Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,874
Nilikuwepo mahakamani leo wakati Jaji Sirilius Matupa akitoa uwamuzi wake juu ya shauri la kupinga kuvuliwa Ubunge Mh.Tundu Lisu.
Nilivyomuelewa Jaji, tayari alikuwa anajua fika kuwa kitendo cha Spika kumvua ubunge Tundu Lissu kilikuwa batili.
Ndio maana hata kesi ya msingi kama ingeendelea Tundu Lissu angeshinda kesi asubuhi mapema na maamuzi ya Ndugai yangebatilishwa.
Ila Jaji alisema kuwa katika shauri hili, uchaguzi wa Mtaturu (kuchaguliwa Mtaturu) haukupingwa Mahakamani ila kulipingwa kiapo cha mtaturu (Mtaturu kuapishwa).Jaji akaendelea kusema kupinga kuapishwa sio kupinga mtu kuwa Mbunge ,kesi nyingi zinazofunguliwa huwa ni za kupinga uchaguzi (Mchakato wa uchaguzi) sio kuapishwa,hivyo mahakama haiwezi kupinga kiapo cha Mtaturu cha Ubunge sababu ni kuingilia muhimili ungine. Hivyo Mtaturu ataendelea kuwa Mbunge.
Kuja kwa kutengua maamuzi ya Spika Ndugai,kama kesi ya msingi itaendelea na mahakama ikatengua uwamuzi wa Ndugai ,hali itakuwaje?
Maana yake moja kwa moja ,Mh.Tundu Lissu atakuwa Mbunge wa Jimbo lake ,vipi Mh. Mtaturu? Je, Jimbo linaweza kuwa na Wabunge wawili?
Akasoma kifungu cha katiba kikisema ,Jimbo litakuwa na Mbunge mmoja tuu .Hivyo kutengua maamuzi ya Spika itakuwa uvunjivu wa katiba sababu jimbo la Mh.Tundu Lisu tayari kuna mbunge ambaye mchakato wa uchaguzi wake haujapingwa na mtu yeyote .
Ushauri wangu
Kwa namna kesi ilivyo hakuna haja ya kukata rufaa,jambo kubwa hapa ni kurudisha kesi mpya mahakama kuu ,ila kuwe na marekebisho kesi hiyo mpya ijumuishe wote , Ndugai na NEC kupitia AG kwa kuitisha uchaguzi jimbo lenye Mbunge na huyo Mtaturu pia kama mshtakiwa namba tatu kwa kushtaki mchakato wake mzima wa kuchaguliwa kwake kuwa Mbunge.
Kuwa alichaguliwa kinyume na sheria na sio kihalali (illegally ) sababu jimbo hilo lilikuwa na Mbunge ila yeye hakukataa kugombea, alikubali huku akijua jimbo hilo linamtu ambaye ni Mbunge halali wa Jimbo hilo Mh.Tundu Lisu.
Kufanya hivi ni kuitengenezea mahakama njia ya kutoingia katika mgogoro wa kikatiba , Mtaturu akijumuishwa ndio njia pekee ya mahakama kumgusa kwa kumtengua na Mtaturu akitenguliwa kuna kuwa na uhuru wa mahakama kutengua uwamuzi wa spika Ndugai ,sababu jimbo litakuwa wazi hivyo maamuzi ya Ndugai yakitenguliwa ubunge utarudi kwa Mh.Tundulisu katika jimbo ambalo litakuwa wazi.
Tofauti na sasa Mtaturu hajaguswa yaani hajashtakiwa kupinga mchakato wake batili wa uchaguzi .Hivyo mahakama imejikuta katika mgogoro mkubwa wa kikatiba.
Nashauri kesi ifunguliwe upya vizuri , Mtaturu ajumuishwe yeye na Spika na NEC (kupitia AG) ili kuipa mahakama uhuru wa kutengua maamuzi ya Spika Ndugai,bila kuingia mgogoro na katiba.
Pia rai yangu,watu tupinguze kulalamika kuwa mahakama inatuonea ,hivi tusipokimbilia au kuiamini mahakama tutakuwa wageni wa nani tena ? ,Kama tunajua hatuwezi kuingia barabarani sasa hivi basi tuendelee kuamini mahakama kama kimbilio letu la kila jambo, tupunguze kulalamika.Mahakama ndio pumzi tuliyobaki nayo sasa ,tusilazimishe kuikata wakati hatuna mbadala ungine.
Shukrani.
Abdul Nondo
abdulnondo10@gmail.com
0659366125.