Mtatiro: Hatua za Bunge, Lipumba na msimamo wangu! Na maajabu ya Bunge na serikali ya CCM

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana mbunge wa Singida Mashariki Mhe.Tundu Lissu, kinyume na maombi yaliyowekwa na mawakili wa Jamhuri ya kuzuia asipewe dhamana.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri amesema, baada ya kupitia hoja za serikali na majibu ya mawakili wa utetezi, haoni mantiki ya kuzuia dhamana kwa Lissu. Hivyo mahakama hiyo imemuachia Lissu kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.10 milioni, kila mmoja.!
 
Ala, mi nilifikiri ukishafungua shauri mahakamani ni lazima mahakama isitishe maamuzi ya pande zote mbili mpaka shauri la msingi la mlalamikaji litakapotolewa maamuzi.


Sasa haya mambo yanakuwaje ?
 
Wangeweza kubadili upepo na CUF ya Lipumba wangeanza kudefend hivyo kupoteza malengo na CUF ya Seif wakapanua wigo wa mapambano ie multiple lanes attack! Adui angechanganyikiwa na kuuawa at a peace meal!

If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat
No move hii ya Lipumba kuwatimua ni kujibu mapigo ya Oporesheni fagia Buguruni HUJAJUA HILO. YAANI Kamwahi adui yake kabla hajaanza mashambulizi pale aliposikia tangazo la mashambulizi. Hapa Lipumba kawa smart zaidi yao. Waliotangaza operesheni sijui kama walitegemea hili, UKIZINGATIA WANAJUA NGUVU YA CCM imelalia kwa Lipumba hapa walitakiwa wawe makini zaidi.
 
Aitwe na bunge kama nani ndani ya serikali au chama chake? Au kila anayesema maneno yasiyopendwa na bunge aitwe bungeni kuhojiwa?. Kama unataka kusema Mtatiro ni kiongozi wa Cuf umepotoka kwasababu huyo spika wako hamtambui kama kiongozi wa Cuf ila anamtambua Lipumba, ndio maana ametekeleza amri ya Lipumba bila kumsubiria Mtatiro ambaye ni kiongozi wa kamati ya uongozi ya Cuf kikatiba ila kiserikali hawamtambui.
Na mimi nasema ni maamuzi ya kihayawani kabisa na yanapaswa kulaaniwa na watu wenye kutumia akili tu, nasubiria kuitwa na bunge kuhojiwa.
Kwani akina Makonda waliitwa km nani? Tukana au kashfu bunge leo uone km hujaitwa. Hujui mipaka ya Bunge....ngoja wengine waeleweshe zaid

sweeper
 
Aitwe na bunge kama nani ndani ya serikali au chama chake? Au kila anayesema maneno yasiyopendwa na bunge aitwe bungeni kuhojiwa?. Kama unataka kusema Mtatiro ni kiongozi wa Cuf umepotoka kwasababu huyo spika wako hamtambui kama kiongozi wa Cuf ila anamtambua Lipumba, ndio maana ametekeleza amri ya Lipumba bila kumsubiria Mtatiro ambaye ni kiongozi wa kamati ya uongozi ya Cuf kikatiba ila kiserikali hawamtambui.
Na mimi nasema ni maamuzi ya kihayawani kabisa na yanapaswa kulaaniwa na watu wenye kutumia akili tu, nasubiria kuitwa na bunge kuhojiwa.
Kwani akina Makonda waliitwa km nani? Tukana au kashfu bunge leo uone km hujaitwa. Hujui mipaka ya Bunge....ngoja wengine waeleweshe zaid

sweeper
 
sasa hiyo New York ilikuwa kuwa na ulazima gani kuandikwa, au ndo mkurya kapanda ndege tenaa!
 
MWENDOKASI WA VI-WONDER TANZANIA!

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J,
#NYC_USA.

[HASHTAG]#Jumapili[/HASHTAG], Tarehe 23/07/2017, Saa 4 asubuhi - Kikao (Feki) cha Kamati ya Maadili ya Lipumba.

[HASHTAG]#Jumapili[/HASHTAG], Tarehe 23/07/2017 (siku hiyo hiyo), Saa 8. Mchana - Baraza Kuu (Feki) la Lipumba.

[HASHTAG]#Jumatatu[/HASHTAG], Tarehe 24/07/2017 asubuhi -
Barua ya Msaliti Lipumba kwenda kwa Spika wa Bunge.

[HASHTAG]#Jumanne[/HASHTAG], Tarehe 25/07/2017 - Ofisi ya Spika yakiri kupokea Barua ya Lipumba na Sakaya, yaujulisha umma na kueleza itafanya uamuzi baadaye.

