Mtatiro aishambulia Chadema Igunga

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Na Peter Mwenda, Igunga

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha mara moja kutangaza kudanganya wananchi wa Jimbo la Igunga kuwa chama hicho kisipewe kura kwa madai kuwa ni CCM-B.

"Mfumo wa uongozi wa CHADEMA hauna tofauti na ule wa CCM kwa sababu ule mfumo wa uongozi wa kupeana ulipo CCM ambao hautawahi kutokea CUF," alisema Bw. Mtatiro.

Alisema CHADEMA ilipata viti maalumu 36 na kushindwa kugawa kwa kuzingatia uwakilishi wa wananchi, bali walipendeleana wao kwa wao kwa kugawa viti 16 kwa mkoa wa Kilimanjaro pekee ambako viongozi wa chama hicho, walitoa kwa wake zao, wadogo zao na jamaa zao.

Alisema CUF Tanzania bara na Zanzibar walipata viti maalum kumi ambavyo ilivigawa bila upendeleo Dodoma (Bi. Moza Abeid), Mwanza (Bi. Mkiwa Kimwanga , Tanga Bi, Amina Mwidau, Mtwara (Bi. Clara Mwatuka, Kaskazini Pemba (Bi. Riziki Omar Juma), Mjini Magharibi Bi. Amina Amour na Kusini Magharibi (Bi. Thuwaiba Idris) ambao wanakilisha wa wananchi badala ya kulimbikizia kundi chache.

Alisema suala la Serikali ya Umoja Zanzibar ni mfumo uliofikiwa na Wazinzibari wenyewe ili kuondoa uhasama uliokuwepo, sasa inakuaje CHADEMA iseme CUF imeingia mkataba wa urafiki na CCM.

Katika mkutano huo mgombea ubunge wa CUF, Bw. Leopold Mahona alisema akichaguliwa atahakikisha wananchi wa Kata hiyo wataondokewa na kero zinazowasumbua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi.

SOURCE:MAJIRA
 
Uongo wako ndio hapo unapoingia utata mkubwa... Chadema ina wabunge 22 wa majimbo + 36 wanakuwa 58..!!. Aksante...

WanaJF tuendelee kuyapuuza haya magazeti uchwara kama Majira na huyu aliepost pia
 
Mtawatambuaje kama CUF nao wapo pasi na kulitaja Chama kubwa Chadema! Wanatafuta umaarufu kupitia Chadema ndio maana hawawataji CCM, TLP, UDP wala chama cha Dovutwa. Utadhani hivi vyama vingine havipo kwenye Uchaguzi Igunga.

CUF walishafulia zamani baada ya kuolewa na CCM a.k.a Mwarabu wao wa Suti 5.
 
Napita tu, nikiandika orodha ya wabunge Wachagga Mods wanafuta..
 
Mbona kama wengi wa hao ni Waisilamu na hakuna aliyezungumzia hilo..Mtatiro anafikiri uongozi kwa wananchi ni kama alivyokuwa anaongoza migomo DARUSO?
Na Peter Mwenda, Igunga

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha mara moja kutangaza kudanganya wananchi wa Jimbo la Igunga kuwa chama hicho kisipewe kura kwa madai kuwa ni CCM-B.

"Mfumo wa uongozi wa CHADEMA hauna tofauti na ule wa CCM kwa sababu ule mfumo wa uongozi wa kupeana ulipo CCM ambao hautawahi kutokea CUF," alisema Bw. Mtatiro.

Alisema CHADEMA ilipata viti maalumu 36 na kushindwa kugawa kwa kuzingatia uwakilishi wa wananchi, bali walipendeleana wao kwa wao kwa kugawa viti 16 kwa mkoa wa Kilimanjaro pekee ambako viongozi wa chama hicho, walitoa kwa wake zao, wadogo zao na jamaa zao.

Alisema CUF Tanzania bara na Zanzibar walipata viti maalum kumi ambavyo ilivigawa bila upendeleo Dodoma (Bi. Moza Abeid), Mwanza (Bi. Mkiwa Kimwanga , Tanga Bi, Amina Mwidau, Mtwara (Bi. Clara Mwatuka, Kaskazini Pemba (Bi. Riziki Omar Juma), Mjini Magharibi Bi. Amina Amour na Kusini Magharibi (Bi. Thuwaiba Idris) ambao wanakilisha wa wananchi badala ya kulimbikizia kundi chache.

Alisema suala la Serikali ya Umoja Zanzibar ni mfumo uliofikiwa na Wazinzibari wenyewe ili kuondoa uhasama uliokuwepo, sasa inakuaje CHADEMA iseme CUF imeingia mkataba wa urafiki na CCM.

Katika mkutano huo mgombea ubunge wa CUF, Bw. Leopold Mahona alisema akichaguliwa atahakikisha wananchi wa Kata hiyo wataondokewa na kero zinazowasumbua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi.

SOURCE:MAJIRA
 
Uongo wako ndio hapo unapoingia utata mkubwa... Chadema ina wabunge 22 wa majimbo + 36 wanakuwa 58..!!. Aksante...

WanaJF tuendelee kuyapuuza haya magazeti uchwara kama Majira na huyu aliepost pia

Mkuu mimi kuwahabarisha wanajamvi imekuwa kosa? Sikutaka kuedit chochote ili wanajamvi mumfahamu Mtatiro rangi zake zote
 
Inaelekea Mtatiro haijui CUF, Maana wenzake wote wamesalimu amri kuwa ccm-b, hata hoja zao bungeni ni kupinga CDM, yeye hataki kukiri.
 
Jamani ukweli siku zote huwa unauma. Mtatiro inamuuma sana lakini kwa sababu yupo kwenye ndoa sasa atafanyaje, tumshauri adai taraka ndo tumuelewe anachokitetea
 
hivi ni kweli kuwa cdm ni chama cha wachaga? nauliza maana hizi kashfa ni za muda sasa ni kweli wamegawana viti maalum vingi kwao? kama ni hivyo basi tuendako yatatokea matatizo makubwa kuliko yaliyopo sasa
 
Labda siku zote huwa wakumbana na mod mchaga...jaribu leo inawezekana alie zamu jukwaa la siasa ni mpema,lol!

Anaweza akawa Mpemba lakini akawa anatumika maana thread zetu wengine zinachinjiwa baharini hata kama hazina habari za chadema
 
Labda siku zote huwa wakumbana na mod mchaga...jaribu leo inawezekana alie zamu jukwaa la siasa ni mpema,lol!

Anaweza akawa mpemba lakini anatumika. Sisi wengine thread zetu hazina shutuma kwa kabila lolote na wala hazina uhusiano na chadema na bado zinachinjiwa baharini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom