Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Kiongozi wa Baraza la Uongozi la CUF, Julius Mtatiro akiwa ameambatana na viongozi wenzake wamefika katika kituo Kikuu cha Polisi(Central) leo hii kuhoji kuhusu kuvamiwa na watu wenye silaha za jadi na mmoja akiwa na Bastola katika Mkutano wao.
Aidha katika Mkutano huo watu kadhaa wakiwemo waandishi wa habari walijeruhiwa vibaya na vifaa vya kufanyika kazi za habari vikiharibiwa vibaya.
=====
KIKAO NA KAMISHNA SIRRO...
Tumemaliza kikao na Kamishna Sirro (Mimi nikiambatana na Wakurugenzi wa kitaifa na Wajumbe wa Baraza Kuu wa CUF) ;
Kamishna Sirro ana roho ya kipekee sana ni Ofisa wa Polisi wa mfano, ametupokea na ametupatia ushirikiano mkubwa sana.
1. Tumempa barua rasmi na ushahidi wa matukio yote ya jinai ambayo chama kimetendewa tangu Agosti mwaka 2016 huku wafanya matukio hayo mabaya wakilindwa.
2. Tumezungumza kwa kina juu ya tukio la Uvamizi wa Vina Hotel na kutaka hatua zichukuliwe haraka.
3. Kamishna Sirro amesikitishwa sana kusikia kuwa viongozi wa chama wameitwa Magomeni ili wapatanishwe na wavamizi/majambazi/mungiki/mazombi. Sirro amekataa utaratibu huo na anasema kuwa makosa ya jinai hupelekwa mahakamani, hayasuluhishwi na Polisi.
4. Tumemkumbushia Kamishna matukio 13 ya jinai ambayo yametendwa na Lipumba na genge lake dhidi ya chama yakiwemo kuteka, kupiga, kuchoma visu, kuvamia n.k. tumemwambia kuwa katika matukio yote hayo, Lipumba na genge lake wameendelea kulindwa.
5. Tumemweleza Kamishna kuwa sisi tumeendelea kuwataka wanachama wawe watulivu ili tuone hatua za POLISI na kwamba hatua zisipochukuliwa, sisi tutachukua hatua.
6. Tumemkumbusha Kamishna Sirro kuwa sisi (chama) ni wengi kuliko Lipumba na Genge lake na kwamba wingi wetu ni silaha kubwa sana na kwamba tunao uwezo wa kuwasambaratisha mara 100 ikiwa tunataka. Lakini sisi bado ni wastahimilivu, tunataka kuona hatua zinachukuliwa na POLISI
7. Kamishna Sirro ameahidi kuwa anachukua hatua, ameelekeza mapungufu yetu, amekubali baadhi ya mapungufu yao na kutoa maelezo baadhi ya mambo muhimu. Hatuwezi kumhukumu Sirro kwa sasa, ila tutamhukumu tukishaona hakuna hatua zinazochukuliwa.
[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J