Mtatiro: OCD ameagizwa na ngazi za juu tupatanishwe na Mungiki

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
OCD na OCCID wa Magomeni, wameelekezwa na mamlaka za juu (zisizotajwa) ati wawaite viongozi wa CUF (waliovamiwa jana na kundi la Mungiki la Lipumba), pamoja na Wavamizi (Lipumba na wenzake) ati OCD na OCCID wawapatanishe viongozi wa makundi hayo.

Baada ya maelekezo hayo, OCCID amewasiliana na viongozi waliovamiwa jana na MUNGIKI kuwaomba eti wakutanishwe na wavamiaji ili waombane radhi!

Yaani, wale wavamizi waliokuwa na bastola, mapanga, nondo na waya za umeme waliovamia mkutano wa jana na kuwapiga viongozi wa CUF na Waandishi wa Habari, eti majambazi hayo yapatanishwe na upande uliovamiwa (chama). Na wapatanishi ni POLISI.

This is so low and very stupid. Watu wamevamia mkutano halali kabisa wa chama, baada ya kuumiza watu na kuwatisha, wakakimbilia kwenye magari na kutokomea, eti watu hao sasa ni lulu na polisi inawalinda kweli kweli, hawagusiki!

Sasa mimi nawaambia POLISI, hebu wawasake wale Majambazi walioua POLISI wetu wasio na hatia kule Kibiti, wakishawapata majambazi hao, wapatane nao. I mean kwamba, POLISI wakapatane kwanza na wale majambazi waliotuulia vijana nane, ndipo waje kupatanisha haya majambazi ya jana VS Viongozi waliovamiwa/Waandishi wa Habari!

POLISI wameelekezwa wasimpeleke mahakamani Jambazi huyo alokamatwa na wameelekezwa wapotezee ile BASTOLA iliyooneshwa na yule Usalama wa Taifa aliyetumwa kuungana na MUNGIKI kufanya shambulio la jana.

Baada ya kujua njama zote hizi chama chetu kinajizatiti kuchukua hatua. Tunataka kuona Majambazi haya wanafikishwa mahakamani haraka na yaeleze ile Bastola ilikuwa ya nani? Hatuwezi kuwa na mazungumzo na watu wanaovaa kininja, wakipiga na kuumiza raia wasio na hatia.

Kama POLISI hawachukui hatua wanachofanya ni kuacha mambo haya yaendelee ili watu waanze kuuana, vifo vikishatokea eti ndiyo watasema kuna JINAI zimetokea. Sisi tunatimiza wajibu wetu. Shameful indeed!

JSM.
 
Huu upuuzi unafanyika Tanzania tuu.
Yaani, wale wavamizi waliokuwa na bastola, mapanga, nondo na waya za umeme waliovamia mkutano wa jana na kuwapiga viongozi wa CUF na Waandishi wa Habari, eti majambazi hayo yapatanishwe na upande uliovamiwa (chama). Na wapatanishi ni POLISI.
 
Siasa bana malalamiko mwanzo mwisho. Mnazisingizia tu mamlaka ya juu ukweli halisi mnaujua wenyewe.
Mimi siku zote huwa nasema ukweli kwa ule uhuni ambayo waandishi wa habari walifanyiwa jana namshukuru Mungu sikuwepo kwenye Press Conference ila 99% mamlaka za juu wanahusika na lile tukio la jana. Wanafahamu ukweli
 
Shuleni kwetu kulikuwa na mwanafunzi akichapwa sana na walimu, mwisho alikuja kuwa sugu na zile bakora hakuziogopa tena. Ndipo alipoanza kupigana na walimu baada ya kuona anaonewa sana, Na walimu kusahau kazi yao ya kusomesha na kuelimisha kama walimu na sio waonevu.
 
Lakini mtatiro nahisa nimjinga flani hivi leo asubuhi amekuja mdomo mrefu kama chupa akiwataja usalama wa taifa kuwa ndiyo wamevamia haya sasa na jambo jipya anasema mungiki wa lipumba huyu jamaa mjinga sana ajifunze kupata ukweli kabla ya kuinua mdomo anakurupuka sana,kesho anaweza kuja na jambo jipya tena.
 
FB_IMG_1492969316063.jpg
Basi na ndugu zetu walioko segerea kwa kesi za kuiba kuku,tuko tayari kupatanishwa na walioibiwa turudishe kuku

Kimsingi kesi ya jinai haina upatanishi,tena inahusisha silaha kama mapanga na bastola,ni kesi ya kutishia kuua, ni kosa kubwa sana liko chini kidogo ya Murder case na linatakiwa kushughulikiwa na Afisa Mwenye Cheo,kwanza wajue bastola ni ya nani,na je matumizi aliyoifanyia ni sahihi? Kama sio hatua za kumnyanganya zifatwe,pia yale mapanga yalitoka wapi?nani kawatuma?
 
mimi naina mambo kama haya ndio yanayosaba isha bunge letu liache kujadili mambo ya maendeleo na kujadili mambo kama haya kwa sababu tungevia hia huru vyombo vyetu vya dola vishughulike kwa munibu wa sheria badala ya kuvipangia
 
