jukwaani ni kawaida kumdhalilisha Mwerevu ili yeye(dikteta) apate sifa kwa watu wajinga wasioweza kuchambua mambo. Hivyo sio ajabu ukashangaa wajinga wakishangilia pale mwerevu adhalilishwapo na dikteta.
Mjinga na masikini wanafanana sifa kwa sehemu kubwa na wote hufurahi waonapo mwerevu na tajiri apatwapo na madhila.
Mtawala anayeziba watu mdomo kamwe usimuamini hata kama utamkuta mbinguni, ni shetani mbaya anayejaribu kuficha maovu yake.
Hata hivyo jambo moja ni dhahiri nalo ni; ukiziba watu mdomo ukiwa uhai, basi watu watakusema ukiwa Mfu. Hivyo akili kumkichwa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Mwanjelwa, Mbeya mjini