Mtatiro: Mambo matano mazuri ya Magufuli akiwa rais

duh walikuwa wanatuimbia kuwa CCM ni ile ile.....sasa sijui hiyo mihemko inatoka wapi ya kufanya magufuli aibadili ccm hii iliyochoka ambayo imemlea na kumpa ukuu huu fake na bajeti wameipitisha ambayo maendeleo ni tirion 5 matumizi ni 17 tirion....

Nawashangaa hii ccm imetoka wapi mpya aliyokuja nayo magufuli na hali wanasema ccm ni ile ile! Itakuwa ile ile ya tumaini jipya,chaguo la Mungu,maisha bora kwa kila mtanzania nk.

Tukichagua hovyo tutalia hovyo na maisha ni yale magumu na michango kede kede ya maendeleo mnasahau kuwa mnachangia maendeleo yenu kupitia kodi. Poleni Watanzania na shetani ccm ila MUNGU yupo nasi atatufungua akili dhidi ya ccm....AMEEN
 
Kushinda okey, kwamba atatufikisha Wtz tunakohitaji kufika?! Nina mashaka makubwa! Divai mpya ktk viliba vikukuu! Si hawa ccm waliopitisha miswaada mitatu ya gas na petrol kwa hati ya dharura ikiwa haina nia njema na Wtz!? Si hawa hawa ccm waliokataa Maoni ya wtz ktk rasimu ya katiba ya Jaji Warioba?! Sasa niambie tunachofurahia nini!? Chama na watu ni walewale! Mimi sina uhakika na tunakoelekea bali matumaini!
 
Binafsi nilikua mfuatiliaji wa makala za Mtatiro kwenye gazeti la mwananchi akiwachambua wagombea wa ccm na upinzani kwa nafasi ya uraisi na nilizikubali.
Kwa hii post naona ni muendelezo wa makala hizo hivyo sio sahihi kumnyooshea kidole kwamba ni njaa au anajipendekeza kwa Magufuli isipokua kitendo cha kuandika upande chanya tu bila hasi wakati alishaahidi kuandika pande zote inaleta wasiwasi kidogo. Namshauri kama amepitiwa basi aedit hii post ili aondoe huu ukakasi unaoonekana.

Mkuu Post Imechukuliwa Toka Gazeti La Mwananchi Na Ameeleza Kuwa Leo Ni Upande Chanya Na Hasi Ataleta Sku Nyingine.
 
mtatiro tunakushukuru kwa uchambuzi wake na liwe fundisho kwa wachambuzi na waandishi wengine ambao bado sio wazarendo katika kutafuta kiongozi sahihi kwa taifa letu,magufuli ni jembe letu huku kwetu vijijini tunasema tutalipa kwa kadi zetu za kura kwa yale uliyotutumikia,
 
hasiye mkubali magufuli ,anaweza kuwa na tabia na sifa zifuatazo
1,mvivu
2,mzembe
3,asiyejua aina ya kiongozi tunaemtaka kwa sasa
4,mwenye element za wizi na kupenda urafiki kazini
5,asiyejua taifa linatakiwa kwenda wapi
6,anayeendekeza siasa na polojo za majukwaani za wanasiasa pasipo kumpima kiongozi wa yale aliyoyafanya na kuwatumikia watanzania masikini .
 
Mkuu Ukwaju hiyo No #3 ya kwamba afufue reli ili kuua biashara ya malori nadhani ndipo hasa pakumpimia mwanzo mwanzo mwa uongozi wake kama akiwa rais.coz akipigia sana kelele hili suala kwamba malori yanaharibu sana barabara sasa ndo tutajua ilikuwa siasa au alimaanisha.
Hapo upo sahihi kabisa na watu wangegundua mapema wangemsaidia Magufuli ka hali na mali kuliko kimtenga na kum-feedback
Mfano Katibu wa wenye Malori ni mtoto wa Best wa Lowassa bado kuna malori yanasomba mazao na mizigo huko Arusha kwa kina Mollel napo ana mkono wake
Kwa vile pana moto na hawaingiliki ili kuokoa maisha yake, ajenge Reli tu na haata huko kaskazini lazima ataiokoa TZ
 
