Mtatiro anasemaje kuhusu hatma na Upepo huu unaovuma CUF Live on STAR TV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtatiro anasemaje kuhusu hatma na Upepo huu unaovuma CUF Live on STAR TV

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Mar 2, 2012.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Habari za Ijumaa wanaJF

  Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara Julius Mtatiro atazungumza kuhusu majaaliwa ya chama hicho kwa sasa kutokana na upepo mbaya wa kisiasa unaovuma katika Chama hicho, Lakini kuna ukweli wowote kuwa kuondolewa kwa Mbunge wa Wawi H.R na kundi lake ndio chanzo cha mpasuko Huu?

  Upande wa pili wa studio atakuwepo Doyo Hassan Doyo kutoka Kambi iliyoenguliwa ya H.R kwa pamoja wakizungumzia majaaliwa ya CUF

  Karibuni katika mjadala tukiangazia nini majaaliwa ya upinzani Nchini kama CUF itameguka mapande mawili?

  Je Uhai wa Chama hiki bado upo kama awali?

  Ofisi ya Musoma ambayo kwa Kanda ya ziwa ni moja ya kati ya ngome yao kubwa imefungwa, inatoa ishara gani kwa chama hiki?

  Pia katika mjadala atashiriki Ansbert Ngurumo.

  Karibuni
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Yahya wewe ndio utakuwa unaendesha kipindi au? Tutupie majadiliano japo kwa ufupi hapa JF.

  Naomba Mtatiro afafanue hili jambo: Kila watu wakijiengua CUF yeye huwa anatoa kauli kwamba hao walikuwa watu wa Hamad na walishafukuzwa siku nyiiingi; hivyo basi Mtatiro atuambie hadi sasa CUF imeishafukuza wanachama wangapi tangia sakata la Hamad Rashid Mohamed.
   
 3. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Kuna uhusiano wowote kati ya Doyo,Hamad na chama kipya cha ADC?
   
 4. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yahya,
  Chama cha CUF kimefikia tamati na kinaendea kufa kabisa. Dhambi ya viongozi wa CUF kujifanya ni malaika na wasioweza kuhojiwa na waliowaweka madarakani, imekimaliza chama na itawamaliza viongozi hao kisiasa.
  Mtatiro ni kijana mwenzetu, amekosea na alikosea sana kupuuza hoja za HR. Kwa kutumia ubabe usio na dira juu ya maamuzi kwa HR, sasa amekiteketeza chama huku hao hao akina Mtatiro wakiendelea kubeza. Jumapili iliyopita nikiwa TBR nilimsikia Mtatiro na Mh Sakaya hapa TBR kwenye mkutano wa hadhara, lakini hawakugusia mpasuko wa kina unaokiandama chama. Tamati ya CUF imefika, ni aibu kubwa kwa masultan Seif na Lipumba, kwamba hakuna afaaaye kuongoza zaidi yao, tamaa zimewazidi na mivuto yao imetoweka.
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Swali kwa Mtatiro,
  Nini hatma ya CUF? Nini mustakbali wa fitna zake kwa Lipumba & Maalim kupitia email juu ya HR tulizozinasa? Je, alichokiamini Mtatiro ndicho anachoendelea kukiamini? Je, uimara wako kisiasa unategemea fitna mnazotengeneza ili muendelee kuwepo madarakani ama? Je, ndio style ya kuisaidia nchi kwa kufukuzana badala ya kupeana onyo?
   
 6. k

  kiponzelo Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cuf na imani kabisa upepo unaonekana wapi unavuma nashangaa mtatiro unashindwa kuona?hivi mtatiro ni elimu gani itumike kukuelimisha kwamba cuf bara kimekufa?
   
 7. N

  NGOWILE JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 454
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wa DODOMA,CUF imekufa kutokana na dhambi ya kufunga ndoa na CCM.Walilidhihisha hilo kwenye uchaguzi wa spika kwani waliunga mkono CCM.Wameonyesha hilo igunga na Jusa kadhihisha kwa kauli kua CUF imeshindwa UZINI kwa sababu kuna wakristo na wabara wengi.Je CUF kweli kwamba ni ya Waislam na Wazanzibari tu? CUF imefukuza wanachama wangapi katika sakata HAMAD RASHID?
   
 8. Imany John

  Imany John Verified User

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  MTATIRO,what is METAMOPHOSIS?

  Kama haujui jibu ni:

  is a word for
  the changing of an animal or
  insect into another, such as a
  caterpillar to a butterfly or a
  tadpole to a frog.

  Swali:
  kwa kua chama chenu kimepitia hatua zote hapo juu je hauoni umebakisha END stage ya KIFO?
  Na dalili zipo wazi.
   
