Mtatizo haya ya udini nchini yanasababishwa na mambo haya tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtatizo haya ya udini nchini yanasababishwa na mambo haya tu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bullet proof, Feb 20, 2013.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. bullet proof

  bullet proof Member

  #1
  Feb 20, 2013
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi sasa nchi yetu inashuhudia mzozo mkubwa wa kdini ambao mpaka sasa umegharimu maisha ya watu, mali, nyumba za ibada nk kinyume kabisa na mazoea yawatanzania.

  Hata hivyo tatizo hili limesababishwa na mambo yafuatayo:

  Kwanza, tabia ya watanzania/waumini wa dini kutikuwa na tabia ya kujisomea. Waumini wengi hususani vijana hawana utaratibu wakusoma vitabu vya dini ie quran na au biblia. Hali hii imewafanya wahuni wachache kutumia mwanya huu kufundisha na kutafsiri aya za misahafu hii kwa kupotosha ili kulenga maslahi/matakwa/hisia zao binafsi. Mathalan, Uislam (waislam) ambao hasa ndo unalalamikiwa zaidi kwa kuwa sababu ya haya matatizo (mauaji, uharibu wa mali nk) hakuna sehemu unafundisha mauaji holela ya kikatili kama haya. Isipokuwa baadhi ya mashekhe/maustaadh mfano wa HASSAN ILONGA wameamua kufundisha chuki tofauti kabisa na Uislam wa MOHAMMAD (SAW). Kiukweli uislam anaoufanya mtu kama ILONGA na ule wa mtume (SAW) ni tofauti sana.

  Pili, Kutojulikana vizuri kwa historia ya nchi zetu ie Tanganyika na Zanzibar. Hii imesababishwa na vijana wengi kutokuwepo wakati wa kupigania uhuru/mapinduzi-wachache sana wamebahatika kusoma historia hizi shuleni lakini wengi zaidi hata hii historia ya kusoma hawaijui. Wengi wanalalamika kuhusu Zanzibar kujitenga na Tanganyika-hii siyo sawa. Mfano, wazanzibar tunaingizwa kwenye mtego ambao hatuujui na watu wa aina ya MAALIM SEIF S. HAMAD, SHEKHE FARID WA UAMSHO nk ambao wanadai ZANZIBAR TUSISHEREHEKEE SIKUKUU YA MAPINDUZI BADALA YAKE TUSHEREHEKEEUHURU WA '63 ALIOPEWA MWARAB.Hawa wamekuwa wakihamasisha wazanzibar kudai kujitoa kwenye muungano kwa kutumia MWAMVULI WA DINI-UISLAM ILI KUPATA KUUNGWA MKONO. Laiti wanzanzibar tungejua adma ya watu hawa ( MAALIM SEIF, FARID, UAMSHO nk ) tungekataa haraka, tunaingizwa menge kwa kutuchonganisha wa ndugu zetu watanganyika ili wapate KURUDISHA WAARAB KWA MGONGO WA UHURU WA '63 WA ZANZIBAR.

  Muungano haujaleata ukristo zanzibar. ukristo umekuwapo zanzibar miaka mingi sana tu kabla ya Uhuru. Mfano kanisana Anglikan la Mkunazini limejengwa mwaka 1873, mikaka takriban 91 baadaye
  ndo muungano unatokea.

  Tatu, Uongozi mbovu. Viongozi wengi tuliowachagua ili kushughulikia matatizo yetu wamegeuka nafasi zao kuwa pahala pa kujipatia neema binafsi huku watanzania wengi tukiendelea kuwa masikini. Ndiyo maana vijana wameendelea kutumiwa sana kwenye vurugu hizi bila hata kufikiria kwa sababu tu wameahidiwa kitu kidogo, na wajanja wachache wamewalaghai kuwa tatizo la umaskini limesabababishwa na ukristo!!!


  ----------------------WAY FORWARD---------------------

  1. Siku za sherehe za MAPINDUZI/MUUNGANO/UHURU wazee wangesaidia kutoa historia za nchi zetu hadharani ili kila mwanachi aijue vizuri nchi yake na malengo ya Uhuru/Mapinduzi badala ya hawa wazee kuletwa tu uwanjani tunawaona then wanaondoka bila kutuambia lolote kuhu nchi zetu.

  2. Waumini wa dini tusome vitabu vyetu ili itusaidie kutopotoshwa na mashekhe/wachungaji/mapadre wahuni kwa kisingizio cha nafasi zao. Hakuna mtu mwenye hodhi(monopoly) ya elimu. Kuwa shekhe/mchungaji/padre haimaanishi wanajua kuliko sisi waumini/maamuma.

  3. Viongozi wa serikali simamieni utawala bora wa sheria. Acheni visingizio. Kuna baadhi ya viongozi, majina yapo, wameshindwa kutekeleza wajibu wao badala yake wanakimbia kwenye misikiti/makanisa kujisafisa eti wanatengwa na wenzao wa dini tofauti hali ambayo huchochea chuki miongoni mwa wananchi.

  Watanzania pia tuamke. Tuache kujitenga kwa dini/kabila/ukanda nk. Tukomae na viongozi hawa wababaishaji watimize wajibu wao.Tunaona jinsi elimu inavyoshuka nchini, badala tukae pamoja, tuseme pamoja, tunaanza kutengana eti oh, waislam tunafelishwa nk.


  MUNGU IBARIKI TANZANIA, HEKIMA, UMOJA NA AMANI ND NGAO ZETU!!!!!!!!
   
 2. MissM4C

  MissM4C JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2013
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,250
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  wellsaid kaka
   
 3. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2013
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Laiti watanzania wengi wangekuwa na mtazamo kama wa mleta hoja hali ya nchi hii isingefikia kiwango cha kukatisha tamaa kama ilivyo siku hizi!
   
 4. lucky sabasaba

  lucky sabasaba JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2013
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 1,673
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Bullet proof umechanganua vizuri sana..umaskini wa kutumiwa na kutoielewa dini ndio tatizo kubwa hapo..nimeishi kwenye nchi za kiislamu kwa miaka saba sasa sijawahi ona mambo yanayotokea Tz sasa,Saudi arabia ndio chimbuko la dini hiyo na zaidi ya 98% ni islams lakini ubabaishaji wa wao kujiona bora kuliko dini nyingine haupo..dubai kuna sehemu kubwa sana imetengwa kwa ajiri ya makanisa yote unakwenda kwenye malls kama spynes unapata mpaka pork(kitimoto)bila tatizo lolote..kama mtoa mada alivyosema tatizo ni kutosoma dini vizuri,islam ni dini nzuri sana tatizo ni cheap islams ambao wanaajifanya kuijua kumbe hawaijuhi..ndio maana nigeria,somalia pakstan kuna matatizo ya kidini yanayofanana..
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2013
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,599
  Likes Received: 5,928
  Trophy Points: 280
  Ningependa sana kuunga mkono hoja kwamba matatizo yanatokana na ukosefu wa elimu ya dini.Na kwamba ujinga huu unaosababisha matatizo.

  Lakini ukweli ni kwamba, dini ni kama udongo ambao uko tayari kufinyangwa vyovyote vile.

  Kama wewe ni mtu wa amani na unataka kutumia dini kuhubiri amani utapata mifano mingi tu ya kutumia.

  Kama wewe ni mtu wa shari na unataka kutumia dini kuhubiri shari, mifano ya shari mingi tu.

  Tatizo si ujinga wa dini. Tatizo ni ujinga period. Na umasikini unaoendana nao.
   
 6. H

  Honestdeos Member

  #6
  Feb 20, 2013
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukosefu wa haki sawa kwa kila mtanzania unachochea na fumua tofauti za kidini. Inapofikia hali hii, waumini wa dini tofauti wanapingana kwa kuamini ndiyo mapigano ya haki. Haki sawa kwa kila mtanzania. Na hii italetwa kwa uongozi mwema ulioungana katika kumletea kila mtanzania maendeleo.
   
 7. hekimatele

  hekimatele JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2013
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 9,500
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Mkuu umeongea mambo ya maana sana. Maneno kuntu.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 8. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2013
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  unemployment is too high! watu hawana kazi wala hawaoni dalili za kupata kazi. wewe unafikiri wakitumiwa kufanya mauaji kwa pesa watakataa? nchi kuwa na uchumi mbaya madhala yake ni mabaya sana kwa raia, wewe angalia somali, ,mali na Nigeria jinsi watu wanavyotumiwa kuleta unyama mitaani.

  Tanzania tulipuuza sana mpango wa kutafutia kazi mwananchi. tulikuwa tunawaita warululaji leo sasa tunawaita materorist! bado keshokuwa tutawaita rebels!
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2013
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,412
  Likes Received: 5,680
  Trophy Points: 280
  tatizo ni kukubali kutumiwa na wanasiasa!
   
 10. lucky sabasaba

  lucky sabasaba JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2013
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 1,673
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Hakuna hiyo point ya unemployment si sababu ata christians wengi tu hawana kazi..nashukuru gadhaffi hayupo he was the main sponsor wa wajinga wa kidini
   
 11. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2013
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,819
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Insha yako nzuri kwa urefu na kama uko shule ya kivukono wakati uleakini maneno mawili tu yanatosha kusemea hali tuliyo nayo Ukosefu wa haki


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 12. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2013
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,082
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  ni kweli kabisa, mkuu
  dini inaweza kutumika namna unavyotaka wewe muumini au mtumiaji wa dini hiyo au kiongozi wa dini hiyo.
  katika protestant ethics and spirit of capitalism max weber 1905
  alieleza namna dini ilivyotumika vizuri kufanya watu kuzalisha mali kwa wingi kwa kufwata vile preachers wao walivyokuwa wanhubiri makanisani. kufanya kazi kwa bidii kutunza muda na kuweka surplus na kwamba mwenye hazina kubwa ya mali duniani ndio atauona ufalmwe wa mbingu.
  that was very interesting and worked quite well
   
 13. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2013
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,082
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  lakini kwa hawa wenzetu ambao dini ndio inawaendesha baada ya wao kuiendesha dini, ni sawa na karl marx alivyosema kwao dini ni opium of mind. ni poisonous to development
   
 14. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,067
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135


  Muandishi wa thread hii unaonekana hujui unachokiongea ila una ungea tu kwa kua unamdomo.

  Wewe unamsiliza Vizuri Sheikh Ilunga, au unakurukupuka tu. Nyie ndio mawakala wa kanisa mnao waimimbisha watu wimbo wa amani na kudhulumu vizazi vyao.

  Wewe unajua historia gani ya nchi hii. Unajua kua Nyerere ndio alieleta Uhuru sio. Hiyo ni historia ya kanisa. Nyerere na John Rupia walitwa na wazee wa kiiislamu ili kukipa chama sura ya utaifa tu. Haya tumesha yaongea saana. Wewe kumbe ndio usiejua historia ya nchi hii.

  Hebu tutajie Askofu au Padre hata mmoja alieshiriki kudai uhuru wa nchi hii? Je kwanini historia ilioandikwa imeficha majina ya mashujaa wa majimaji walio nyongwa na wajerumani. Kwanini inataja majina moja moja. Je wewe unajua jina la kwanza la kinjeketile kiongozi wa vita ya MAJI MAJI. Hiyo ndio historia unayo ipigania ifundishwe. Je unajua mchango wa Sheikh Selemani Takadiri katika historia ya nchii?. Unajua kwanini Nyerere alilia kwenye kikao, kwa maneno ya Sheikh Selemani Takadiri?. Je unajua salamu za wanatanu walizokua wanasalimiana wanapokutana kabla ya salamu ya zidumu fikra sahii za mwekiti wa chama?.

  Wewe unajua Historia gani?

  USALITI WA NYERERE KATIKA NCHI HII KWA WAISLAMU, NI SAWA NA USALITI WA MKE WAKO ANAPOKUTILIA SUMU KWENYWE CHAKULA. SIO KAMA ALIKUA MJANJA AU SHUJAA. NI HUJUMA ZA KUAMINIWA.

  UVUMILIVU WA WAISLAMU NDIO ULIOLIFIKISHA TAIFA HAPA TULIPO. HAYO YA MTWARA YANA MIZIZI YAKE.

  AMANI HUONDOKA PALE WANAO DHULUMIWA WANAPOKATAA KUENDELEA KUDHULUMIWA. SASA MSIROPOKE NA KUJIDAI KUANDIKA MAKALA ZA KUIMBA AMANI NA KUWADANGANYA WATU.

  HII MBEGU YA UDINI ILIPANDWA NA NYERERE KWA MASLAHI YA KANISA DHIDI YA WAISLAMU. ref. SIASA YA TANZANIA NA KANISA KATOLIKI by DR. JOHN C. SIVALON.

  UACHE KUONGEA MAPUMBA YAKO HAPA, SISI TUNAONGEA KITU AMBACHO KIPO.
   
 15. paul buswelu

  paul buswelu Member

  #15
  Feb 20, 2013
  Joined: Dec 14, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Usimlaumu alieandika,jilaumu wewe kwa kauli zako,inaonekana wewe unaudini na wewe kama vile mchinjaji
   
 16. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,099
  Likes Received: 3,326
  Trophy Points: 280
  Mitazamo ni mizuri, je kwa sasa wangapi wanaijua historia ya nchi hii? kila dini ina nafasi yake katika historia hasa katika kipindi cha ukombozi uhuru, tunapaswa kujua historia ilivyo siyo hii tunayofundishwa yenye kuanzia mwaka TANU....
   
 17. v

  victor kilauo Member

  #17
  Feb 20, 2013
  Joined: Nov 9, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli nimeamini CCM ni kiboko! Imetufikisha hapa tulipo! Imepandikiza udini ili akili zetu ziishie kujadili yanayohusu dini na kuacha kuangalia wanavyotafuna nchi. Mtu wa kawaida ukitaka kumtoa kwenye truck anzisha jambo ambalo litamfanya awe bussy! Sasa hivi tumeletewa elimu za kichina kama tunavyosema bidhaa dhaifu zinazotoka china na ndo maana tunashuhudia 60% ya vijana wanapata zeo! Hii inatokana na kutowajali walimu katika maslahi yao.

  Badala ya kujadili mambo haya, tayari tunaumiza vichwa na mapandikizi yanyohujumu uhai wa watu ilimradi wakidhi matakwa yao ya utawala! Unaweza kuamini kweli nchi inayotawaliwa kisheria yenye Jeshi la Wananchi, Makachero kila kona, Jeshi la Polisi, Magereza na taasisi zote za ulinzi na usalama mambo kama haya yanatokea na wahusika hawakamatwi kama hakuna mkono wa wakubwa? Ili kutufanya tusiangalie tena masuala ya msingi, hili sasa linakuwa gumzo kuangalia ni nani anayejua Qurani au Biblia na historia isiyoleta tija! Hebu tuangalie kwa undani kuhusu mambo ya msingi yanayoliandama taifa kwa sasa! Mikataba mibovu, Elimu isiyokidhi matarajio ya Watanzania, Huduma za msingi kama maji safi, ajira, mikataba yenye tija kwa taifa,mitaji kwa wajasiriamali wadogo, kati na wakubwa na mambo kama hayo!
   
 18. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2013
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  1.Ni ngumu sana kujisomea kwa kizazi hiki ukizingatia elimu ilivyoshuka kiasi kwamba watu wanaingia form 1 bila hata kujua kusoma.
  2. Historia mashuleni kwenyewe walimu mgomo wanafunzi wenyewe wanaufaulu wa f mashuleni hiyo historia wanailewa vizuri, na kwa matokeo haya ya ufaulu 5% tutegemee mengi zaidi.
  3. Uongozi umejaa ubinafsi, ufiadi na unafiki wa hali ya juu!

  So nchi imetengeneza mabom ya kulipuka lipuka bila mpango
   
 19. salimkabora

  salimkabora JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2013
  Joined: Nov 10, 2012
  Messages: 2,458
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli hili ndilo kubwa zaidi. Tatizo hapa ni njaa ingawa pia ukosefu wa elimu huria na ya kidini vinachangia lakini michango hiyo inakuja katika sura ya njaa. Hebu leo hii mchukue mtu kama P.o.n.d.a Umpatie unaibu waziri au mwenyekiti wa lijitume lenye ulaji mkubwa kama utamsikia katika hizo harakati zake chafu. Ufisadi na uongozi m-bovu umeibua njaa katikati ya mamilioni ya wananchi na kujenga chuki kwanini wachache wanafaidi wakati wengine hawana kitu. Pamoja na sababu nzuri za mtoa hoja tuunganishe na hili tupate kitu kizima.
   
 20. dist111

  dist111 JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2013
  Joined: Nov 29, 2012
  Messages: 2,914
  Likes Received: 1,244
  Trophy Points: 280
  Umeongea vizuri sana, ila binafsi siamini kuwa WaTz ni wadini, ila naamini kuna watu wanachochea hili jambo kwa manufaa yao (NB: ndio sekta pekee ambayo inaweza sababisha kutoelewana kwa WaTz) na WaTz tusipokuwa makini lengo lao litatimia
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...