hasiye mkubali magufuli ,anaweza kuwa na tabia na sifa zifuatazo
1,mvivu
2,mzembe
3,asiyejua aina ya kiongozi tunaemtaka kwa sasa
4,mwenye element za wizi na kupenda urafiki kazini
5,asiyejua taifa linatakiwa kwenda wapi
6,anayeendekeza siasa na polojo za majukwaani za wanasiasa pasipo kumpima kiongozi wa yale aliyoyafanya na kuwatumikia watanzania masikini .
Cc Dr.W.Slaa John Mnyika Tundu Lissu
 
Last edited by a moderator:
View attachment 267742

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Dk John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais wa chama hicho kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Kwanza kabisa napenda kumpongeza sana Magufuli kwa hatua aliyofikia na kumtakia kila la heri. Naomba kukiri kwa uwazi kwamba katika uchaguzi unaohusisha vyama vya siasa ni lazima mshindi atapatikana na kwa Tanzania ni lazima mshindi huyo atoke kwenye chama cha siasa.

Tanzania ina vyama 22 vilivyosajiliwa na vinavyofanya kazi sasa, tutake tusitake ni lazima rais wa nchi atatoka katika chama kimojawapo, na kwa sababu CCM imeshapitisha mgombea wake na yeye ana fursa ya kushinda uchaguzi kama ambavyo fursa hiyo ilivyo kwenye vyama vingine. Natumia nafasi hii kufanya uchambuzi wa dhati juu ya taswira ya serikali ya Magufuli ikiwa atafanikiwa kushinda uchaguzi wa mwaka huu. Taswira ya namna hii pia nitaifanya kwa wagombea wengine wa vyama ambavyo vitaamua kuweka wagombea urais.

Katika kulifanya jukumu hili nitachambua masuala 10 ambayo nafikiri kwamba yanaweza kujenga utawala wa Magufuli, ikiwa atachaguliwa na Watanzania kuwa rais wa awamu ijayo.

Mambo matano kati ya hayo nayatazama kama taswira bora na mengine matano yanaweza kuwa taswira hasi. Katika uchambuzi wa leo nitaanza na mambo matano ambayo ni taswira bora.

Usimamizi bora

Taswira ya kwanza ambayo Magufuli anaweza kuirejesha bila wasiwasi ni usimamizi thabiti wa serikali na nidhamu ya utendaji ndani ya serikali. Naamini kuwa serikali ya Magufuli itakuwa ya kiusimamizi na yeye mwenyewe anaweza kulifanya jambo hilo bila kusita. Katika nyadhifa nyingi alizopitia hadi sasa ameijenga taswira hii kila alikopita na bado inambeba hata ikitokea anachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano.

Tukumbuke kuwa moja ya mambo ambayo yameanguka kabisa nchini hivi ni utendaji ndani ya serikali. Tunafahamu kuwa wafanyakazi ndani ya serikali ukiachilia mbali matatizo waliyonayo kwa maana ya vipato, hata mambo madogo ambayo wangeweza kuyasimamia ndani ya dakika au saa chache huchukua wiki kadhaa na hata miezi kadhaa. Utaratibu wa utoaji huduma umekwama sana na nadhani kama akiwa na uwezo huo atafanikiwa kutatua changamoto kubwa na ya siku nyingi. Ikiwa utendaji wa serikali unaimarika na huduma zinatolewa kwa wakati, tutaweza kujenga taifa linalokwenda mbele bila kujali chama gani kiko madarakani.

Msimamo imara

Taswira bora ya pili ya serikali ya Magufuli inaweza kuwa ni misimamo katika masuala ya msingi na kutoyumba sana. Magufuli muda wote ambao amekuwa kiongozi ameonyesha jambo hilo. Kila mara amekuwa na misimamo hata kama siyo sahihi. Kwa tafsiri nyingine hii huwa ni njia bora ya uongozi wa nchi japokuwa misimamo ya serikali au kiongozi mkuu wa serikali huwa haipaswi kuwa juu ya haki na matakwa ya wananchi.