 9. K

  KWELIMT Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  ZA ASUBUHI SALAMA YAHAYA!

  AWALI YA YOTE MI NI KATI YA WANANCHI AMBAO NI WAFUATILIAJI WA VIPINDI VYENU,KIPINDI CHENU NI NZURI SANA,ILA NINA

  WASIWASI WATU WENGI KAMA WAFANYAKAZI,WANAFUNZI N.K AMBAO KWA MUDA KAMA HUU WAKO BIZE KUTAFUTA SHILINGI

  HAWAWEZI KUFUATILIA, NAPENDEKEZA KINGEFANYIKA USIKU SAA 3 USIKU ILI WATU WENGI WAWEZE KUFAIDIKA,KUSHIRIKI ILI

  KUPATA NA KUSAIDIA KUFIKISHA UJUMBE KWA WATANZANIA WOTE.


  Anyway,kuhusu mada iliyoko mezani,ni dhahiri hapa tulipofika,hakika kwa kauli tata kama za akina viongozi Mtatiro,JUssa nadhani CUF inafikia mwisho wa uhai wake kisiasa.Cjui CUF hawana washauri wa kulea vijana kiitikadi na kiuongozi ili waweze kuendana na maadili ya kitanzania na ya kiuongozi.Mh JUSSA aliwahi kutoa lugha ya matusi kwa mh SITTA kana kwamba wako sawa kiumri,Mh SITTA ni waziri wa serikali ya muungano ila hakulijali kabisa hilo.

  Pili,amethibitishia umma kuwa CUF imeshindwa Uzini kwa kuwa pale kuna wakristo wengi sana,wabara wengi sana.Hizi kauli ambazo hatukutegemea kutolewa na viongozi wa kuu kama akina Jussa.Je, Tendwa kwanini hakutoa karipio kuhusu kauli hii?

  MGOGORO WA CUF NI WA KIMASLAHI ZAIDI,UPANDE MOJA UNATAKA KUINGIA KUFAIDI MATUNDA YA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA.ULIOPO MADARAKANI UNATAKA UENDELEE KUFAIDI KEKI ILE.  NB:SAMAHANI SIWAPANGII UTARATIBU WA KUPANGA VIPINDI VYENU.  Nawasilisha.
   
 10. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Swali kwa mtatiro:
  Unadai kwamba kauli ya Jusa haikuonyeshwa kwa mapana ili watu wamuelewe. Sasa je, inakuwaje Kiongozi Mwenzako mnayefanya nae kazi pamoja siku hadi siku hadi leo hamjamuuliza ni kwa nini alizungumza aliyozungumza unakuja kuzungumza kwenye televisheni kutufafanulia kauli zile kwa kufikiri May be alikuwa anamaanisha hivi, may be alimaanisha vile? Huoni kwamba hayo ndio mapungufu yenu ninyi kama viongozi wa CUF na ndio inapelekea kuua chama chenu?
   
 11. N

  NGOWILE JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 454
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wa Dodoma.Mtatiro tueleze CUF imejifunza nini IGUNGA,UZINI,na sasa tuwaeleweje kwa kujitoa Arumeru?
   
 12. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Matatiro aseme ukweli kuwa Cuf siyo ile ya enzi zile CUF ngangari na ngunguri na kama mnafuatilia utaona bnaada ya cuf kuacha itikadi ile imepoteza mvuto.
   
 13. MKL

  MKL Senior Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi mtatiro unaposema hoja ya udili ililetwa na raisi mwaka 2010, unamaanisha nini? nakumbuka ni raisi huyu huyu alipigiwa debe sana na Askofu Methodius KIlaini mwaka 2005 kuwa JK ni changuo la Mungu na mbona hakusema kuwa kuna udini? Jussa aliropoka ni vema kwa niaba yake naomba ukiri hili badala ya kusema mmeomba tape ya mazungumzo hayo mlimani tv. Jussa na CUF kwa ujumla ni bora mkiri kuwa mwenzenu alichemka na hivyo kuwaomba radhi watanzania litakuwa ni jambo jema zaidi, Lingine ni kuwa Hebu Mtatiro tupe data Hamadi rashidi alikuwa na wafuasi wangapi kwani kila wafuasi wenuwanapohama chama unasingizia kuwa ni wafuasi wa hamadi. na kama Hamadi alikuwa na wafuasi wengi hivyo basi hamkuwa na haja ya kumfuka kwani wanachama karibu nusu ya CUF ni wafuasi wake basi....... Unasemaje kuhusu hayo mawili Mtatiro....?
   