Lakini mtatiro nahisa nimjinga flani hivi leo asubuhi amekuja mdomo mrefu kama chupa akiwataja usalama wa taifa kuwa ndiyo wamevamia haya sasa na jambo jipya anasema mungiki wa lipumba huyu jamaa mjinga sana ajifunze kupata ukweli kabla ya kuinua mdomo anakurupuka sana,kesho anaweza kuja na jambo jipya tena.
Sababu ya Mtatiro kuwashutumu Usalama wa taifa kutokana vitendo vya Mungiki wa Lipumba wanatumiwa na serikali ya ccm. Leo itokezee kikundi chochote kivamie mkutano wa ccm utaona usalama wa taifa na polisi itakavyofanya kazi ya kuwatafuta wavamizi. Lakini cha kushangaza magari,silaha na mmoja wa wavamizi ushahidi wote upo wazi, Polisi hawajatoa taarifa wala kuwafikisha kituo cha polisi washutumiwa. Hii inaonesha serikali inahusika(ina baraka zake) na mambo mengi ya hujuma za serikali kwa raia wake lazima usalama wa taifa itumie mbinu zake kufanikisha hujuma. Ndio maana Mtatiro akasema usalama wa taifa wanahusika, haiwezekani kundi lishambulie waandishi wa habari na mkutano bila ya kukamatwa na vyombo vya sheria.
 
Lakini mtatiro nahisa nimjinga flani hivi leo asubuhi amekuja mdomo mrefu kama chupa akiwataja usalama wa taifa kuwa ndiyo wamevamia haya sasa na jambo jipya anasema mungiki wa lipumba huyu jamaa mjinga sana ajifunze kupata ukweli kabla ya kuinua mdomo anakurupuka sana,kesho anaweza kuja na jambo jipya tena.
Angalia ulichoandika kisijekuwa ni vice versa kwako. Maana kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
OCD na OCCID wa Magomeni, wameelekezwa na mamlaka za juu (zisizotajwa) ati wawaite viongozi wa CUF (waliovamiwa jana na kundi la Mungiki la Lipumba), pamoja na Wavamizi (Lipumba na wenzake) ati OCD na OCCID wawapatanishe viongozi wa makundi hayo.

Baada ya maelekezo hayo, OCCID amewasiliana na viongozi waliovamiwa jana na MUNGIKI kuwaomba eti wakutanishwe na wavamiaji ili waombane radhi!

Yaani, wale wavamizi waliokuwa na bastola, mapanga, nondo na waya za umeme waliovamia mkutano wa jana na kuwapiga viongozi wa CUF na Waandishi wa Habari, eti majambazi hayo yapatanishwe na upande uliovamiwa (chama). Na wapatanishi ni POLISI.

This is so low and very stupid. Watu wamevamia mkutano halali kabisa wa chama, baada ya kuumiza watu na kuwatisha, wakakimbilia kwenye magari na kutokomea, eti watu hao sasa ni lulu na polisi inawalinda kweli kweli, hawagusiki!

Sasa mimi nawaambia POLISI, hebu wawasake wale Majambazi walioua POLISI wetu wasio na hatia kule Kibiti, wakishawapata majambazi hao, wapatane nao. I mean kwamba, POLISI wakapatane kwanza na wale majambazi waliotuulia vijana nane, ndipo waje kupatanisha haya majambazi ya jana VS Viongozi waliovamiwa/Waandishi wa Habari!

POLISI wameelekezwa wasimpeleke mahakamani Jambazi huyo alokamatwa na wameelekezwa wapotezee ile BASTOLA iliyooneshwa na yule Usalama wa Taifa aliyetumwa kuungana na MUNGIKI kufanya shambulio la jana.

Baada ya kujua njama zote hizi chama chetu kinajizatiti kuchukua hatua. Tunataka kuona Majambazi haya wanafikishwa mahakamani haraka na yaeleze ile Bastola ilikuwa ya nani? Hatuwezi kuwa na mazungumzo na watu wanaovaa kininja, wakipiga na kuumiza raia wasio na hatia.

Kama POLISI hawachukui hatua wanachofanya ni kuacha mambo haya yaendelee ili watu waanze kuuana, vifo vikishatokea eti ndiyo watasema kuna JINAI zimetokea. Sisi tunatimiza wajibu wetu. Shameful indeed!

JSM.

!
!
wananchi waliomkamata yule mmoja hawakumtendea haki yule waliyemvunja mguu na kumgusagusa. Wangeonesha kwamba wao ni wale wenye hasira kali kwelikweli
 
Lakini mtatiro nahisa nimjinga flani hivi leo asubuhi amekuja mdomo mrefu kama chupa akiwataja usalama wa taifa kuwa ndiyo wamevamia haya sasa na jambo jipya anasema mungiki wa lipumba huyu jamaa mjinga sana ajifunze kupata ukweli kabla ya kuinua mdomo anakurupuka sana,kesho anaweza kuja na jambo jipya tena.
Aise sijawahi Kuona mtu hajitambui kama huyu jamaa yeye litakalo kuja mdomoni tu anaonge
 
Back
Top Bottom