Moja ya mambo ambayo serikali iliyopita ilikosa, ni pamoja na kukosa misimamo na kuwa na “double standard”. Mfano mdogo tu ni kwenye mchakato wa katiba mpya ambapo Rais anayeondoka alisimamia uanzishwaji bora wa mchakato huo, akaunga mkono katika hatua zote na rasimu zote, lakini akaja kuwageuka wajumbe wa tume hiyo na rasimu yao ya pili alipolihutubia Bunge Maalumu la Katiba. Naamini Magufuli si mtu wa kugeuka na kuna masuala mengi anaweza kuyasimamia kwa dhati na kila mmoja wetu akakubali kuwa, naam! Hapa kuna kiongozi anasimamia masuala haya.

Uwezo wa kusimamia miradi


Taswira ya tatu ya serikali inayoweza kuundwa na Magufuli ikiwa atachaguliwa kuwa rais ni uwezo wa kusimamia miradi ya maendeleo. Magufuli ni mtu wa namna hiyo na ametuonyesha katika sekta ya ujenzi na hasa katika eneo la barabara. Moja ya masuala ambayo nayaona kama mafanikio makubwa ya serikali ya Kikwete ni ujenzi wa barabara, ukiniuliza, nitakwambia jambo hili ndilo Kikwete anapaswa kujivunia atakaporudi nyumbani kwake pale ‘Msoga’. Lakini aliyeleta mapinduzi hayo kiusimamizi ni Magufuli.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa “ikitolewa tenda ya ujenzi wa barabara nchini Tanzania na India halafu nchi zote zikakabidhi tenda hizo kwa watoto wa marais wa nchi, kule India walau barabara ya ‘kudanganyishia’ itajengwa lakini hapa Tanzania unaweza usione hata kokoto” (tafsiri yangu). Dhana hiyo ina maana kwamba huku kwetu wizi na kujijazia manoti ndivyo vitu vinavyoshamiri na kwa tafsiri ya Mwalimu “ilipasa Magufuli awe anaongoza kwa kuchukua noti za barabara na kuzijaza tumboni kwake”, jambo ambalo limekuwa nadra kutokea na kama liliwahi kuwepo ndiyo tutajua sasa wakati watu wataanza kutoa taarifa zake kwa sababu anataka kwenda Ikulu. Kwa uwezo huu wa kiusimamizi namuona Magufuli akisimamia miradi ya serikali kwa ustadi mkubwa hata kama siyo “waziri wa miradi” katika serikali atakayoiunda.

Mawaziri imara

Taswira ya nne nayoiona katika serikali ya Magufuli ikitokea anashinda urais wa Tanzania ni uundaji wa Baraza la Mawaziri na nyadhifa za kiutendaji zilizojaa watu wenye uwezo kuliko marafiki. Serikali zetu kadhaa zilizopita ikiwamo hii inayoondoka zimekuwa na sifa ya kubeba marafiki kufa au kupona. Siyo siri kwa JK amelalamikiwa mno na mara kadhaa serikali yake ilionekana kama “imejaa washkaji” watu wanaolindana na kuoneana haya kwa heshima za urafiki kuliko kuangalia maslahi ya nchi.

Magufuli anaweza kuwa dawa ya serikali za ushkaji kwani tangu kwenye mchakato wa kupata wagombea ndani ya CCM hakuonekana kama “kitisho” na hakuwa na makundi nyuma yake, penyeza yake ya kimya kimya hadi anakuwa mgombea urais wa CCM imemsaidia kuanza kujenga marafiki wasio na masharti ya kutaka kubebwa naye. Marais wengi huunda mitandao na mitandao hiyo huwapa fedha mapema na huwasaidia kila jambo, wanapofika madarakani huwa na deni la kuilipa mitandao hiyo, malipo yenyewe ni miradi ya serikali, tenda mbalimbali na vyeo lukuki. Naamini Magufuli hatakuwa na tatizo hilo na itamsaidia kutengeneza serikali isiyo na “washkaji kibao.”

