Mtatiro: Madaktari waliomwangukia JK ni wasanii

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
haya ndiyo maneno ya JULIUS MTATIRO wa CUF NGANGARI kuhusu ishu ya madokta na serikali ya JK
[h=5]
"Kwa mtizamo na uzoefu wangu, walikuwa wanatengeneza sinema, kwa vyovyote vile kama serikali ilivyowalipa usalama wa taifa na wahuni wam-mwakyembe DR. ULIMBOKA, ndivyo hivyo wamewalipa baadhi ya makada wa CCM ambao ni madaktari wanafunzi ili wajivishe vyeo vya uongo na ukweli ili kudanganya umma.

Najua wanatumikia matumbo yao masikini na wanajaribu kusaliti mapambano ya kudai haki zao wenyewe.

Wakati nikiwa naongoza vyuo vikuu Tanzania kama katibu mkuu, kuna wakati tuliongoza mgomo kudai mikopo iboreshwe nchi nzima, tukafukuzwa CHUO, wakati tuko majumbani, CCM ikawachukua makada wake wanafunzi na kumtumia kiongozi mmoja aliyetusaliti akatangaza ati KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU ANAMUOMBA RADHI RAIS WA NCHI......

Leo jamaa huyo amelipwa mshahara wa kutumia tumbo lake, amepewa ukuu wa wilaya na bwana mkubwa....matumbo yanaua fikra pevu za vijana, vijana wanakosa mwelekeo kabisa.

Na utakuta hawa madaktari wa jana ati wameahidiwa kupewa GX 100, kusomeshwa nje ya nchi, kupewa nyadhifa nzuri au utakuta wamepewa milioni mojamoja tu. Masikini wa mungu!

Bahati ya pekee iliyopo ni kuwa CCM haitawadanganya watanzania wote wakati wote."

source:eek:n his page ,facebook


[/h]
 
Ukweli umeishadhihirika. Walioomba msamaha ni wanafiki wachache waliotumiwa na magamba. Hizi ni enzi nyingine ndugu zanguni.
 
Hivi hawa walipoomba msamaha walitegemea nini?.. kwa sababu walijibiwa jibu lisilo rasmi kuwa "mwizi akikiri ni sheria kuchukua mkondo wake"

Sasa what is their next move?..maana sidhani kama watarudi tena hata kwa wale waliowasaliti!!
 
asigwa Sinema nafikiri ni muungano wa CCM and CUF kuwalagai watanzania
 
Last edited by a moderator:
wanatufanya wajinga, huyo dokta mwenyewe aliye kuwa anaomba msamaha anaonekana kabisa anaongea anajua laikuwa anaongaa upuuzi wa hali ya juu, basi wafunguliwe mashtaka ya kuuwa kwa kukusudia. Njaa mbaya sana.. na kusema tuna ahidi hatuta fanya mgomo tena hii ni kauli ya kipuuzi kupindukia. we've got a log way to go
 
Mtatiro chunga kauli zako wewe ni kiongozi kwenye jamii. Siasa za kiharakati za vyuoni usizihamishie kwenye hali halisi. Madaktari hawa wana akili zao timamu wametafakari kwa kina juu ya mgomo wao na kugundua kuwa wanaoathirika ni watanzania wenzao hivyo kwa busara wameamua kuomba radhi, tatizo liko wapi hapo?
 
Ukweli utaendelea kujulikana na kila mwenye akili anajua kinacho endelea.

Wameamua kutumika na ccm ili kupata ukuu wa wilaya baadaye.
 
Tanzania ni zaidi ya uijuavyo, "Tujenge hoja, tuelimishane, tusahishane, tukosoane, tukubaliane katika Ukweli kwa maslahi ya Taifa maana Ukweli ukiuzima ipo siku utajilipizia kisasi, mwisho tusameheane.
 
Mtatiro chunga kauli zako wewe ni kiongozi kwenye jamii. Siasa za kiharakati za vyuoni usizihamishie kwenye hali halisi. Madaktari hawa wana akili zao timamu wametafakari kwa kina juu ya mgomo wao na kugundua kuwa wanaoathirika ni watanzania wenzao hivyo kwa busara wameamua kuomba radhi, tatizo liko wapi hapo?
ACHA PUMBA HIZO!. KWANINI MTATIRO ASISEME UKWELI?.. Waliojitokeza awali ni vibaraka wa CCM, ndiyo maana viongozi wao walijitokeza jana na kukanusha!.. Ni busara gani kuyaacha madai ya msingi na kupiganiaha ujinga ili kuganga njaa?.. Watu wanalazwa chini, vifaa vya tiba duni na haba, viongozi wanatibiwa ulaya, madaktari wanadai maslahi bora, lakini cha ajabu wabunge wanaongezewa milioni 3.6 kwa wabunge 352. Je, ni kweli serikali haina hela kama si uhuni?.. Au na wewe ni mhuni mwenzao?
 
Mtatiro chunga kauli zako wewe ni kiongozi kwenye jamii. Siasa za kiharakati za vyuoni usizihamishie kwenye hali halisi. Madaktari hawa wana akili zao timamu wametafakari kwa kina juu ya mgomo wao na kugundua kuwa wanaoathirika ni watanzania wenzao hivyo kwa busara wameamua kuomba radhi, tatizo liko wapi hapo?
Wametafakari kwa kina juu ya njaa zao na kugundua kuwa wanahitaji kula kwa kuwasaliti wenzao, tatizo lipo kwenye usaliti.
 
Tunapitia kipindi kigumu lakini muhimu sana. ni wakati wa watu kuchagua ama kutumikia matumbo yao au kutumikia maslahi ya umma, maslahi ya walio wengi, ambao ni maskini na walalahoi. ni wakati wa kuchagua ama kuwa mtu usiye na falsafa yoyote katika maisha yako isipokuwa moja tu - kama kuchumia tumbo utaita ni falsafa. watu waliokamata rasilimali za nchi na waliopora mamlaka kutoka kwa wananchi wapo tayari kutumia mbinu zozote zile waendelee kustawi. kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingine atafikia wakati analazimika kutoa uamuzi: ashiriki rushwa, ufisadi, uporaji wa mali za walalahoi, na kujitajirisha yeye na jamaa zake, au aachane na vinono hivyo ashinde juani akipiga miayo lakini akilinda maslahi ya taifa. ni uamuzi mgumu lakini kila mmoja wetu kwa nafasi yake atatakiwa mara kwa mara kufanya maamuzi. maisha siyo rahisi kwa hao interns, lakini ndio mapambano yenyewe. it can be very grim and bloody. but we have to do it. wakati mwingine inawezekana kufanya utaratibu wa kusaidiana ili kupunguza ukali wa maisha, hasa kwa wale wanaokuwa wahanga wa mapambano. utengano wetu unatuumiza sisi wenyewe na kuchelewesha kutekeleza malengo yetu.

Malengo ya mgomo wa madaktari yanafahamika vizuri sana, na ni kwa manufaa ya kada nzima ya udaktari na sekta nzima ya afya. hivyo ni kwa manufaa ya taifa tena kwa muda mrefu ujao. kuyasaliti malengo hayo kwa ajili ya riziki ya muda mfupi, ni uasi.
 
Njaa mbaya sana nyambafu,yaani watu wazima wanatumika kama kondom bila kujijua,lakini waangalie historia ya magamba wanamtindo gani.
 
watakuwa wamelipwa na cashier ridhiwani..anatembea na fuko la pesa dogo..haya mambo ya mtoto wa rais kukwapua hazina ya taifa tunayasikiaga kwa madikteta wa africa magharibi..
 
Back
Top Bottom