[HASHTAG]#Jumanne[/HASHTAG], Tarehe 25/07/2017 jioni - Katibu Mkuu wa CUF (Seif Sharif) amuandikia Spika wa Bunge kumjulisha kuwa Barua za Lipumba na Sakaya ni Feki kwa sababu Lipumba si mwanachama, na kubwa kuliko yote hakuna kikao cha Baraza Kuu HALISI na HALALI kilichofanyika, maana vikao vyote vya chama havimuungi mkono Lipumba.

[HASHTAG]#Jumatano[/HASHTAG], Tarehe 26/07/2017 mchana - Spika aridhia kufukuzwa wabunge 8 na apeleka taarifa NEC. Adharau na kukiuka hata taarifa halisi aliyopewa na Katibu Mkuu kuwa barua alizopelekewa na Sakaya na Lipumba hazitoki kwenye mamlaka ya Baraza.

[HASHTAG]#Jumatano[/HASHTAG], Tarehe 26/07/2017 Jioni - Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaridhia na kutoa agizo kuandaliwa wa Wabunge wapya ikishawasiliana na Lipumba

Tarehe 27/07/2017 Asubuhi - NEC yatangaza Wabunge wapya wa Lipumba.
_________________##_####____________
[HASHTAG]#Najaribu[/HASHTAG] kujiuliza, Kasi hii ingetumika kuleta viwanda tangu John Magufuli aingie madarakani, hivi sasa si Tanzania ingekuwa na kiwanda cha ndege? Yaani Bombardier zingetengenezewa hapo nchini!

[HASHTAG]#Kasi[/HASHTAG] hii ingetumiwa na Serikali kutoa huduma hospitalini, shuleni, ofisini n.k. wagonjwa wasingekufa kwa Maradhi ya kijinga kwenye foleni za Upasuaji na huduma nyepesi.

[HASHTAG]#Kasi[/HASHTAG] hii ingetumiwa na serikali kusambaza umeme na maji safi na salama, kusingekuwa na familia inapoteza wapendwa wao kwa sababu ya maradhi ya maji.

[HASHTAG]#Kasi[/HASHTAG] hii ingetumika kupambana na mafisadi, wale wote waliongia mikataba ya kipuuzi ya madini, na walioisababishia nchi hasara kubwa kwenye sekta ya ujenzi, taifa letu lingekuwa la haki kweli kweli.

[HASHTAG]#Kasi[/HASHTAG] hii ingetumika kujenga viwanda vya nguo alivyoahidi JPM wiki iliyopita, hivi sasa (leo, kutokea wiki iliyopita) tungekuwa tunapandisha marobota ya mitumba kuwapelea wazungu wakavae Ulaya!

KASI! SPIDI! MBIO! MFUKUZANO.... call it any name!

@Nilikuwa naangalia uzinduzi wa Treni ya Risasi (Bullet Train) inayotembea Kilomita 350 kwa saa iliyozinduliwa nchini China jana. Post hii haihusu yanayoendelea huko nchini.

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J

HAKIKA KWA MWENDO KASI HUU TANZANIA YA VIWANDA NI SIKU CHACHE TU ZIJAZO.
 
Namfuatilia sana Mtatiro na namuombea sana kuwa anamaanisha anayoyaandika. Maana tumeshachanganyikiwa na kinachoendelea hivyo isije kuwa naye kapelekwa USA katika kupisha haya yatimie!
 
Mtatiro, tangu mgogoro huu uanze, ninyi kama CUF, ni hatua gani mlizochukua kutafuta suluhu ili kumaliza mgogoro? au mlitaka CCM nio wawasaidie kumaliza mgogoro wenu?

je! hamkushauriwa?
 
"Have you ever stood
In the darkness of night
Screaming silently
You're a man?
Have you ever thought
That a time would come
When your voice would be heard
In a new nation?
Have you waited for so long
Till your unheard song
Has stripped away your very soul?
Well, then
Believe it, my friend
That this silence can end
We'll just have to get guns
And be men."
 
Mwisho wa haya ni timu ya Maalim na Mtatiro kwenda Chadema ....huu mgogoro unakuzwa kupitia CCM na Chadema ....CUF inasambaratika ....Mtatiro anajipa moyo lakini hii ngoma wameshapigwa ....
Mkuu ukisikiliza mahojiano ya TV clouds na Maalim Seif, Lipumba na Msaidizi wa msajili wa vyama, ni rahisi sana kujua looser katika hii vita ni nani.
Lupumba alienda na KATIBA ya CUF na kujieleza based on katiba ya CUF inasemaje.
Msajili pia alieleza based on KATIBA ya CUF inasemaje.
Maalim Seif hakutaka hata kuigusa KATIBA ya chama na sikumbuki kama alikumbuka au alijisahaulisha kwenda nayo.

Lipumba Alisema yupo tayari kufanya mdahalo na Maalim na timu yake ili kulimaliza suala la mgogoro
Maalim Seif alikataa katakata kuonana na Lipumba.
 
Mkuu unayosema ni maneno ya kweli tupu.
Tatizo ambalo hata wewe waweza kuniunga nkono ni ombwe la uongozi katika vyama vya upinzani na uimara wa uongozi katika chama tawala uliopo kwa sasa.
Sasa hivi siasa za Tanzania ni mchafukoge mno, yaani vise versa.
Baadhi ya raia, tumeachwa tunaelea angani bila kukidhi kiu yetu ya ushabiki wa kisiasa.
Hao chadema niliishasema kuwa chama alichokitengeneza katibumkuu Slaa ni chama kizuri na kina sera nzuri, ila kwa sasa hakina viongozi wa maana. viongozi wote ni wababaishaji.
Hakuna hata mmoja mwenye sifa za kuongoza nchi kwa sasa.
Tukija ccm. Rais mzuri, ila ndani ya chama bado kuna "mafisi" makandokando hayajaisha kwa kuwa bado hayajamulikwa.
Ulinganisho.
Rais Magufuli alitakiwa awe kiongozi wa chadema, maana anafuata na kuzitekeleza sera zake za kutumbua mafisadi na kinyoosha nchi, kama ambavyo Slaa alitamani.
Mbowe alitakiwa awe mwenyekiti wa ccm yenye masalia ya mafisadi, ambayo kila uchao ndiyo amekuwa mtetezi wa mafisadi tangu 2015 alipolambishwa pesa za sabuni ya kutakatishia mafisadi, mwana kabadilika, kakoma kukosoa mafisadi.
Hawasemi tena vibaya, amekuwa ni kipenzi chao, tofauti na msimamo wa katibu mkuu mstaafu wake.

Ushabiki wa kisiasa ndio tatizo kubwa kwa watanzania,watanzania wanashidwa kufahamu kuwa mwanasiasa akiwa Mbunge, Raisi, Mwenyekiti wa mitaaa kakaa kwenye kiti cha uongozi kwasababu ya wananchi,raia ndio waliomchagua kwa kumpigia kura, kazi yake ni kuwatumukia raia..

Tafauti ya watanzania na raia wa nchi nyengine ni kuwa Tanzania raia wa kawaida wanawaogopa wanasiasa badala ya wanasiasa kuwaogopa Raia..

Watanzania wamejawa na mapenzi ya vyama hata kama chama hakiwatendei haki,wako wanaokufa na CCM lakini nyumbani hakuna hata cha jio,wanakuwa barabarani kumlinda mkuu wa chama,wako wanakufa na CDM na CUF hata kama hivi vyama havina masilahi yoyote kwao..

Mpaka pale watanzania watakapo amka na kufahamu kuwa wanasiasa wako pale walipo kwa masalahi yao binafsi,wanatajirika kila siku kwa jasho la wanachama ndio Tanzania itakuwa huru....
 
Kinachowapa moyo kina Mtatiro ni uungwaji mkono wanaoupata toka kwa wanachama walio wengi ndani ya CUF.
Sefu hana watu bara.Angekuwa nao angeshachukua ofisi ya buguruni hata kwa kumwaga damu
Mnaomuunga mkono sefu mnapoteza muda na nguvu zenu tu,subirini urais wa mezani anaowaahidi kila siku.
Sefu amekwama,suluhisho akubali kukaa na Lipumba,hakuna jisnsi yoyote atakayoweza kuibuka mshindi hapa
 
d1469e4491f5edbaa74dd21e04a188a1.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna makosa yalifanywa na cuf, badala ya kumpuuza lipumba siku ile alipofanya upuuzi ule siku hiyo yangepelwkwa maombi mahakamani chini ya hatibya dharura kupiga upuuzi ule na order ya mahakama ingekuwa ishatoka, wamekimbiza mchakato ili hata amri ya mahakama ikitoka hata kesho haina maana tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtatiro na viongozi wote wa upinzani wa nchi hii, tuache kuwadanganya wananchi na tuache woga. Nchi hii dawa yake ni UASI. Tukubali wote kuwa Lissu. Tuache woga tulikomboe Taifa hii itamaanisha wengine kuingia jela na wengine kupoteza maisha. Hii lugha ya kulinda amani ifutwe kabisa. Wazee kama Lowasa inabidi watusubiri.

Vijana mko wapi. Twendeni barabarani.
 
Back
Top Bottom