CCM yenye nguvu


Taswira ya tano inayoweza kujitokeza ni uwezekano wa kurejesha nguvu ya CCM ambayo inasambaratika, na naamini hili linaweza kujitokeza sana hasa kwenye kipindi cha kwanza cha uongozi wake. Siamini kama ataweza kurekebisha taswira ya CCM kwa miaka mitano mingine (ikiwa atapata vipindi vyote viwili) kwa sababu hatujaona utendaji halisi wa serikali ijayo, ikiwa CCM ndiyo itashinda. Wananchi wengi hawaiamini tena CCM na jambo hilo linaweza kuipeleka ikaangushwa katika uchaguzi wa mwaka huu, lakini ikitokea CCM inavuka kizingiti na inapona kuangushwa halafu Magufuli anakuwa rais, anaweza kujizatiti na akatumia miaka mitano kufanya mambo makubwa yatakayowafanya wananchi warudishe imani kwa chama hicho. Ila akifanya vibaya sana atazidi kuididimiza. Kwa mtazamo wangu wa msisitizo ni kwamba naona akifanikiwa kwenye eneo hili, japokuwa naweka msisitizo wa pili kuwa ni lazima tusubiri kujua ikiwa atashinda kipindi chake cha kwanza kitakuwaje kiuongozi.

Julius Mtatiro ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii. Ana shahada ya uzamili (M.A) na anahitimu shahada ya Sheria (LLB) Julai mwaka huu: +255787536759, juliusmtatiro@yahoo.com). Uchambuzi huu ni maoni yake binafsi.

Source: Mwananchi, July 13, 2015.


Hizi degree za madesa bwana shida sana.Huyu unaemsifia alikuwepo kwenye Bunge maalum la katiba na kwa kushirikiana na wezi wenzake walifinyanga maoni ya watanzania yaliyolenga kuweka misingi Imara ya kiungozi na kiutawala.sasa mtu Mwingine anaibuka na degree yake ya kudesa bila hata kufikiria kidogo tu anatoa uharo
 
Daima Magufuli ni Tingatinga. Atafanya mazuri
watanzania mpaka tuje tuelewe Kuwa ndani ya ccm hatuwezi kupata rais bora tutakuwa kaburini.angalia wale waliokuwa wananyoshewa vidole Kuwa ni wezi na mafisadi sasa si wezi Wala mafisadi tena,wamekuwa kitu kimoja na sisi kama mazuzu tunawasifu Kuwa wamemaliza tofauti zao vizuri na vyama vingine viige.kwani ni hatutaki kujiuliza hao wizi na wasafi wameungana pamoja kwa FAIDA ya nani?watanzania au chama chao?chama kwa wezi na wasafi hahahahahahaha!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
hasiye mkubali magufuli ,anaweza kuwa na tabia na sifa zifuatazo
1,mvivu
2,mzembe
3,asiyejua aina ya kiongozi tunaemtaka kwa sasa
4,mwenye element za wizi na kupenda urafiki kazini
5,asiyejua taifa linatakiwa kwenda wapi
6,anayeendekeza siasa na polojo za majukwaani za wanasiasa pasipo kumpima kiongozi wa yale aliyoyafanya na kuwatumikia watanzania masikini .
Mwezi wote nchi hii including Magufuli waliungana kuyakataa maoni ya wananchi katika rasim ya pili ya katiba mpya.maoni yaliyolenga kuweka mifumo(systems) za kupata kinyume cha haya uliyoorozesha Hapa.Watu masikini wa akili hutegemea zaidi watu badala ya mifumo (systems)pole
 
Daima Magufuli ni Tingatinga. Atafanya mazuri
wewe unashangaa tingatinga ?kuna watu waliitwa chaguo la Mungu but still wanapiga maendeleo kwa kuonesha foleni za barabarani na watu wanaopenda fastjet huku shirika Lao la umma likiwa na ndege moja yenye uwezo wa kubeba abiria 50 tu.Mungu atuhurumie tu
 
Back
Top Bottom