 14. R

  Ritts Senior Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtatiro anamtetea Jussa kuwa mlimani tv walimnukuu vibaya kuhusu udini uko uzini.anataka mlimani Warelease huo mkanda.MTATIRO CHOKA MBAYA
   
 15. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Doyo katoa msemo leo nimeupenda,anasema kumpuuza Ahmad na wakongwe waasisi ni kosa kubwa na Maalimu Seifu na wenzake wamesahau mchango wa Ahmad uliowafikisha hapo walipo,akasema ''UKiona mbwa kakaa juu ya mti ujue kuna aliyempandisha juu"Binafsi nimeupenda huo msemo.
   
 16. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Swalo kwa Mtatiro:
  Kuna tuhuma ulipewa shilingi milioni 128, na Mketo shilingi 82 kama IMPREST kule Igunga, yani cash money ambayo hadi leo hii hamjawasilisha return yake in details zaidi ya ujumla wake, Unatuambia nini hapo?
   
 17. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Swali kwa Mtatiro:
  Katika moja kati ya mikutano ya Maalim Seif kule Pemba alinukuliwa akisema 'CUF imvuruge Mhe. Hamad Rashid ama Hamad Rashid Aivuruge CUF' una lipi la kuzungumza juu ya hili?
  Pili Unasemaje kuhusu ile Email ya Maalim Seif akimtumia Profesa Lipumba ikisema tunamfukuza jamaa yako na hata hayo maneno aliyonukuliwa katika mikutano ya kuvurugana yalikuwepo katika email hiyo na dhamira ya dhati ya kuwatimua Hamad Rashid na wenzake ilishachukuliwa na Maalim hivyo kile kikao kilikuwa ni cha kutimiza wajibu tu.
  Mwisho, Nini matarajio yenu katika kesi hii inayoendelea iliyofunguliwa na Mhe. Hamad Rashid na kina Doyo, Je, unaamini mtashinda?
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kuna tuhuma zilitolewa jana na Hamad kwamba Mtatiro alipewa milioni 128 kwa ajili ya uchaguzi igunga, akazitumia vibaya kiasi kwamba alikamatwa na hawara nyumba ya wageni akiwa ametelekeza kamapeni!
   
 19. O

  OMUSILANGA JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 384
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndgu yahaya habar! Siasa ni kila kitu i.e afya ni siasa,kilimo ni siasa,michezo ni siasa,uchumi na viwanda ni siasa etc lakini kwa murejesho huu wa kijana msomi mwenzentu Julius Mtatiro ni wazi kuwa siasa ni uongo ulio kubuhu na kichaka cha watu wachumia matumbo. MWL ALIPATA KUSEMA "UKWELI HAUPENDI KUPUUZWA PUUZWA,UKIPUUZWA HUWA UNA TABIA YA KUJILIPIZA KISASI." Ni ukweli kuwa changamoto ni sehemu ya mafanikio but hali inayo endelea ndani ya CUF ni wazi kuwa credibility before the public imepotea. CUF ya leo siyo ile ya enzi za ngunguli na ngangari .Chama kama taasisi kipo ICU, je Mtatiro anaweza kutuongoza kwenye kufikia Tanzania tuitakayo? Kama kijana mwenzetu tafakari sana na chukua hatua, siasa unazofanya ni siasa mfilisi, hii ni sawa na tembo kujificha kwenye shamba la karanga asi onekane. Nenda kaimarishe chama Musoma,Tanga,Mtwara etc ofisi zimefungwa baada ya viongozi kuji uzuru, hulioni hilo? MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU BARIKI MABADILIKO.
   
 20. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Anawajibika kutoa majibu kwa Watanzania na awe mkweli kwani yeye ni kiongozi wa taifa.

  Habari za Ijumaa wanaJF

  Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara Julius Mtatiro atazungumza kuhusu majaaliwa ya chama hicho kwa sasa kutokana na upepo mbaya wa kisiasa unaovuma katika Chama hicho, Lakini kuna ukweli wowote kuwa kuondolewa kwa Mbunge wa Wawi H.R na kundi lake ndio chanzo cha mpasuko Huu?

  Upande wa pili wa studio atakuwepo Doyo Hassan Doyo kutoka Kambi iliyoenguliwa ya H.R kwa pamoja wakizungumzia majaaliwa ya CUF

  Karibuni katika mjadala tukiangazia nini majaaliwa ya upinzani Nchini kama CUF itameguka mapande mawili?

  Je Uhai wa Chama hiki bado upo kama awali?

  Ofisi ya Musoma ambayo kwa Kanda ya ziwa ni moja ya kati ya ngome yao kubwa imefungwa, inatoa ishara gani kwa chama hiki?

  Pia katika mjadala atashiriki Ansbert Ngurumo.

  Karibuni[/QUOTE]
   
Loading...