Mtatiro: Mikutano ya Rais yote ni LIVE ila bunge wananchi wafanye kazi wanapoteza mda

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Mkutano mkuu wa CCM.

Ziara za 'mheshimiwa-mtukufu', akiwa Kahama, Singida, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Maswa, maadhimisho ya mapinduzi kule Zanzibar.

Kuzindua mwendokasi, maadhimisho ya siku ya Uhuru, sherehe za muungano, maadhimisho siku ya wafanyakazi, YOTE HAYO, YAMEONESHWA MUBASHARA (LIVE).

Kumbe sasa tatizo la kutokuonesha 'Bunge-Live' siyo ukosefu wa pesa (kama tulivyodanganywa awali).., lakini ni vipaumbele vya nani na kipi kionekane kwa sababu zipi., AU bado sababu ni 'Muda-wa-kufanya-kazi'!? Kwani wakati tunatazama hizo ziara na huo mkutano mkuu.., kazi zinakuwa zimesimama wakati huo.., endeleeni kuchezesha antena tu, maana aliyeturoga inaonekana hakuwa timamu!

Martin Maranja Masese Copyright.
 
Hata bunge pia huwa LIVE, isipokuwa ushabiki wetu tunaona kuwa Ile LIVE sio yenyewe

Ziara zinazoonyeshwa LIVE ukuangalia vizuri muda utaona ni wastani WA nusu saa Mpaka lisaa limoja na nusu

Na sio LIVE SIKU NZIMA KAMA TUNAVYOTAKA, kitu ambacho hakifanyiki duniani kote (hasa Kwenye jumuiya ya madola)

Bunge huwa LIVE Kwa vipindi Fulani, kisha linaendelea kurekodiwa Kwa vipindi vilivyobaki, hata Ziara na Kazi Zach raisi si zote huwa Live Bali chache
 
Na cku zote serikali ya awamu ya tano haitaki kabisa kuambiwa ukwelj na ndo maana wanawakamata watu bila hatia na kwa kisingizio cha uchochezi. Na police nao imekuepo kwa ajili ya wana ccm na serikali yao. Kipindi kile cha uchaguzi wa rais wabunge na madiwani. Sisi huku kwetu tulipata shidah sana. Nakumbuka wakati watu wanasherehekea ushindi wa mbunge wetu wa upinzan tulikiona cha moto. Lakin ushindi wa rais wenzetu walitesa sana tena na police wanafata nyuma nao wakisheherekea kwa pamoja bila matatizo yyte wakuna mabomu walanini. Huu ni upendeleo wa hali ya juu sana na ni ubaguzi usiokibalika. Nchi yetu sote hii why tunyanyasane?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si ndio maajabu anaenda na msaafara magari elfu moja wananchi wanaamrishwa wamgojee masaa nane a kisha jinadi maana anafanya kampeni akimaliza kampeni zake anawaacha wananchi na maneno ya kuwa uudhi kuwa kati sha tamaa na bei za chumvi kiberiti mafuta ya taa be tri za tochi sukari juu wenyeviti wa vijiji wana pora kuku wa wananchi na mbuzi wa wananchi eti wanamkarimu raisi hivyo anawaongezea umaskini
 
Mbaya zaidi ni huyu rais mwenye laana asiyenafaida alafu anajiweka live............xxiiuuuuuuu
 
Kipindi kile bunge live lilikatazwa alafu wakaweka live msiba wa sitta NILIFURA KWA HASIRAA!!!!
 
Hata bunge pia huwa LIVE, isipokuwa ushabiki wetu tunaona kuwa Ile LIVE sio yenyewe

Ziara zinazoonyeshwa LIVE ukuangalia vizuri muda utaona ni wastani WA nusu saa Mpaka lisaa limoja na nusu

Na sio LIVE SIKU NZIMA KAMA TUNAVYOTAKA, kitu ambacho hakifanyiki duniani kote (hasa Kwenye jumuiya ya madola)

Bunge huwa LIVE Kwa vipindi Fulani, kisha linaendelea kurekodiwa Kwa vipindi vilivyobaki, hata Ziara na Kazi Zach raisi si zote huwa Live Bali chache
....Nonsense

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu wa Israel sasa imetosha! Tutolee hili kituko tunataka kiongozi mwenye busara kuongoza nchi! Toa kituko hiki!!
 
Ndio maana Tundu Lissu akamwaga ukweli kwa tabia hiyo ya hila na ubaguzi.
Matokeo yake baada ya kuutoa huo ukweli mchungu Lissu ameitwa mchochezi!

Lakini serikali hii ilivyo na mazingaombwe, mtu inayemtuhumu kuwa mchochezi badala ya Polisi kuelezea uchochezi wake ni upi wao wanaenda kumpima mkojo, hivi Lissu alitamka hayo maneno kupitia 'mkojo' wake na hakutamka hayo maneno kwa mdomo wake!?
 
Mkuu ndiyo huu udikteta uchwara ambao ni lazima tuupazie sauti popote pale tulipo ili ukomeshwe kabisa. Katiba na sheria za nchi ni lazima ziheshimiwe na wote. Hakuna aliye juu ya katiba ambaye anastahili kuzuia haki za raia na vyama vya upinzani nchini ambazo zimo ndani ya katiba na sheria za nchi kwa woga wake wa kuogopa maovu yake mbali mbali au ya ndani ya chama chake kuwekwa hadharani.

[HASHTAG]#lissuthegreat2020[/HASHTAG]

Salama waheshimiwa wananchi!
Kiukweli mimi binafsi naishangaa serikali ya awamu ya 5 kwa kuwafanya wananchi kama 'wajinga' 'malofa' na 'wapumbafu'.

Tunamwona Magufuli ziara zake zote yuko live TBC na hapa ninapoandika makala hii ni kwamba TBC imelazimika kukata matangazo mengine kama vile ya dini ili kuonesha ziara ya rais live.

Ripoti mbili za makinikia zilisomwa live huku bunge likiendelea.

Kinachonishangaza:

1. Tunaambiwa bunge live ni gharama na itawafanya wananchi wasifanye kazi, lakin ziara ya rais kuwa live siyo gharama na wala haiwafanyi wananch wasifanye kazi.

2. Vyama vya siasa visifanye mikutano ya siasa wananchi wafanye kazi ila chama tawala kinazunguka nchi nzima kinapga siasa kikisaidiwa na siasa za Rais

Je, huu ni uungwana au ndo ubaguzi ulioelezwa na Lisu?
Tujibu kwa hoja...
 
Bunge mipasho, bora Rais Magufuli afungue miradi ya maendeleo ya wananchi waliompigia kura

Sent using Jamii Forums mobile app
Isipokuwa Magu kumuita mbunge wa Chadema kuwa hako kabunge ka upinzani ka Chadema siyo mipasho!?

Hakika TZ tunakwenda kubaya, kwa kuwa ukifanya comparison ya yale yaliyotamkwa na wabunge Lema, Halima Mdee na haya yaliyotamkwa na Lissu na hayo yanayotamkwa na Presidaa wetu kila siku, nadiriki kusema mchochezi wetu namba moja hapa nchini anayeleta ubaguzi wa hali ya juu na ambaye anaonyesha nia ya kutaka kutuvurugia Umoja wetu ambao nchi hii imeulea kwa miaka mingi ni Magu mwenyewe!

Penye ukweli lazima usemwe, hata kama hayo magereza yataendelea kujengwa ili kuwarundika huko maelfu kwa maelfu ya sisi waTZ ambao tutaitwa wachochezi eti tu kwa sababu tunamkosoa Rais wetu, wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18(1) inatamka wazi kuwa kila mwananchi yuko huru kutoa maoni yake na hakuna chombo chochote kinachopaswa kuingilia maoni hayo ya hao wananchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom