Hapana mkuu ...upinzani una miaka 25 ya uhai lakini wanafanya makosa yale yale ....wengine tulijiaminisha Chadema ni tofauti lakini nao wanapita kule kule ....hii CUF inakufa sababu ya Chadema na CCM ....Maalim na kundi lake wanaungwa mkono na Chadema while Lipumba yupo na CCM ....ushawishi wa hawa wana CUF nje ya CUF hautakuwa na nguvu ile ile ....hesabu za hovyo hovyo tu ....subiri uone hii vita inapoenda ...Nyakati za sasa inatakiwa kuwa very smart kwa wapinzani kuendelea kuoperate
Ni mpumbavu pekee anayeweza kushangilia ujinga huu!
Na ni Kiongozi asie makini pekee ndiye anayeweza kubariki unajisi huu wa haki!
Duniani kote na sehemu zote zilizopoteza Amani, watu wake hasa viongozi walitenda matendo haya.
Natabiri Amani ya Nchi hii itavurugika si muda mrefu. Ni vigumu kupora haki za watu kila kukicha kisha mtarajie utulivu.
Na kwa kuwa tumejawa unafiki, sitashangaa wapinzani wakipewa lawama baada ya Amani kutoweka!
Ifikie wakati wenye magonjwa mazito wazuie kuendelea na nyadhifa nyeti kwa usalama wa Nchi hii!
Uwezo wao wa kufanya maamuzi sahihi umeyumba!
Amri kutoka juu marekani amri inatoka chini kwenda juu na ndio democracyWakuu mnakumbuka mahakama ilichukua juma moja kuondoa utata wa amri ya TRUMP Kwamba ni halali au sio halali. Jibu likawa ni HALALI na watu wakaendelea kuingia USA.
Sasa huku TZ, kuna utata, na kesi ipo mahakamani: LIPUMBA ni mwanachama/mwenyekiti halali au sio halali?
Sasa umekatika mwaka na nionavyo mimi uamuzi utatolewa 2021. Sababu ni nini?
je, athari za kuchelewesha kuondolewa utata ni zipi? je, mahakama zetu zipo huru kweli?
Hakika huku kutumika kwa lipumba na ccm na serikali yake iko siku italigharimu Taifa hili na mwisho wake unakujaHATUA ZA BUNGE, LIPUMBA NA MSIMAMO WANGU!
[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J,
[HASHTAG]#NewYork[/HASHTAG].
1. Juzi Jumatatu Lipumba na Sakaya walimuandikia Spika wa Bunge kumjulisha kuwa "Baraza Kuu la CUF" (feki) limewafukuza uanachama Wabunge 8 wa Viti Maalum wa CUF. (Spika alishaandikiwa na Katibu Mkuu kumjulisha kuwa Baraza Kuu halali la CUF ni lile lililochaguliwa mwaka 2014 na muda wake utaisha mwaka 2019 na Baraza hilo halali ndilo lililomfukuza Lipumba).
2. Jana, Jumanne, Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kwa umma kuujulisha kuwa imepokea maelekezo kutoka kwa Sakaya na Lipumba kuwa wabunge hao 8 si wanachama na Ofisi hiyo ikaeleza kuwa bado inatafakari hatua za mwisho za kuchukua.
3. Leo Jumatano, Ofisi ya Bunge imetangaza uamuzi wake, kwamba inakubaliana na maelekezo ya Lipumba na Sakaya na kuwa imewavua wabunge hao 8 ubunge wao wa Viti Maalum, na kuwa imeiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuijulisha kujaza nafasi hizo zilizo wazi.
_________________________________________
Nataka kuwaeleza wanachama na watanzania wote, kwamba viongozi wa chama wanakutana kuendelea kuchukua hatua.
Tunajua kuwa Vyombo vya Serikali hivi sasa vinafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa aidha CUF inamkubali "MSALITI" Lipumba kuwa Mwenyekiti wake, au CUF isambaratike. Na suluhisho la hali hii haliwezi kuwa kukaa chini na MSALITI.
Mnapopambana na WASALITI WALIOKUBUHU na wako ndani ya nyumba yenu, vita yake siyo ndogo. Lakini mimi binafsi ni muumini mkubwa wa HAKI na UKWELI. Naamini kuwa CUF itavuka misukosuko hii.
Kwa jicho moja wapo watu wanachekelea na kudhani kadhia hii ni ya CUF tu, mimi natizama hali hii kama Mapambano ya Dola ya kuhakikisha vyama mbadala vinaongozwa na wasaliti ili Dola iendelee kuwatumia kuzamisha demokrasia na ushindani wa kisiasa nchini.
Dola ikifanikiwa kuisambaratisha CUF, vyama vingine vya upinzani havitakuwa salama, taasisi zingine za kiraia hazitakuwa salama pia. Anayeyatizama mapambano haya kama vita ya ndani ya CUF hajaisoma dunia - haya ni mapambano makubwa, dhidi ya demokrasia ya Tanzania.
Mimi ni mwanademokrasia imara na sitayumbishwa na WASALITI. Kumkubali Lipumba na genge lake itakuwa na maana ya kuiua CUF moja kwa moja Tanzania Bara, maana alipojaribu kukimbia mwaka 2015, ndipo CUF iliibuka na kuwa chama imara mara 10 Tanzania bara. Na kurudishwa kwake kwa nguvu kunakofanywa na dola ni mkakati wa kuimaliza CUF na suluhisho lake haliwezi kuwa CUF kumtambua Lipumba.
Hata DOLA ikifanya nini, LIPUMBA ameshadharaulika na hawezi kuisaidia tena dola hii yenye upofu. Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Seif Sharif Hamad na viongozi wa chama wanaendelea na hatua mbalimbali muhimu na mtajulishwa
Vita imeshapanuka, sasa ni LIPUMBA, OFISI YA MSAJILI WA VYAMA, RITA, BUNGE, NEC, IKULU, USALAMA WA TAIFA na CCM. Kundi lote hilo linaamini kuwa bila kumrudisha Lipumba halitaweza kuidhibiti CUF. Sisi viongozi tuko imara sana na tunaamini kuwa HAKI huweza kucheleweshwa tu!
We shall OVERCOME this! More Stable! And more Vibrant!
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG], 26 Julai 2017.
Hakika. Cuf wanaelekea shimoni. Kwani mwisho wa kadhia hii ni Lipumba kubaki na cuf isiyo na nguvu kwani Zanzibar hawamtaki. Na maalim baada ya kuaibishwa na Lipumba huku akishikwa mkono na cdm kuelekea shimoni atawapigia debe cdm Zanzibar na yeye kubaki kuwa kibaraka wa cdm na huo ndio utakuwa mwisho wa cufMwisho wa haya ni timu ya Maalim na Mtatiro kwenda Chadema ....huu mgogoro unakuzwa kupitia CCM na Chadema ....CUF inasambaratika ....Mtatiro anajipa moyo lakini hii ngoma wameshapigwa ....
Ni mpumbavu pekee anayeweza kushangilia ujinga huu!
Na ni Kiongozi asie makini pekee ndiye anayeweza kubariki unajisi huu wa haki!
Duniani kote na sehemu zote zilizopoteza Amani, watu wake hasa viongozi walitenda matendo haya.
Natabiri Amani ya Nchi hii itavurugika si muda mrefu. Ni vigumu kupora haki za watu kila kukicha kisha mtarajie utulivu.
Na kwa kuwa tumejawa unafiki, sitashangaa wapinzani wakipewa lawama baada ya Amani kutoweka!
Ifikie wakati wenye magonjwa mazito wazuie kuendelea na nyadhifa nyeti kwa usalama wa Nchi hii!
Uwezo wao wa kufanya maamuzi sahihi umeyumba!
Mtatiro anajipa moyo tu. Hayo maji yalipofikia sio size yao tena. Anafikiri sisi watz hatuna macho?Nyie akina mtatiro endeleeni kushangaa tuu na mtashangaa hadi kiama
usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
Hope lessNyie akina mtatiro endeleeni kushangaa tuu na mtashangaa hadi kiama
usitembee juu ya ardhi kwa majivuno