Mtatiro: Hatua za Bunge, Lipumba na msimamo wangu! Na maajabu ya Bunge na serikali ya CCM

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,706
2,000
Mwisho wa haya ni timu ya Maalim na Mtatiro kwenda Chadema ....huu mgogoro unakuzwa kupitia CCM na Chadema ....CUF inasambaratika ....Mtatiro anajipa moyo lakini hii ngoma wameshapigwa ....
kaka mfano wako ni sawa na ngedere kumsusia shamba, CUF ni brand name kubwa - itakuwa kosa kubwa kumsusia mtu Brand name "CUF" mtu ambaye aliicha kwenye mazingira mazito mno kweye uchaguzi Mkuu.

Walifanikiwa kuisambaratisha NCCR -Mageuzi, wakajaribu CDM wakakwama; ila ngoja tuone huu mziki wa CUF utakuwaje - maana muvi ndiyo limefikia pahala patamu sana.
 

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
4,617
2,000
Tatizo lilianza mlipoolewa na chadema hatimaye kununuliwa na kada kindakindaki wa chama changu, jitu pesa laigwanani wa watu kaweka vyama vitatu vizito mfukoni kwake na prof. atahaha sana kuwanasua mpaka anaonekana chizi
 

mbandeon

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
1,451
2,000
Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kuandika uandikacho unless kalewa. And you prove the same
Of course, kwasababu mimi niko huru sio mfungwa kama wewe uliyeshurutishwa usifie kila kitu cha Mbowe na ukosoe kila kitu cha Magu.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,953
2,000
Of course, kwasababu mimi niko huru sio mfungwa kama wewe uliyeshurutishwa usifie kila kitu cha Mbowe na ukosoe kila kitu cha Magu.
Hebu weka quote ya makosa ya Mbowe ambayo mimi nimesifia. Au weka jambo la maana la Magu ambalo nimelipinga. Acha kupiga mayowe bila sababu!
 

HesabuKali

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
2,241
2,000
Aitwe na bunge kama nani ndani ya serikali au chama chake? Au kila anayesema maneno yasiyopendwa na bunge aitwe bungeni kuhojiwa?. Kama unataka kusema Mtatiro ni kiongozi wa Cuf umepotoka kwasababu huyo spika wako hamtambui kama kiongozi wa Cuf ila anamtambua Lipumba, ndio maana ametekeleza amri ya Lipumba bila kumsubiria Mtatiro ambaye ni kiongozi wa kamati ya uongozi ya Cuf kikatiba ila kiserikali hawamtambui.
Na mimi nasema ni maamuzi ya kihayawani kabisa na yanapaswa kulaaniwa na watu wenye kutumia akili tu, nasubiria kuitwa na bunge kuhojiwa.
 

Rita Warobi

JF-Expert Member
May 17, 2017
343
1,000
Lipumba amekua a lughing to many, ameshadharaulika na watu wengi tangu ajiuzulu kwa mbwembwe nyingi na kurudi kung'ang'ania kukalia kitu alichokikimbia mwenyewe kwa hiari yake
 

mbandeon

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
1,451
2,000
Hebu weka quote ya makosa ya Mbowe ambayo mimi nimesifia. Au weka jambo la maana la Magu ambalo nimelipinga. Acha kupiga mayowe bila sababu!
Dang! i knew it ... kama usharudi kisutu nenda kapete chai kwanza.
 

forex

Senior Member
Jun 15, 2017
198
250
HATUA ZA BUNGE, LIPUMBA NA MSIMAMO WANGU!

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J,
[HASHTAG]#NewYork[/HASHTAG].

1. Juzi Jumatatu Lipumba na Sakaya walimuandikia Spika wa Bunge kumjulisha kuwa "Baraza Kuu la CUF" (feki) limewafukuza uanachama Wabunge 8 wa Viti Maalum wa CUF. (Spika alishaandikiwa na Katibu Mkuu kumjulisha kuwa Baraza Kuu halali la CUF ni lile lililochaguliwa mwaka 2014 na muda wake utaisha mwaka 2019 na Baraza hilo halali ndilo lililomfukuza Lipumba).

2. Jana, Jumanne, Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kwa umma kuujulisha kuwa imepokea maelekezo kutoka kwa Sakaya na Lipumba kuwa wabunge hao 8 si wanachama na Ofisi hiyo ikaeleza kuwa bado inatafakari hatua za mwisho za kuchukua.

3. Leo Jumatano, Ofisi ya Bunge imetangaza uamuzi wake, kwamba inakubaliana na maelekezo ya Lipumba na Sakaya na kuwa imewavua wabunge hao 8 ubunge wao wa Viti Maalum, na kuwa imeiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuijulisha kujaza nafasi hizo zilizo wazi.

_________________________________________
Nataka kuwaeleza wanachama na watanzania wote, kwamba viongozi wa chama wanakutana kuendelea kuchukua hatua.

Tunajua kuwa Vyombo vya Serikali hivi sasa vinafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa aidha CUF inamkubali "MSALITI" Lipumba kuwa Mwenyekiti wake, au CUF isambaratike. Na suluhisho la hali hii haliwezi kuwa kukaa chini na MSALITI.

Mnapopambana na WASALITI WALIOKUBUHU na wako ndani ya nyumba yenu, vita yake siyo ndogo. Lakini mimi binafsi ni muumini mkubwa wa HAKI na UKWELI. Naamini kuwa CUF itavuka misukosuko hii.

Kwa jicho moja wapo watu wanachekelea na kudhani kadhia hii ni ya CUF tu, mimi natizama hali hii kama Mapambano ya Dola ya kuhakikisha vyama mbadala vinaongozwa na wasaliti ili Dola iendelee kuwatumia kuzamisha demokrasia na ushindani wa kisiasa nchini.

Dola ikifanikiwa kuisambaratisha CUF, vyama vingine vya upinzani havitakuwa salama, taasisi zingine za kiraia hazitakuwa salama pia. Anayeyatizama mapambano haya kama vita ya ndani ya CUF hajaisoma dunia - haya ni mapambano makubwa, dhidi ya demokrasia ya Tanzania.

Mimi ni mwanademokrasia imara na sitayumbishwa na WASALITI. Kumkubali Lipumba na genge lake itakuwa na maana ya kuiua CUF moja kwa moja Tanzania Bara, maana alipojaribu kukimbia mwaka 2015, ndipo CUF iliibuka na kuwa chama imara mara 10 Tanzania bara. Na kurudishwa kwake kwa nguvu kunakofanywa na dola ni mkakati wa kuimaliza CUF na suluhisho lake haliwezi kuwa CUF kumtambua Lipumba.

Hata DOLA ikifanya nini, LIPUMBA ameshadharaulika na hawezi kuisaidia tena dola hii yenye upofu. Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Seif Sharif Hamad na viongozi wa chama wanaendelea na hatua mbalimbali muhimu na mtajulishwa

Vita imeshapanuka, sasa ni LIPUMBA, OFISI YA MSAJILI WA VYAMA, RITA, BUNGE, NEC, IKULU, USALAMA WA TAIFA na CCM. Kundi lote hilo linaamini kuwa bila kumrudisha Lipumba halitaweza kuidhibiti CUF. Sisi viongozi tuko imara sana na tunaamini kuwa HAKI huweza kucheleweshwa tu!

We shall OVERCOME this! More Stable! And more Vibrant!

[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG], 26 Julai 2017.
Seif's CUF is in Defence & Lipumba's CUF is in attack! A person in attack is the one who owns initiatives! He decides where to punch a hole in enemy's defence! What should one in defence do is to launch a preemptive attack!

If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat
 

Mcharo son

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
2,739
2,000
Wakuu mnakumbuka mahakama ilichukua juma moja kuondoa utata wa amri ya TRUMP Kwamba ni halali au sio halali. Jibu likawa ni HALALI na watu wakaendelea kuingia USA.

Sasa huku TZ, kuna utata, na kesi ipo mahakamani: LIPUMBA ni mwanachama/mwenyekiti halali au sio halali?

Sasa umekatika mwaka na nionavyo mimi uamuzi utatolewa 2021. Sababu ni nini?
je, athari za kuchelewesha kuondolewa utata ni zipi? je, mahakama zetu zipo huru kweli?
KOSA WALILOFANYA CUF WAKATI LIPUMBA KAAMUA kujitoa ni wao kutoliweka kiofisi zaidi kuogopa joto la uchaguzi. Ni sawa na Chadema walivyokaa kimya Slaa alipojichomoa. Hawajamlima barua rasmi ya kujiondoa kwake wakitegemea atarudi au kuogopa joto la uchaguzi kipindi kile. Kisheria Lipumba kaona mwanya huo ndio kajua akirudi hakuna wa kumzuia (kisheria) KWANI HAKUNA MAANDISHI YA KIOFISI NA YA KIUTARATIBU WA katiba yao ULIOHALALISHA KUTOKA MADARAKANI KWA LIPUMBA. Ndio hicho kinachowatesa sasa.
Ila ki-maadili lipumba anajua alishajitoa, kinachompa matumaini ni nguvu ya Msaada aliohadiwa kupata endapo akifanya haya anayofanya.
 

Mcharo son

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
2,739
2,000
Seif's CUF is in Defence & Lipumba's CUF is in attack! A person in attack is the one who owns initiatives! He decides where to punch a hole in enemy's defence! What should one in defence do is to launch a preemptive attack!

If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat
Yap, ila wale waliotaka kuanzisha operesheni fagia Buguruni MOVE YAO SIJUI KAMA WALIIPANGA VIZURI upande wa kuzuia mabomu ya reactions hizi
 

Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,531
2,000
Sasa atachaguliwa na nani huyo lipumba wenu wakati wanachama wa cuf Tz bara wote hatumtaki msaliti na pandikizi lenu ccm?

Mkuu sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa toka nizaliwe.

Jikazeni mpambane na siasa zenu maana wote wasanii nyinyi na prof hakuna mwenye afadhali wote wasanii tu.

Mnahangaika sana ila lengo kuu ni ruzuku nyingine mbwembwe tu.
 

forex

Senior Member
Jun 15, 2017
198
250
Yap, ila wale waliotaka kuanzisha operesheni fagia Buguruni MOVE YAO SIJUI KAMA WALIIPANGA VIZURI upande wa kuzuia mabomu ya reactions hizi
Wangeweza kubadili upepo na CUF ya Lipumba wangeanza kudefend hivyo kupoteza malengo na CUF ya Seif wakapanua wigo wa mapambano ie multiple lanes attack! Adui angechanganyikiwa na kuuawa at a peace meal!

If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom