Mtatiro:CHADEMA wanapoteza muda kuitukana CUF

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro ameonya harakati za vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi ujao.

Waraka wa Mtatiro ulionaswa na Habarimpya.com unalenga kuvionya vyama ya upinzani hususan CUF na CHADEMA kutokana na mkakati aliouita kuwa ni feki na ambao Chama Cha Mapinduzi CCM wanauchekelea.

Katika waraka huo ambao Mtatiro alielezea kuwa unalengo la kuidhoofisha CUF kutokana na jitihada za CHADEMA kukishambulia Chama hicho kila wakati, badala ya kuunganisha nguvu za upinzani kwa lengo la kuing'oa CCM madarakani.

"CHADEMA wanapoteza muda kuitukana CUF ambayo haihusiki hata kidogo na umasikini ulioasisiwa na CCM kwa nusu karne,kitendo cha Wenje kuihusisha CUF na siasa za ushoga ni cha kipuuzi na cha kitoto mno. Ezekiel Wenje na CHADEMA , wala hamtaishia hapo, mtaanza kutukanana ninyi kwa nyinyi"alisema Mtatiro katika waraka wake.

"Hatuwezi kuendelea kuwa na Bunge na Wabunge wanaotumia vibaya nafasi tulizowapa, na maposho yanayotokana na jasho letu kwa kuanza kufanya mambo yasiyo na maana, mtu unapewa fulsa ya kusoma maoni ya kambi rasmi ya upinzani, badala yake unaanza kurusha vijembe na matusi, Watanzania wanataka kuona kambi rasmi inayojitambua na yenye hadhi ya kutoa hoja zenye mashiko kuliko hizi siasa za upinzani kutukana mpinzani mwenzie tena mahali rasmi kama Bungeni,tunahitaji Kambi rasmi inayojiheshimu na isiyofanya siasa za kihuni
 
akamuulize kwanza Prof Lipumba kwanini walimsaidia JK 2010 kushinda na walimsaidiaje... ama anapinga hawakumsaidia?
 
Huyu ndiye kiongozi wa kile chama chenye mlengo wa.kiliberali ambacho wabunge wake wanawaambia wenzao wakome, wakome, wakome mara mia moja. Awape kwanza hao wabunge mwongozo wa kuongea.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Waraka? Mbona kayaweka facebook wall yake same day? Ungesema Lipumba leo Mwanza sawa. All in all, hakuna jipya
 
Ccm hoyee!! Hivi Ntatiro anadhani CDM nimaboya? Yale yale, ya ndoa za jinsia nyingi, Cuf inataka kuwa na ndoa za wanaume wangapi?
 
Mtatiro hajui hana chake CUF anatumiwa ili kubalance safu ya uongozi ionekane ya kitaifa na yenye kuwakilisha dini zote.Kama anabisha amuulize Prof Lipumba alichokisema msikiti wa Idrissa alikuwa anamaanisha nini ?.
 
Mtatiro hajui hana chake CUF anatumiwa ili kubalance safu ya uongozi ionekane ya kitaifa na yenye kuwakilisha dini zote.Kama anabisha amuulize Prof Lipumba alichokisema msikiti wa Idrissa alikuwa anamaanisha nini ?.
acha chuki kwa ukirsto wk
 
Yeye mtatiro alishafanya jitihada zipi za kuunganisha nguvu ya vyama vingine ? Na unaungana vp na Chama ambacho kipo katika mwafaka na chama tawala?
 
acha chuki kwa ukirsto wk

983725_289156777887996_1295913343_n.jpg
Wana Arusha wana matusi, yaani makamu wa rais kabisa watu hata kwenye kikombe hawajai
 
Back
Top Bottom